Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Hakuna mtoto anaezaliwa akiwa panya road. Hili ni kundi la vijana ambao wamejitoa mhanga baada ya kushindwa kutofautisha faida kati ya kuishi na kufa. Ni kundi la vijana ambao hawana Cha kupoteza,
Mifumo yote ya kiuchumi imewafungia nje.

hakuna kijana anaependa kuzunguunga na mizigo kichwani na mikononi kwenda Huku na huko kuuzia watu bidhaa barabarani, kwenye mabaa, na kwenye magari kuuzia waheshimiwa wanaostarehe baa na kwenye ma V8 barabarani. Ni kazi ngumu sana sana sana kwa vijana.

sera zetu mbovu ndizo zinazozalisha panya road ambao tunaona dawa Yao ni kuwanyamazisha kwa risasi badala ya kuwapa chakula, mavazi, matibabu, malazi na elimu Bora na sahihi.

panya road wako kwenye kundi moja na wamachinga, madada poa, watumia dawa za kulevya, waokota chupa za plastics majalalani, wauza chuma chakavu na wanaobet kwenye mitandao. Wanabadilishana TU shughuli zao za kujioatia riziki.

badala ya kuwaua kwa risasi hebu Wana siasa kaeni kitako kwanza kutafakari kwa kina kuhusu chanzo na suluhisho la panya road ili mjue tatizo ni nini na wapi tumekosea badala ya kuhalalisha kuwamiminia risasi watoto wetu wenyewe kwa makosa yetu. Kuua mtanzania mmoja sio jambo la kujivunia.
Nakubaliana na hoja yako kuwa "panya road" (umachinga wa kupora mali) ni matokeo ya sera na mikakati ya kiuchumi.

Japo wapo WanaJF ukitaja Rais wa Awamu ya Tano unabebeshwa gunia la matusi, lakini ukweli unabaki kuwa msimamo wake kuhusu wafanya biashara ndogondogo, aka Machinga, uliwapa fursa vijana wasio na kazi ya kuajiriwa kufanya biashara ndogondogo wakaachana na "upanya road".

Serikali iliyoko madarakani, pamoja na nia njema ya kuweka utaratibu mzuri wa biashara ndogondogo, utekelezaji wa kuwaondoa barabarani umechukuliwa mapema kabla ya kuweka mazingira rafiki.

Niliwahi kushauri kuwa Halmashauri, kwa kushirikiana na VETA, kujengwe vibanda vya biashara kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu (km maegesho ya magari, vituo vya mabasi, masokoni, nk) na/au kutengenezwe vibanda vya kuhamishwa. Vibanda hivi viuzwe kwa Machinga kwa mkopo. Pamoja na kuweka miji safi, itawapa fursa ya kipato, wafanya biashara ndogondogo, ambao soko lao ni watu katika maeneo yao ya kazi. Hata Mama Ntilie wanaweza kutengezewa vibanda vya kuhamishwa na kukopeshwa vifaa vya kuhifadhi vyakula vyao visipoteze ubora wake.

Utawala wa Awamu ya Sita ulishutumiwa kwa kuwepo kundi la watu wasiojulikana. Hili kundi lililenga aina fulani ya watu katika jamii. Lakini kuwepo kwa "panya road" katika jamii imedhirika sasa athari zake ni kubwa sana maana wanavamia watu wa kipato cha chini. Hawathubutu kufanya maeneo ya wenye nacho au Viongozi Wakuu wa Serikali na Vyama vya Siasa.
 
Kundi la Vijana wanaojihusisha na Uhalifu Maarufu kama 'Panya road' wamevamia nyumba moja Kawe mtaa wa Mzimuni usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2022 na kujeruhi watu watano na Kumsababishia kifo Binti aliyetambulishwa kama Maria paschal Basso mwenye umri wa miaka 24.

Eneo la tukio na pameonekana uharibifu walioufanya kwenye nyumba ikiwemo kuvunja milango na kufanikiwa kuingia ndani, na kuwapora simu na fedha na kuharibu vitu mbali mbali ikiwemo TV.

Pia baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa huo ambao wameeleza kuwa tukio hilo lilifanyika usiku wa saa 8 na vijana wanaokadiriwa kufikia 30 waliokuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga.

