Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Maria Basso (24) amefariki dunia baada ya watu zaidi ya 10 kuvamia nyumbani kwao Kawe Mzimuni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 14, 2022 na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Wiliam Mkonda imedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Septemba 14 saa 2:30 usiku maeneo ya Kawe mzimuni, kikundi cha wahalifu wakiwa na silaha za jadi, walivamia nyumbani kwa jina Paschal Basso (56).

Amesema baada ya kuvamia nyumba hiyo yenye vyumba 15, walivunja milango na kupora fedha, simu za mkononi, kujeruhi watu watatu na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Paschal (24).

"Tukio walilofanya wahalifu hawa ni baya na linalotakiwa kulaaniwa na kukemewa na Mtanzania yoyote anayechukia uhalifu kwa watu kama hawa ambao hawataki kutumia njia halali za kujitafutia kipato," amesema Kamanda Mkonda.

Kufuatia tukio hili, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawasaka wahalifu wote waliohusika katika tukio hilo pamoja na kuimarisha doria za miguu na mgari katika maeneo yote.

“Tunaendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika kukabiliana na uhalifu wa aina hii katika maeneo yao,” amesema.

Akizungumza na Mwananchi, shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni jirani Benitto Edward amesema usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba usiku, kundi la vijana zaidi ya 20 wakiwa na mapanga, visu, bisibisi na marungu walivamia nyumba hiyo iliyopo Kawe Maringo.

“Baada ya kuvamia nyumba hiyo walianza kuvunja mlango mmoja baada ya mwingine wakiamrisha kupatiwa vitu mbalimbali kama vile simu, fedha na kompyuta mpakato (laptop),” amesema Edward.

Matukio ya watu kuvamiwa yameendelea kushika kasi na kutishia usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo wiki moja tu tangu, Panya Road kuibuka tena na kuvamia nyumba 24 za wapangaji mtaa wa Kabaga Kinyerezi.

Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Kamfipo Gidion, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Maria alifariki alfajiri ya kuamkia jana kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mwananchi
This is sad. Poleni sana
 
Ningekuwa Rais ningemfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa DSM, tena ningetegea yupo kwenye ziara ndio nitengue uteuzi wake.

Na ningetuma watu wakamnyang'anye gari katikati ya ziara.

Huwezi kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wa Mkoa halafu Panya road wanakushinda na unaendelea kubaki ofisini.

Hii ni mara ya pili watu wanakatwa mapanga na hao panya road. Nimeanza kuona ni kwanini Magufuli alikuwa anatumbua hawa watu, hawatimizi majukumu yao kwa usahihi.
 
Serikali inawa chekea sana hawa watoto , ongoza nchi kwa mkono wa chuma uone kama kuna taka taka yoyote inayoitwa panya road itatokea.

Kamata wote vulisha nguo wazamishe kwenye tanuru la moto waungue mpaka wabaki majivu uone kama kuna kikundi chochote cha kishenzi kitaji tokeza.
 
Tatizo la maisha ya nyuma ya Keyboard unaweza kuwa wewe ndio Makonda mwenyewe au una maslahi binafsi na ulichoshauri.
CCM awamu 06 imeshindwa kulinda usalama wa raia na malizo iondoke by 2025 kwa lazima , hii ingetokea enzi za JPM kuna watu ndani ya WIZARA husika wangeshawajibika mpaka sasa.......kwa sasa hakuna accountabilty kabisa .....
 
Ningekuwa Rais ningemfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa DSM, tena ningetegea yupo kwenye ziara ndio nitengue uteuzi wake.

Na ningetuma watu wakamnyang'anye gari katikati ya ziara.

Huwezi kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wa Mkoa halafu Panya road wanakushinda na unaendelea kubaki ofisini.

Hii ni mara ya pili watu wanakatwa mapanga na hao panya road. Nimeanza kuona ni kwanini Magufuli alikuwa anatumbua hawa watu, hawatimizi majukumu yao kwa usahihi.
Kutwa yupo Bunju na Mabwepande kutatua migogoro ya Ardhi wakati DC na DED wapo.Makalla nilimdharau alipomshauri Rais ajenge soko la Machinga Jangwani!
Na leo nimemuona Bunju anawaambia Wananchi waliovamia eneo la klabu ya Simba wahame🤣🤣
 
CCM awamu 06 imeshindwa kulinda usalama wa raia na malizo iondoke by 2025 kwa lazima , hii ingetokea enzi za JPM kuna watu ndani ya WIZARA husika wangeshawajibika mpaka sasa.......kwa sasa hakuna accountabilty kabisa .....
Hi nchi bila mkono wa chuma kweli haiwezi kwenda kabisa , watamsumbua tuu mama yetu apate presha bure ......
 
Hao sio panya road ni wafuasi wa Magufuli wanamkwamisha Samia ili ionekane kwa miaka mitano ya JPM kwanini hali ilikuwa shwali alisikika mlevi mmoja akisema!
ndo wafanyie tukio nyuma ya kituo cha polisi , au polisi pia ni wafuasi wa JPM , kwahiyo Mama hawez kuwadhibit kisa ni wafuasi wa JPM ?
 
Makonda hapana...jeshi la police lifanye kazi yake ipasavyo tu
 
Kutwa yupo Bunju na Mabwepande kutatua migogoro ya Ardhi wakati DC na DED wapo.Makalla nilimdharau alipomshauri Rais ajenge soko la Machinga Jangwani!
Na leo nimemuona Bunju anawaambia Wananchi waliovamia eneo la klabu ya Simba wahame🤣🤣
Jiji limemshinda. Kwanza hata sijui mamlaka ya uteuzi iliona nini kwake hadi ikampa DSM.
Kama kuna wakuu wa Mikoa wa kufuta kazi, yeye anapaswa kuwa namba moja.
 
Kupatwa kwa Uandishi. Basi badili heading tu nayo iwe na neno Chadema ili kichefuchefu chako kipone
 
Polisi wana akili ? , makonda licha ya kuitwa zero brain lakini he was somehow smart kuliko polisi, alijua kuwa control, watu hata gari zao walishindwa ku repair
Kwahiyo Makonda ndiye alitoa pesa za kurepair?? Au alitumia tu ubabe kwa wenye Garage pamoja na kukomba pesa za wafanyabiashara kwa kisingizio anatengeneza magari ya polisi
 
Back
Top Bottom