Passport kutolewa ndani ya siku 3

Passport kutolewa ndani ya siku 3

Kuna ndugu yangu alikuwa anataka kwenda kenya akaambiwa akate ile temporary wamemkatalia kubwa
Hapana cvyo mkuu....huwa wanauliza unataka kubwa ama ndogo...uksema kubwa there u go....yangu inaexpire 2029 na nlitumia njia nlodadavua hapo juu.
 
[emoji4][emoji4][emoji4] Asante jibu lako limenisaidia sana.. Nilikua sijui kabisa uhamiaji ndio wanahusika na hayo mambo

Asante sana mkuu
Kama hautanii ni laki na nusu ndani ya siku 14 unapata tu samahani kama nimekukosea unajua nilifihisi unatania.
 
Mfumo umetengenezwa kuzuia wananchi wasipate pasipoti ndio maana wanataka barua ya kazi, mwaliko, shule nk ili upewe pasipoti.

Inashangaza sana kwa kweli
Kuna mijitu ilijipa haki miliki ikidhani hata hati ya kusafiria raia wa kawaida hawastahili...hii ndio mentality ya baadhi ya watawala wa nchi maskini.
 
Hata siku moja inawezekana ni kuwa na national database nzuri ya taarifa sahihi za raia...

Kwa sasa utapata mtu ako na national ID, pasi iliyokwisha muda lakini bado akitaka epasspprt kuna mlolongo wa vithibitisho ikiwemo national ID
 
Mwenye uwezo wakunisaidia kupata passport ndani ya wiki naomba aje pm.
Usitake kuweka mazingira ya kupigwa bila sababu. Passport mimi nilipewa ndani ya siku tatu ukijumlisha siku ya kupeleka maombi iikuwa ya kwanza na kuichukuwa ilikuwa siku ya tatu.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha fomu umejaza vizuri na kuprint kabla hujaenda, jazia kwenye vibanda pale nje, watakuelekeza vizuri. Fomu elfu 20 tu na unalipa kwa simu serikalini. Hakikisha unakopi zinazosomeka vizuri za viambatanisho vyote vinavyotakiwa. Ukiwa umezaliwa mpakani unawezwa ombwa cheti cha kuzaliwa cha bibi yako mzaa mama. Mimi nilipeleka affidavit ya bibi maana hana cheti na barua ya mwenyekiti wa kijiji chake ya utambulisho pamoja na cheti cha maza na changu. Ukilipia maombi pale uhamiaji, lipia kwa simu ili uwe na risiti papo hapo. Kuna dada alilipia benki pale wakamwambia asubiri mpaka benki ipeleke hesabu hazina ndo wazione. Maana japo benki wanakupa risiti, hutapigwa picha wala finger prints bila anayefanya hivyo kuiona hiyo pesa kwenye mtambo wao. Nikashauriwa na walionijazia fomu nikalipe kwa simu maana huonekana ndani ya dakika chache.

Ukiwa na kila kitu chako tayari, unahakikisha tu unakuwa pale mapema maana kuna foleni kubwa ya kutoka kwa wale mapassport officers kuitwa kwenye finger prints. Ukiwa kwenye hizo foleni lazima utahudumiwa hiyo siku hata usiku wa manane. Wakikupiga picha na finger prints zako, in principle kesho yake pasi yako inatoka. Ila unapewa tarehe ya keshokutwa kuichukuwa makao makuu ya zamani mjini.

Kwahiyo kama huna cheti original cha kuzaliwa anzia RITA, au kwa wazee kwa mwanasheria, vitambulisho vya uraia nenda NIDA, Vyeti vya ndoa kama ulibadili majina, etc. Ili mradi uende pale umekamilika.
Ukiingia kwenye mtandao wao, utaona mahitaji ya vinavyotakiwa kwa aina ya pasi unayoitaka.

