Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho amefanikiwa kushinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka katika Tuzo za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Julai 21, 2022.
Tuzo hizo zimetolewa Rabat Nchini Morocco ambapo Sakho alikuwa akiwania nafasi hiyo dhidi ya Gabadinho Mhango wa Orlando Pirates na Zouhair El Moutaraji wa Wydad Athletic Club.
Sakho alilifunga bao hilo wakati #Simba ikishinda 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas mchezo wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam, Februari 13, 2022