Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
mimi swala zima la kuwepo kwa haki za binadamu sijawahi kulielewa!

watu kama hawa wakikamatwa mashirika ya haki za binadamu nazo zinakuja juu wasiumizwe kwa kuwa zinatambua haki zao! Je, wale wanaopata shida kutokana na "shughuli" zao inakuwaje?

ni mwendo wa tairi, mafuta ya taa na kiberiti tu huko mtaani siku hizi hata kama mtu kaiba sukari!

Leo sukari, kesho?
 
Kuzuia vibaka ni rahisi sana lakini Kuna watu walioko juu wananufaika na uhalifu uwe wizi wa Mali za umma,uwe ugaidi ,uwe ni utakatishaji wa fedha, uwe ni uuzaji wa madawa ya kulevya . Uhalifu wowote una kundi la wanufaikaji? Nchi yenye ardhi kubwa namna hii lakini Kuna watu wanakaa mjini hawana kazi Vijana wakubwa.
Tunatumia Sheria za kijinga za Ulaya wanaoishi kwenye barafu!!! Ujinga Gani huu.
Fanya misako ya kitaifa nyumba Kwa nyumba kijana yeyote asiyesoma mwenye zaidi ya miaka 19 kamata peleka kwenye mapori chini ya usimamizi wa Jeshi la kujenga Taifa na Magereza na migambo . Jenga Kotazi za kuishi anzisha Kilimo Cha lazima . Weka maji ya kumwagilia kutegemea na mkoa . Kama ni Mtwara peleka Mtwara Lima korosho kama ni Tanga Lima mkonge,machungwa , mahindi ,Fuga lazima akizingua piga chuma tupa kule, Kama ni Singida Lima alizeti, kama ni Tabora Fuga Nyuki ,shinyanga Pamba, Mbeya Lima viazi ,mpunga , Moshi peleka Lima kahawa Kijiji au peleka Handeni kama Wamasai. Nchi hii ni ujinga mkubwa sana kuwaacha Vijana wasio na kazi mijini wakati ardhi ipo Kuna na tuna majeshi yasiyo na vita. JKT isiwe ni sehemu ya kunufaisha wachache kuwalimia mashamba yasiyo na tija Kwa Vijana. Kazi ya JKT iwe ni kuanzisha mashamba na kuyasimamia mwanzo mwisho mpaka yatoe viwanda na kuajiri hao Vijana kama wakati wa mkoloni.
Unaanzisha Shamba la Zabibu unaanzisha kiwanda Cha mvinyo unawaajiri na kuwalipa Vijana hao sio huu ujinga wa kuwagalagaza Vijana kwenye matope na Kilima mahindi halafu wanakula kama wafungwa miaka miwili wanaruji nyumbani eti hakuna ajira. Natamani hii nchi ningeipewa miaka kumi. Afrika nzima na Asia wangekuja Kununua kila kitu hapa hapa kuanzia vyakula na Mali ghafi. Hapo hatujagusa viwanda vya saruji. Ningehakikisha mpaka Huko mitaani wanatengengeza saruji kwenye viwanda vidogo vidogo Kwa ajili ya maskini Kununua sementi za viwango vya chini nyingine ingeuzwa nje. Hakuna bidhaa ingetoka nje kama inapatikana hapa au kulimwa hapa.

