Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Kwa yaliyotokea Kawe na Temeke hatuna namna zaidi ya kumuombea Mungu wa mbinguni atupe ulinzi wake

Bwana usikie kuomba kwetu!
Wewe Jo Haina mjukuu panya road kweli,kwani SI kumwomba Mungu TU,ila inahitajika bidii binafsi Ili Mungu akuongoze uweze fikia malengo au kufanikiwa,ila unapokuwa mvivu na kupenda maisha rahisi bila jasho matokeo yake ndio hayo, bahati mbaya utakuta hata msomi anachagua afanye nini asifanye nini,akitarajia kile alicho fikiria kichwani, mwake itamvusha, matokeo yake ndio Yale takwimu zinasema vichaa wengi wakati ni kushindwa kujisimamia na kijiongoza,hivyo kupelekea kukosekana utulivu wa akili,hata kuathiri afya,na kupelekea haja ya Tina ya kuirejesha akili katika Hali yake,kuweza kujitambua,na kuweza kuyatambua mazingira uanayo mzunguka mtu.
 
Walipotushinda wazungu ni hapa ... Instead of kupambana kutatua matatizo yetu tumekaa tukisubiri Mungu atende ..

Pambanieni mali zenu na Maisha yenu ...

He doesn't give a damn about y'all mfs
 
Hivi polisi na vyombo vya ulinzi wameshindwa kuwashibiti hawa

Ova
Nashangaa wanaojiita usalama wa Taifa sijui wapo kukusanya taarifa gani za kiusalama,intelijensia ya polisi nayo ipo lakini hakuna chochote.
 
Polisi sasa wafanye majukumu yao ya msingi ya kulinda wananchi dhidi ya vitendo hivi vya kihalifu, haya mambo yakiachwa yaendelee huko mbeleni mitaa itakuwa haikaliki......uhalifu wa kudhuru watu na kupora itakuwa ni sehemu ya maisha.
Baada ya kukaribia kufilimbwa na panya road tumeanaza kuona umuhimu wa polisi.[emoji23]
 
Silaha wametutaka turudshe na kutulinda hawatulindi
 
Polisi tumeanza kuona umuhimu wenu.[emoji134]

Swali:Hiyo mitaa inayovamiwa na panya road haikaliwa na hawa ndugu zetu polisi,wajeda..iweje mtaa utekwe bila jamaa kudhibitiwa?
 
Ndugu wanajamii hapa Dsm pamekuwa na matukio makubwa sana ya watoto WADOGO sana polisi waliwapa jina Panya road Hawa watoto WETU kwakuwa wameshindwa kuishi na jamii nyingine kwa udhaifu wa wazazi au jamii husika Sasa polisi Tena jeshi kubwa KUSHINDWA na kundi la watoto waliohutimu darasa la Saba na kutawala vyombo vyote vya habari ni kuonsha udhaifu mkubwa kwa Hili jeshi hasa kwa Dsm mkuu wa polisi ameshindwa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Serikali ilegeze sheria za kumiliki bunduki.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Maria Basso (24) amefariki dunia baada ya watu zaidi ya 10 kuvamia nyumbani kwao Kawe Mzimuni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 14, 2022 na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Wiliam Mkonda imedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Septemba 14 saa 2:30 usiku maeneo ya Kawe mzimuni, kikundi cha wahalifu wakiwa na silaha za jadi, walivamia nyumbani kwa jina Paschal Basso (56).

Amesema baada ya kuvamia nyumba hiyo yenye vyumba 15, walivunja milango na kupora fedha, simu za mkononi, kujeruhi watu watatu na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Paschal (24).

"Tukio walilofanya wahalifu hawa ni baya na linalotakiwa kulaaniwa na kukemewa na Mtanzania yoyote anayechukia uhalifu kwa watu kama hawa ambao hawataki kutumia njia halali za kujitafutia kipato," amesema Kamanda Mkonda.

Kufuatia tukio hili, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawasaka wahalifu wote waliohusika katika tukio hilo pamoja na kuimarisha doria za miguu na mgari katika maeneo yote.

“Tunaendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika kukabiliana na uhalifu wa aina hii katika maeneo yao,” amesema.

Akizungumza na Mwananchi, shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni jirani Benitto Edward amesema usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba usiku, kundi la vijana zaidi ya 20 wakiwa na mapanga, visu, bisibisi na marungu walivamia nyumba hiyo iliyopo Kawe Maringo.

“Baada ya kuvamia nyumba hiyo walianza kuvunja mlango mmoja baada ya mwingine wakiamrisha kupatiwa vitu mbalimbali kama vile simu, fedha na kompyuta mpakato (laptop),” amesema Edward.

Matukio ya watu kuvamiwa yameendelea kushika kasi na kutishia usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo wiki moja tu tangu, Panya Road kuibuka tena na kuvamia nyumba 24 za wapangaji mtaa wa Kabaga Kinyerezi.

Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Kamfipo Gidion, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Maria alifariki alfajiri ya kuamkia jana kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mwananchi
 
Nawapa pole wanawake wote wa Dar na nawaombea wawe salama kutokana na wimbi la panyaroad.

Upande wa wanaume nawaombea pia lolote liwakute.
"..hilo nalo kalitazameni...". amesikika mama mmoja akitoa agizo kwa sauti ya upole.
 
Magu alikuwa anakwambia "I wish ningekuwa IGP". Yani madogo wanatamba tu mjini na serikali imechemka imebaki kuwatqzama tu.

Madogo ni wahuni wamepinda lazima washughulikiwe kihuni kwa ukatili wa hali ya juu.
 
Polisi CCM hawana ubavu Kwa panya rod ,lakini wakisikia hata Saa nane usiku CHADEMA wanaongea utaona wanamabomu nk
 
Back
Top Bottom