Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Kipindi cha Nyerere tulikuwa na usemi Kila raia ni Askari lakini kimekuja hiki kizazi cha chips mayai imekuwa tabu tupu vitoto vitano vikiwa na mapanga na bisibisi vinaweza kufunga mtaa wote mkajinyeanyea humo ndani hata wa kumsaidia mwenzie asiwepo

Pole mkuu ndio ukubwa kama nyinyi wenyewe majilani mnashindwa kusaidiana polisi tutawalaumu bule
Mzee Wacha ujinga. Watu zaidi ya 40 Wenye mapanga unazani Rahisi hivyo.
 
Kundi la Vijana wanaojihusisha na Uhalifu Maarufu kama 'Panya road' wamevamia nyumba moja Kawe mtaa wa Mzimuni usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2022 na kujeruhi watu watano na Kumsababishia kifo Binti aliyetambulishwa kama Maria paschal Basso mwenye umri wa miaka 24.

Eneo la tukio na pameonekana uharibifu walioufanya kwenye nyumba ikiwemo kuvunja milango na kufanikiwa kuingia ndani, na kuwapora simu na fedha na kuharibu vitu mbali mbali ikiwemo TV.

Pia baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa huo ambao wameeleza kuwa tukio hilo lilifanyika usiku wa saa 8 na vijana wanaokadiriwa kufikia 30 waliokuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga.

Wahalifu hao waliwapiga na kuwajeruhi watu wanne ambapo wawili walikuwa mahututi na kati yao mmoja amefariki huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Wazungu wametumia panya road miaka yote(wezi kwa njia za uchochoroni, rushwa, udhalimu, uhasama, na mpaka uuaji wa kikatili).

Wacheni Lugha za Kimbari.
 
hawa mapanya kwa nini wanatushinda wakati wanaishi mitaani mwetu.

Nashauri Jeshi letu la Polisi lifanye operesheni kabambe ya mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyuma, vijiwe vyote vya uvutaji bangi vitokomezwe.

Ikishindikana basi dawa yao ni moto tu.
 
Serikali pamoja na kukusanya tozo nyingi Kwa raia bado inashindwa kutulinda na panya road.

Tozo Zetu mnaiba basi mtulinde na panya road.

Nipo hapa nauguza majeraha ya Jana.
Watu wenyewe ni hawa akina masauni,Mwigulu , january... hapa ni mwanzo tu, wameshajua kuwa sasa hawawezekani, watatenda mauaji makubwa some times to come soon!
 
Kwamba walinda usalama wa raia na mali zao wako likizo wote
 
Kwa yaliyotokea Kawe na Temeke hatuna namna zaidi ya kumuombea Mungu wa mbinguni atupe ulinzi wake

Bwana usikie kuomba kwetu!

Hii kazi kuna watu ni kazi zao wanalipwa mishahara na wengine kodi hawalipi. Kumpa mungu kazi hii tena itakuwa ni kumkosea sana.

Hawa wenye dhamana ndiyo wa kuanza nao.
 
Back
Top Bottom