Pamoja na udhaifu wake wote ilionao, ni kwanini CCM inaamini itatawala Tanzania milele?

Pamoja na udhaifu wake wote ilionao, ni kwanini CCM inaamini itatawala Tanzania milele?

Kuongoza nchi pekee ndiyo kigezo cha kupima uimara wa CCM? Hivi hatuwezi kusema kigezo cha kupima uimara wake kiwe ni jinsi gani wanaiongoza nchi!!??
Mbona tunaongozwa vizuri tu, kama kuna tatizo tunawakosoe wajirekebishe.
 
kinachowadangaya ni Dola, Vyombo vya ulinzi kuwa kwenye mikono yao wanahisi ndio watakuwa watawala milele
 
Hicho chama kinahusika kwenye kila madudu yanayotokea kwenye nchi yetu. Hakuna jambo baya kwa Watanzania ambalo halijatokana na CCM kuwa madarakani. Lakini CCM wenyewe kwa kujiamini kabisa wanasema kwamba watatawala Tanzania milele?

Haya ni maneno yanayoonesha CCM ina kiburi cha uzima kiasi kwamba inaamini mpaka kyama yenyewe itakuwa inaitawala Tanzania.

Au CCM inawaona watanzania ni mazezeta wasioweza kuwatoa madarakani?
Kitendo cha askari polisi na maafisa wa jeshi kuwa makada wa CCM kinyume na katiba isemayo hawapaswi kuwa wanachama wa vyama vya siasa ndio kiburi chao kinapoanzia.

Ila tukikomaa na kipata katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi haya yote yata koma na ccm itaondoka tuu
 
Hicho chama kinahusika kwenye kila madudu yanayotokea kwenye nchi yetu. Hakuna jambo baya kwa Watanzania ambalo halijatokana na CCM kuwa madarakani. Lakini CCM wenyewe kwa kujiamini kabisa wanasema kwamba watatawala Tanzania milele?

Haya ni maneno yanayoonesha CCM ina kiburi cha uzima kiasi kwamba inaamini mpaka kyama yenyewe itakuwa inaitawala Tanzania.

Au CCM inawaona watanzania ni mazezeta wasioweza kuwatoa madarakani?
Katiba mbovu, ujinga na upole wa watanzania ndio assets za CCM.
 
Mantiki kuu ya demokrasia inasema: “Watu hupata utawala wanaoustahili au wanaoupenda”.

Hivyo basi, CCM kutawala milele ni dhahiri kuwa ndicho chama kinachopendwa, kinachohitajiwa na kinachovumilika kwa Watanzania wengi. Huu ndio ukweli wenyewe.

Ikiwa si hivyo, basi idadi kubwa ya Watanzania ni mazuzu na wanafiki wakubwa! Btw mleta mada jitahidi pia kusoma comments za wachangiaji between the lines.

Manake hakuna mtu au chama kinachoweza kuwa madarakani muda mrefu bila “ridhaa” ya watawaliwa. Hakika siku ridhaa hiyo ikifa, CCM itasambaratika kwa njia saba!
 
Wanajiamini kupitia hii mifumo mibovu ya uchaguzi.
 
Ni kweli, na baadae akarudi CCM. Lakini CHADEMA ndiyo mwaka 2008 walimwita Lowassa Fisadi na kuweka hadharani ni kwa nini Lowassa ni fisadi.. Nakumbuka Mzee Nimrod Mkono alikuja na kuelezea kwa undani kimetokea nini baada ya Lowassa kuitwa Fisadi.

Baada ya Mzee Mkono kutoa maelezo hoja ikatokea kiasi alicholipwa Mzee Mkono na serikali kutokana na Kesi iliyosababishwa na Maamuzi ya Lowassa akiwa waziri wa maji. Kwa ivo suala la Lowassa kuitwa fisadi si la kuendelea. Mtu akiwa mwizi na akaacha wizi utaendelea kumwita mwizi? Ukiendelea kumwita mwizi mtu aliyeacha wizi, huo utakuwa ni uoenzi.

Lakini wakati CHADEMA wanamwita Lowassa fisadi wenye mwanachama wao wakati huo yaani CCM, walikuwa wanasemaje??
Shida yako ndio hiyo kila kitu wanachofanya Chadema unataka kujilinganisha na CCM, Chadema kikuwe kunahitajika kijitofautishe na CCM kimatendo
 
Agenda za Watanzania ni zipi??
Hakuna wapinzani. Watakapotokea CCM watabadilisha msimamo wao.

Upinzani utakaotokana na Watanzania, sio kikundi fulani cha watu wachache, Wenye interest zao na kulazimisha Agenda zao ndio ziwe Agenda za Watanzania.

Siku Watanzania watakapoungana kutetea maslahi yao ndio utakuwa Mwisho wa CCM. Kwa sasa No, waliopo Nje ni wabaya kuliko waliopo ndani.
 
Unaweza kufa ukamuacha mwenzako hai, hataweza kukumbusha.
Sijui kwa miaka 2000 ijayo. Lakini mimi na wewe tutakufa tutaiacha CCM madarakani, isipokuwa hivyo niite mbwa. Tunza hii comment siku upinzani wakishinda nikumbushe
 
Labda walidanganywa wana CCM waliokuwa mahasimu wa kisiasa wa Lowassa.
Wapinzani walimwita Lowassa fisadi na wakamweka kwenye list yao ya list of shame na wakasema Wana ushahidi wa ufisadi wake lakini wakaja kumteua kuwa mgombea wao wa Uraisi
 
Niko jirani zaidi na wewe ninayekuuliza sasa hivi.
Ajenda za Watanzania ni zipi?
Waulize watanzania waliopo Jirani na wewe
Kama huwaoni nenda kesho mitaani kawaskia.
Siwezi kuwajibia, wafuate uwaulize mwenyewe.
 
Tatizo uelewe wa Watanganyika ndiyo tatizo.
 
Tatizo uelewe wa Watanganyika ndiyo tatizo.
 
Back
Top Bottom