Pamoja na uteuzi wa Dotto Biteko na Paul Makonda. Rais Samia bado hakubaliki kanda ya ziwa

Hata dhalimu mwenyewe hakuwa na ushawishi huo huko Kanda ya ziwa, ndio maana aliishia kupora uchaguzi. Isitoshe huyo mama hahitaji kura hata Moja kuwa rais wa nchi hii, ni suala la kuagiza vyombo vya Dola na time ya uchaguzi kumtangaza kwa kura azitakazo. Dhalimu magu ndio aliasisi box la kura kutoheshimiwa.
 
Ingekuwa Kiswahili cha Kenya wangwuliza, "Ati?"
 
Usilete chuki zako hapa. JPM alikubalika kila kona ya Tanzania. Hilo la wizi wa kura linategemea
Umesahau 2010 CHADEMA walipata kura nyingi tu ?
 
Umesahau mawasiliano mkuu
 
Acha kusema uongo. Kanda ya Ziwa Victoria siyo kama unavyofikiria wewe. Mwache mama achape kazi, na kazi iendelee. Kwani hao wawili uliowataja wanawakilisha jamii ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.
 
Mbona Mchato alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa sasa hivi hautumiki
 
Kanda ya ziwa ni jadi, kukubali kutawaliwa na mwanamke ni kipengele kikubwa - CCM bila kutumia mbinu za kigaidi kumnadi mama - wasahau.
Mama atapita kwa kishindo, garagabaho.
 
Mbona Mchato alijenga uwanja wa ndege wa kimataifa sasa hivi hautumiki
Chato ipo Zanzibar au Tanganyika!? Kama ipo Tanganyika wala sina shida! Kwa sababu fedha za Tanganyika zinajenga Tanganyika ila Je fedha zipi za Pemba zinajenga Geita!? Au fedha kiasi gani za Forodhani zinajenga Njombe? Ndo maana suluhu ni katiba mpya tu Mkuu
 
Labda wewe uliye kalia umbea nauzushi wako.lakini mamilioni ya watanzania wanampenda sana Rais Samia na wanaendelea kumuunga mkono kwa nguvu zao zote.
Rais mwenyewe anajua ni nani wanamwambia ukweli! Na anajua wale wanaompamba ili kutafuta teuzi wajipatie mkate wa kila siku.

Umesahau kuweka namba yako ya simu mkuu.
 
Mama Samia ni Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM.
Kwa sasa, bado wakati wa kampeni. Kazi inayotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha chama kinakubalika ili wakati wa uchaguzi wagombea wake wachaguliwe ambapo mgombea urais yupo ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…