Pamoja na udhaifu wake wote ilionao, ni kwanini CCM inaamini itatawala Tanzania milele?

Kuongoza nchi pekee ndiyo kigezo cha kupima uimara wa CCM? Hivi hatuwezi kusema kigezo cha kupima uimara wake kiwe ni jinsi gani wanaiongoza nchi!!??
Mbona tunaongozwa vizuri tu, kama kuna tatizo tunawakosoe wajirekebishe.
 
kinachowadangaya ni Dola, Vyombo vya ulinzi kuwa kwenye mikono yao wanahisi ndio watakuwa watawala milele
 
Kitendo cha askari polisi na maafisa wa jeshi kuwa makada wa CCM kinyume na katiba isemayo hawapaswi kuwa wanachama wa vyama vya siasa ndio kiburi chao kinapoanzia.

Ila tukikomaa na kipata katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi haya yote yata koma na ccm itaondoka tuu
 
Katiba mbovu, ujinga na upole wa watanzania ndio assets za CCM.
 
Mantiki kuu ya demokrasia inasema: “Watu hupata utawala wanaoustahili au wanaoupenda”.

Hivyo basi, CCM kutawala milele ni dhahiri kuwa ndicho chama kinachopendwa, kinachohitajiwa na kinachovumilika kwa Watanzania wengi. Huu ndio ukweli wenyewe.

Ikiwa si hivyo, basi idadi kubwa ya Watanzania ni mazuzu na wanafiki wakubwa! Btw mleta mada jitahidi pia kusoma comments za wachangiaji between the lines.

Manake hakuna mtu au chama kinachoweza kuwa madarakani muda mrefu bila “ridhaa” ya watawaliwa. Hakika siku ridhaa hiyo ikifa, CCM itasambaratika kwa njia saba!
 
Wanajiamini kupitia hii mifumo mibovu ya uchaguzi.
 
Shida yako ndio hiyo kila kitu wanachofanya Chadema unataka kujilinganisha na CCM, Chadema kikuwe kunahitajika kijitofautishe na CCM kimatendo
 
Agenda za Watanzania ni zipi??
 
Unaweza kufa ukamuacha mwenzako hai, hataweza kukumbusha.
Sijui kwa miaka 2000 ijayo. Lakini mimi na wewe tutakufa tutaiacha CCM madarakani, isipokuwa hivyo niite mbwa. Tunza hii comment siku upinzani wakishinda nikumbushe
 
Labda walidanganywa wana CCM waliokuwa mahasimu wa kisiasa wa Lowassa.
Wapinzani walimwita Lowassa fisadi na wakamweka kwenye list yao ya list of shame na wakasema Wana ushahidi wa ufisadi wake lakini wakaja kumteua kuwa mgombea wao wa Uraisi
 
Niko jirani zaidi na wewe ninayekuuliza sasa hivi.
Ajenda za Watanzania ni zipi?
Waulize watanzania waliopo Jirani na wewe
Kama huwaoni nenda kesho mitaani kawaskia.
Siwezi kuwajibia, wafuate uwaulize mwenyewe.
 
Tatizo uelewe wa Watanganyika ndiyo tatizo.
 
Tatizo uelewe wa Watanganyika ndiyo tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…