Wanasiasa wametuchelewesha Kwa kuendekeza siasa. Wapiga kura wangu ndio lugha yao. Siku hizi hakuna Tena Sheria ya kuwalazimisha watu kufanya kazi . Vijana Wana nguvu lakini wamekaa vijiweni kuendesha boda boda TU badala ya kuwatawanya wakazalishe Huko vijijini kama mpango kamili wa kuanzisha viwanda. Ukianzisha Shamba la mahindi la Vijana zaidi ya mia mbi unaweka na mashine za kusaga na kukoboa. Magari ya kusafirisha ,nyumba za kuishi ,wanasimamiwa Kijeshi kwa lazima baada ya miaka 10 wanakua ni watu huru wanaoajiriwa kuzalisha. Kuna nchi Ulaya zinaendesha uchumi wake Kwa kuzalisha magogo ya mbao TU. Yani hawana ardhi ya Kilimo zaidi ya kupanda miti na miti inachukua muda mrefu kukua Kwa sababu ya barafu. Sisi ardhi nzuri lakini wapumbavu wanaweka mabilioni ya pesa wanakopesha Vijana bodaboda badala ya kuwapeleka shambani kwa fedha hizo wakazalishe chakula. Leo hii Mchele unapanda Bei badala ya kushuka. Nafaka kama mahindi yanapanda Bei badala ya kushuka. Mahindi ,Mchele ,n.k. ni vyakula pia vya wanyama. Mchele na mahindi vinatakiwa biwe Bei Chee Ile mpaka nguruwe wale na Kuku na Ng'ombe na hatimaye binadamu ale mlo Bora wa nyama ,mayai, maziwa na mifugo ya samaki. Leo mwafrika chakula chake ni nafaka tuu muda wote na Tena mlo mmoja Kwa siku na kwa Bei juu.
Angalau Huseni Bashe anaweza akaja kuwa Waziri Mkuu Bora kabisa endapo nitafanikiwa kuwa mfalme wa Tanganyika Territory baada ya makia Elizabeth.
 
Tukisema hayati kuna mambo aliyaweza sana tunaitwa SUKUMA GANG basi tuache yapite maana wao wanaishi masaki sio mbagala wanaona hadithi tu...

Hayati alikuwa mtu haswaa.
 
Wenyewe wanapendelea zaidi barabarani. Huko ndiko Kuna za kubrashia viatu.
Kinana mbona hasemi kitu kuhusu polisi kukabili panya rodi au kwasababu panya rodi siyo kero kwenye matembezi yake kama ilivyokuwa kwa trafiki barabarani.
 
Hii ishu wakabidhiwe wananchi tuu, wakiuawa kama kumi hv lazima wapoe
 
Mpuuzi Makonda angekuwa nchi za watu wenye akili angekuwa jela, sijawahi kuona mtu mpuuzi na mshamba kama Makonda, alikuwa na kila sifa ya madikteta uchwara wengine waliowahi kutokea Africa na alikuwa mwizi pia
 
Watakuwepo ila tatizo wanavaa mlegezo, mlegezo na mwizi/jambazi huwa havipatani.
Huko wanapoonewa na hao panyaroad hakuna ulinzi, sasa sehemu ambayo haina ulinzi si wanavamiwa mda wowote tu.. ulinzi unaanza na wananchi ulinzi sio polisi tu tatizo watu wamekariri kwamba ulinzi ni polisi au jeshi tu la hasha ulinzi unaanza na wananchi kulindana wao kwa wao
 
Vyombo vya ulinzi kama vile hawana habari!
Mbona matukio ya kisiasa wanayatolea macho
Alafu huyu mkuu wa mkoa mambo kama haya wala hayapi kipaumbele
Yeye matukio ya wasanii,mara sijui mihogo nyama choma coco beach

Blshyt...

Ova
 
Watu wamemfuata mwali wao mnaanza kusingizia panyaroad, teteaneni nyinyi kwa nyinyi ukisikia kelele toka nje mbio mbio ukiwa umebeba kitu cha kujihami nenda kawasaidie wenzio jirani yako ni ndugu yako sio unasikia kelele wewe unajifungia ndani eti unasubiri polisi waje huku watu wanaumizwa tu kwa kukatwakatwa na mapanga wengine mpaka wanauwawa alafu wewe unasubiri uje uilaumu serikali tu kwa jambo ambalo ungeweza kulitatua kwenye mtaa wako au kijiji chako yaan mnasubiri serikali ije iwafundishe jinsi ya kulindana nyinyi kwa nyinyi?
 
Back
Top Bottom