Panya Road waua mtu mmoja Kawe na kujeruhi wengine watatu
Wajaribu kutrace simu .. akikamatwa mmoja tu .. .. washakwisha Ila ulinzi shirikishi uimarishwe..wakirudi na hasira zao..mtaa hautakalika..

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Police warudi kwenye majukumu yao ya msingi. Haiwezekani mtaani hamna police wa doria ila barabarani kila baada ya kilometa moja au mita mitatu unakuta wamerundikana.
 
Police hawawajibiki.ondoa IGP na kamanda wa police Dsm, hawawajibiki.
 
Ndugu wanajamii hapa Dsm pamekuwa na matukio makubwa sana ya watoto WADOGO sana polisi waliwapa jina Panya road Hawa watoto WETU kwakuwa wameshindwa kuishi na jamii nyingine kwa udhaifu wa wazazi au jamii husika Sasa polisi Tena jeshi kubwa KUSHINDWA na kundi la watoto waliohutimu darasa la Saba na kutawala vyombo vyote vya habari ni kuonsha udhaifu mkubwa kwa Hili jeshi hasa kwa Dsm mkuu wa polisi ameshindwa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app

Wameshindwa wazazi majirani Kama wewe na jamii.
 
Ndugu wanajamii hapa Dsm pamekuwa na matukio makubwa sana ya watoto WADOGO sana polisi waliwapa jina Panya road Hawa watoto WETU kwakuwa wameshindwa kuishi na jamii nyingine kwa udhaifu wa wazazi au jamii husika Sasa polisi Tena jeshi kubwa KUSHINDWA na kundi la watoto waliohutimu darasa la Saba na kutawala vyombo vyote vya habari ni kuonsha udhaifu mkubwa kwa Hili jeshi hasa kwa Dsm mkuu wa polisi ameshindwa

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Kesho RC atatoa tamko akiwa kavaa miwani yake nyeusi 😂😂🥂
 
Wamachinga wamewashinda na hawana silaha za jadi, Sasa ngoja tuone kwa Hawa wenye visu, mapanga na nyembe
 
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Maria Basso (24) amefariki dunia baada ya watu zaidi ya 10 kuvamia nyumbani kwao Kawe Mzimuni.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 14, 2022 na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Wiliam Mkonda imedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo Septemba 14 saa 2:30 usiku maeneo ya Kawe mzimuni, kikundi cha wahalifu wakiwa na silaha za jadi, walivamia nyumbani kwa jina Paschal Basso (56).

Amesema baada ya kuvamia nyumba hiyo yenye vyumba 15, walivunja milango na kupora fedha, simu za mkononi, kujeruhi watu watatu na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Paschal (24).

"Tukio walilofanya wahalifu hawa ni baya na linalotakiwa kulaaniwa na kukemewa na Mtanzania yoyote anayechukia uhalifu kwa watu kama hawa ambao hawataki kutumia njia halali za kujitafutia kipato," amesema Kamanda Mkonda.

Kufuatia tukio hili, Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawasaka wahalifu wote waliohusika katika tukio hilo pamoja na kuimarisha doria za miguu na mgari katika maeneo yote.

“Tunaendelea kuwasisitiza viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika kukabiliana na uhalifu wa aina hii katika maeneo yao,” amesema.

Akizungumza na Mwananchi, shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni jirani Benitto Edward amesema usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba usiku, kundi la vijana zaidi ya 20 wakiwa na mapanga, visu, bisibisi na marungu walivamia nyumba hiyo iliyopo Kawe Maringo.

“Baada ya kuvamia nyumba hiyo walianza kuvunja mlango mmoja baada ya mwingine wakiamrisha kupatiwa vitu mbalimbali kama vile simu, fedha na kompyuta mpakato (laptop),” amesema Edward.

Matukio ya watu kuvamiwa yameendelea kushika kasi na kutishia usalama wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo wiki moja tu tangu, Panya Road kuibuka tena na kuvamia nyumba 24 za wapangaji mtaa wa Kabaga Kinyerezi.

Kaimu Amidi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Kamfipo Gidion, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Maria alifariki alfajiri ya kuamkia jana kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mwananchi
Jamani huyu sio kuwa ni mwanafunzi tu Bali ni mfanyakazi wa kampuni ya milvik chini ya kitengo Cha sales associate na ni muajiriwa Kwa Zaid ya mwaka so nashangaa tumpe heshima yake pia
 
Juzi walivamia mtaani kwangu mbagala chamazi...wamekata watu mapanga sana....afu siku hzi sio watoto tu...kuna watu wazima pia
 
Serikali pamoja na kukusanya tozo nyingi Kwa raia bado inashindwa kutulinda na panya road.

Tozo Zetu mnaiba basi mtulinde na panya road.

Nipo hapa nauguza majeraha ya Jana.
pole mkuu ndo lile tukio la chamazi kwa mapemba usiku wa kuamkia leo?
 
Akiwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, CHADEMA walimchafua sana Makonda na kumsingizia mambo mengi.

Ugaidi,Uuaji, utesaji n.k tena walienda mbali na kumhusisha na dhulma kubwa kubwa,rushwa na upigwaji risasi wa Tundu Lissu.

CHADEMA waliuaminisha Umma kuwa Makonda atakuja shtakiwa kwa makosa yake lukuki kwa namna ambavyo waliyatanabaisha. Nmesubiria kusikia hata kesi moja dhidi ya Makonda kuhusiana na Shutma hizo. Mpaka leo kimya.

Hii inaonesha Makonda alichukiwa na kuonewa sana na Chadema. Huyu jamaa ndo alikuwa punching bag ya Chadema. Baada ya kutokuwa Mkuu wa Mkoa imeonekana kumbe hakuwa a makosa yoyote yale. Issue ilikuwa ni Ukuu wa Mkoa.

Natoa wito Chadema kumwomba Radhi Makonda Paul na kuahidi kuwa hawatarudia tena tabia hizo za kuchafua watu.
View attachment 2357181
 
Tatizo watu ni WAOOOOOGA WAOOOGA au niseme % kubwa ya watu especially wanaume wana vinasaba vya UOGA
 
Back
Top Bottom