mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Nakubaliana na hoja yako kuwa "panya road" (umachinga wa kupora mali) ni matokeo ya sera na mikakati ya kiuchumi.Hakuna mtoto anaezaliwa akiwa panya road. Hili ni kundi la vijana ambao wamejitoa mhanga baada ya kushindwa kutofautisha faida kati ya kuishi na kufa. Ni kundi la vijana ambao hawana Cha kupoteza,
Mifumo yote ya kiuchumi imewafungia nje.
hakuna kijana anaependa kuzunguunga na mizigo kichwani na mikononi kwenda Huku na huko kuuzia watu bidhaa barabarani, kwenye mabaa, na kwenye magari kuuzia waheshimiwa wanaostarehe baa na kwenye ma V8 barabarani. Ni kazi ngumu sana sana sana kwa vijana.
sera zetu mbovu ndizo zinazozalisha panya road ambao tunaona dawa Yao ni kuwanyamazisha kwa risasi badala ya kuwapa chakula, mavazi, matibabu, malazi na elimu Bora na sahihi.
panya road wako kwenye kundi moja na wamachinga, madada poa, watumia dawa za kulevya, waokota chupa za plastics majalalani, wauza chuma chakavu na wanaobet kwenye mitandao. Wanabadilishana TU shughuli zao za kujioatia riziki.
badala ya kuwaua kwa risasi hebu Wana siasa kaeni kitako kwanza kutafakari kwa kina kuhusu chanzo na suluhisho la panya road ili mjue tatizo ni nini na wapi tumekosea badala ya kuhalalisha kuwamiminia risasi watoto wetu wenyewe kwa makosa yetu. Kuua mtanzania mmoja sio jambo la kujivunia.
Japo wapo WanaJF ukitaja Rais wa Awamu ya Tano unabebeshwa gunia la matusi, lakini ukweli unabaki kuwa msimamo wake kuhusu wafanya biashara ndogondogo, aka Machinga, uliwapa fursa vijana wasio na kazi ya kuajiriwa kufanya biashara ndogondogo wakaachana na "upanya road".
Serikali iliyoko madarakani, pamoja na nia njema ya kuweka utaratibu mzuri wa biashara ndogondogo, utekelezaji wa kuwaondoa barabarani umechukuliwa mapema kabla ya kuweka mazingira rafiki.
Niliwahi kushauri kuwa Halmashauri, kwa kushirikiana na VETA, kujengwe vibanda vya biashara kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu (km maegesho ya magari, vituo vya mabasi, masokoni, nk) na/au kutengenezwe vibanda vya kuhamishwa. Vibanda hivi viuzwe kwa Machinga kwa mkopo. Pamoja na kuweka miji safi, itawapa fursa ya kipato, wafanya biashara ndogondogo, ambao soko lao ni watu katika maeneo yao ya kazi. Hata Mama Ntilie wanaweza kutengezewa vibanda vya kuhamishwa na kukopeshwa vifaa vya kuhifadhi vyakula vyao visipoteze ubora wake.
Utawala wa Awamu ya Sita ulishutumiwa kwa kuwepo kundi la watu wasiojulikana. Hili kundi lililenga aina fulani ya watu katika jamii. Lakini kuwepo kwa "panya road" katika jamii imedhirika sasa athari zake ni kubwa sana maana wanavamia watu wa kipato cha chini. Hawathubutu kufanya maeneo ya wenye nacho au Viongozi Wakuu wa Serikali na Vyama vya Siasa.