Tusiwe wepesi kupenda mteremko, na kukompliketi mambo sie wenyewe bila sababu. . Uhamiaji nilikuwepo september na kiukweli wanajitahidi kwenda na mfumo mpya na kasi ya bwana mkubwa.
 
Wanarudisha aisee, mwaka jana nilienda pale kumsindikiza mtu wakanikazia eti nivae kama mtumishi wa Umma, ilitokea mvutano mpaka mzee mmoja (nadhani ni mkubwa wao) akaingilia ndio nikapita..... mwaka ujao natarajia kwenda kurenew sasa nataka nijipange kabisaaaa.
Passport inakaa miaka mingap
 
TANZANIA KUOMBA PASSPORT NI SAWA UNAOMBA PEPO UHAMIAJI WANAONA WAKIKUPA PASSPORT UTAKUWA UMEULA. KITAMBULISHO CHA TAIFA NI KITU KIKUBWA KULIKO PASPORT UNATAKIWA UKIWA NA KITAMBULISHO MOJA KWA MOJA WANAKUPA PASSPORT LAKINI HAWATHAMINI KITAMBULISHO nimeandika kwa herufi kubwa wajitambue
 
Kama hautanii ni laki na nusu ndani ya siku 14 unapata tu samahani kama nimekukosea unajua nilifihisi unatania.
Nilikuwa sitanii mkuu.. Je unaweza pata passport ata kama hauna safari ya kwenda nje ya nchi yani kuwa nayo tu kwaajili ya emergenc?
 
Ya rafiki yangu hyo .
Ila mpaka ameipata kafanya kazi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
20191111_134448.jpeg
 
Uhamiaji sina hamu nao kwanza kila askari ana kishoka wake, sasa wewe nenda kihalali utasumbuliwa mpaka ukome mi nakumbuka niliambiwa nikalete cheti cha kuzaliwa cha bibi mzaa mama, na hapo kumbuka nna Kitambulisho cha Taifa, ambacho kina taarifa zote,lakini bado nikaambiwa kalete Cheti cha kuzaliwa tena , hakuridhika akaniambia kalete cheti cha form4 nacho nimeweka haya barua ya mwenyekiti wa S/ya mtaa nayo nikaweka, Haya akaanza maswali ya kibwege unaenda wapi?cjui barua ya mwaliko?nikamwambia Siiiinnnaaaaa akaniambia nenda pale stationary muone Kenge gani sijui kumbe kishoka haya nae akaangalia form akaniambia mwanangu hapa bila 70 hupiti.Duuuuh!!! Nikatoa 70 nikampa form kesho najikuta fingerprint baada ya siku 3 mkoba huu hapa jamaa anao mkononi.
 
Mfumo umetengenezwa kuzuia wananchi wasipate pasipoti ndio maana wanataka barua ya kazi, mwaliko, shule nk ili upewe pasipoti.

Inashangaza sana kwa kweli
Ushawahi kuomba passport mkuu? Nenda na NIDA yako then utaona mambo yalivyo
 
Hata kwetu kama NIDA na Uhamiaji wangekuwa taasisi moja nadhani mtu mwenye NIDA taarifa zake zinajitosheleza kupata passport. Shida ni pale vitu ulivyoombwa wakati wa NIDA, Uhamiaji nao wanavitaka tena na nyongeza juu kama chetu mama cha kuzaliwa

Aaah wapi unapewa hii ya kawaida
 
Eti kitambulisho cha NIDA kinatolewa na serikali ya Tz halafu mtumishi wa serikali ya Tz hataki kukiamini
si ndio hapo Kitambulisho cha Taifa kina taarifa zote hicho pekee kingetosha lakini utaambiwa, Cheti cha kuzaliwa, affidaviti ya mzazj, barua ya S/ya mtaa , barua ya mdhamini, hii ndio sijuagi ina faida gani halafu hizo info z msingi zote zipo kwenye I'd ya Nida, Sasa barua ya S/ya mtaa yanini??????????
 
Back
Top Bottom