Wahalifu hao waliwapiga na kuwajeruhi watu wanne ambapo wawili walikuwa mahututi na kati yao mmoja amefariki huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Serikali yoyote haiwezi kuajiri vijana wote,ila hakuna councelling yoyote ile iliyofanyika kwa baadhi ya vijana namna ya kuukabili uchumi nchini.Serikali inasema wajiajiri lakini hawana elimu na mitaji
 
Serikali yoyote haiwezi kuajiri vijana wote,ila hakuna councelling yoyote ile iliyofanyika kwa baadhi ya vijana namna ya kuukabili uchumi nchini.Serikali inasema wajiajiri lakini hawana elimu na mitaji
Matatizo yote haya ya vijana kukosa fursa ni kutokana na kuua sekta binafsi, mataifa yote yaliyoendelea yamefanikiwa kutokana na kukua kwa sekta binafsi, kutegemea serikali ndo ifanye biashara na kutoa ajira ni kujidanganya. Haya tuliyashuhudia kwa mashirika ya ndege kama fast jet kuwekewa mizengwe na kuondoka ili watu wapate sifa ya kufufua shirika la ndege la umma ambalo limeishia kuwa mzigo kwa walipa kodi.​
 
Huwezi kuitenga CCM na Panya road, maana panya road ni tunda la sera na Ilani mbaya kwa vijana. Wabunge wetu wamepitisha mambo ambayo yanaongeza panyaroad mitaani. Yako wapi mashamba makubwa (plantations) ya mkonge, ngano, mpira, kahawa, chai, kokoa, mpunga, pamba, mifugo na viwanda vinavyochakata mazao yake ambayo yanazoa vijana wengi kuwapitia ajira huko? viko wapi vyuo vya kati vya kuwapatia vijana ujuzi wa kujiajiri? iko wapi mikopo ya kuwapatia vijana mitaji ya kujiajili wenyewe? ziko wapi pembejeo za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa vijana, yako wapi masoko ya kuuza mazao ya kazi za vijana? Wabune badala ya kujadili maswali haya wanajadili namna ya kuwamiminia risasi watoto ambao ni wahanga wa sera zetu. Nani hajui kama kosa la kuiba ni ama kufungwa au kupigwa risasi au kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali? panya road wanayajua yote haya lakini waechagua kufa kwa risasi kuliko kufa kwa njaa kwenye mapagale wanakolala kwa umaskini.
 
Panya road ni mradi wa watu wazito, vinginevyo wametoa wapi magari ya kuwakimbiza baada ya tukio?
wakati watu mkihamisha macho yenu kwenye panya road kuna watu wanatumia mwanya huo kufanya mambo makubwa ya ajabu. mara zote jifunze kuangalia nyuma unapokwenda mbele. tunahamishwa akili zetu zitoke kwenye tozo na bei kupanda
 
Hizi op zinafanyikaga kimya kimya tu

Watu wanamalizwa

Ova
Na hilo ndo swala zuri...
Serikali za mitaa zinalea sana huu upuuzi

Fukwe za bahari zimejaa vijana wasio na kazi, wao kila siku baharini
 
Sisi tumechoma moto mmoja usiku wa kuamkia leo wengine walikimbia n wakati sasa wa wananchi kupeana mbinu za kiulinz pale panapotokea uhalifu

Ss tuna mbinu zetu za kiulinz ambazo n ngumu kuzjua kwa mgen au mwiz

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwanza inatakiwa tujue chimbuko la hawa panya Road ni nini? I Kuwaua wala siyo solution kwa sababu wao wamesha jidhiri kwa lolote.
 
Kwanza inatakiwa tujue chimbuko la hawa panya Road ni nini? I Kuwaua wala siyo solution kwa sababu wao wamesha jidhiri kwa lolote.
Kwa Hiyo wananchi wama wao wakae kimya wauawe na kuibiwa mali zao halali.
Hapana Kwa kweli kama panya road akikamatwa ready handed ni halali kabisa kuuawa ili kuwamaliza.
Binadamu ni kiumbe Bora akifuata Sheria na kutenda matendo mwema.
BInadamu akiawa mhalifu ni mbaya kuliko mnyama wa porini hivyo hapaswi kuhurumiwa hata chembe mana anakua ni tatizo kubwa sana kwenye jamii
 
Back
Top Bottom