Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo?

Haiwez kuwa sawa kulingana na power ya hizo engine ya V8 ina nguvu kubwa msukumo mkubwa kuliko Passo pamoja na ukubwa wa tairi hiyo n fact nyingine tena ndio maana mwenye bus kubwa akitembea 120 wewe mwenye gari ndogo kumshika mpaka ukanyage 150 kuendelea kutokana na gari yako.
Iliwahi kututokea tukiwa mbeya jamaa wa V8 tuliyekuwa tunafahamiana nae alitupita maeneo ya vwawa pale tukienda tunduma tukamuuliza anatembea na speed ngap akasema yupo kwenye 80 na sisi tulikua na 90 labda n sababu ya miinuko pia sijajua kwa tambarale ila nadhan haziwezi kuwa sawa
 
Askari wa barabarani na tochi zao wanapimaje?? Sababu kwenye vibao vya 50 wakipima v8 wataona km inaenda 60 wakat kiuhalisia yupo kwenye 50. Au inakaaje hii
 
Haiwi sawa IST ikiwa mkubwa ndo inakua V8 ka IST ni kagari mtoto kapo under 18
 
Kwa sababu ya size ya tairi askari wakipima speed wataona km v8 ameover speed.
 
sijajua mnachotaka kujua passo inatembea hadi speed 120 na iko control vizuri tu passo aliwahi nipita nikiwa na Rav4 niko speed 80 sasa cjui mnaanzaje kuidhau engine engine ya passo.
Physics inaeleza kila kitu kuhusu mnachotaka kujua tatizo ni lugha ya kiswahili ni lugha maskini huwezi elezea kwa kiswahili.
 
Kwa hiyousiijitutumue kununua gari kubwa, ukidhani una advantage kubwa sana dhidi ya gari ndogo. Nunua gari kubwa kwa sababu maalumu za kitaalamu sio kufata mkumbo.
 
Haziwezi kuwa sawa mkuu
Hatua Yako na Usain bolt haziwezi kufanana ,hivyo mkiwa kwenye speed sawa lazima atakupita sababu ya urefu wa hatua zake
Complete frequency of V8 will cover more distance than Passo's tire
Speaking from thought not experience
Kwa nadharia hii kama trekta likiwa na spidi ya 40km/h na Land cruiser V8 ikiwa kwenye spidi ya 40km/h for a given distance.

Inamaana trekta litawahi kufika?
 
Ukienda kimahesaba za pysics na law zake zote ziko speed moja ila practically haziwezi kua sawa kwa sababu hii
1. Kwenye mlima passo ataanza kusieze kwa sababu engine ni ndogo na hivo itaachwa
Hujaelewa swali au makusudi?
 
Sio kweli hiyo 140 uliyoiona ipo katika miles na sio km jaribu ku convert itakupa 220+km/h.
 
Ukubwa wa tairi kwenye kucover distance. Ukubwa wa V8 ukiwa unacover 1.8m basi wa Passo unacover 1.2m hivyo zikiwa kwenye mwendo sawa V8 kutokana na ukubwa wa tairi zake itakuwa mbele licha ya rotation kuwa sawa
Duuu!
 
Kudadeki alieleta Elimu kwa lugha ya Mkoloni ndie anaefanya watu wajichanganye hapa, huwezi kupima kasi bila Muda na huwezi kupima umbali bila kasi, Mtu anakuuliza anaetumia saa moja kutembea umbali wa km 80 akiwa na Passo au V8 nani anawahi kufika kimsingi hakuna Swali hapo ni chemsha bongo tu, Uwe mlefu au mfupi wote mkitumia Dk 10 kutoka ubungo kwenda kimala wote mtakuwa mmetembea umbali sawa tofauti mfupi atapiga hatua nyingi na mlefu atapiga hatua chache ila wote watakuwa wametembea umbali ule ule na kwa muda ule ule
 
Mtoto wa shule ya msingi akikimbia kwa Kasi ya km 10/saa na Usain Bolt naye akakimbia kwa Kasi ya km 10/saa, wote wanakimbia Kasi ile ile na watatumia muda ule ule kufika wanapoishia.

Tofauti ni dogo anatumia juhudi nyingi kwa mwendo huo ilhali Usain Bolt ni kama anacheza tu kwa spidi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…