Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Nawapa pole wanawake wote wa Dar na nawaombea wawe salama kutokana na wimbi la panyaroad.

Upande wa wanaume nawaombea pia lolote liwakute.
Huko Dar mnakojifanyaga mko busy na kusaka pesa msipoweka ulinzi shirikishi wa sungusungu mtakatwa mapanga daily maana Polisi hawawezi kuwepo kila sehemu..

Cha ajabu eti kuna ulinzi shirikishi,hapo Serikali inatakiwa iwaruhusu vikundi vya ulinzi kufanya doria rasmi usiku vinginevyo hakuna suluhisho..

Maana Hata ukifanya oparesheni za kuna siku wataibuka tena..
 
Kundi la Vijana wanaojihusisha na Uhalifu Maarufu kama 'Panya road' wamevamia nyumba moja Kawe mtaa wa Mzimuni usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2022 na kujeruhi watu watano na Kumsababishia kifo Binti aliyetambulishwa kama Maria paschal Basso mwenye umri wa miaka 24.

Eneo la tukio na pameonekana uharibifu walioufanya kwenye nyumba ikiwemo kuvunja milango na kufanikiwa kuingia ndani, na kuwapora simu na fedha na kuharibu vitu mbali mbali ikiwemo TV.

Pia baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa huo ambao wameeleza kuwa tukio hilo lilifanyika usiku wa saa 8 na vijana wanaokadiriwa kufikia 30 waliokuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga.

Wahalifu hao waliwapiga na kuwajeruhi watu wanne ambapo wawili walikuwa mahututi na kati yao mmoja amefariki huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Polisi wanajua kuwaumiza Chadema, basi
 
Hivi wakati wanavunja milango huwa haitoi kelele? tujitahidi kuwa na namba za majirani pamoja na viongozi wa mitaa
 
Polisi sasa wafanye majukumu yao ya msingi ya kulinda wananchi dhidi ya vitendo hivi vya kihalifu, haya mambo yakiachwa yaendelee huko mbeleni mitaa itakuwa haikaliki......uhalifu wa kudhuru watu na kupora itakuwa ni sehemu ya maisha.
 
Serikali pamoja na kukusanya tozo nyingi Kwa raia bado inashindwa kutulinda na panya road.

Tozo Zetu mnaiba basi mtulinde na panya road.

Nipo hapa nauguza majeraha ya Jana.
Kipindi cha Nyerere tulikuwa na usemi Kila raia ni Askari lakini kimekuja hiki kizazi cha chips mayai imekuwa tabu tupu vitoto vitano vikiwa na mapanga na bisibisi vinaweza kufunga mtaa wote mkajinyeanyea humo ndani hata wa kumsaidia mwenzie asiwepo

Pole mkuu ndio ukubwa kama nyinyi wenyewe majilani mnashindwa kusaidiana polisi tutawalaumu bule
 
Back
Top Bottom