Mwenye uwezo wakunisaidia kupata passport ndani ya wiki naomba aje pm.
Usitake kuweka mazingira ya kupigwa bila sababu. Passport mimi nilipewa ndani ya siku tatu ukijumlisha siku ya kupeleka maombi iikuwa ya kwanza na kuichukuwa ilikuwa siku ya tatu.
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha fomu umejaza vizuri na kuprint kabla hujaenda, jazia kwenye vibanda pale nje, watakuelekeza vizuri. Fomu elfu 20 tu na unalipa kwa simu serikalini. Hakikisha unakopi zinazosomeka vizuri za viambatanisho vyote vinavyotakiwa. Ukiwa umezaliwa mpakani unawezwa ombwa cheti cha kuzaliwa cha bibi yako mzaa mama. Mimi nilipeleka affidavit ya bibi maana hana cheti na barua ya mwenyekiti wa kijiji chake ya utambulisho pamoja na cheti cha maza na changu. Ukilipia maombi pale uhamiaji, lipia kwa simu ili uwe na risiti papo hapo. Kuna dada alilipia benki pale wakamwambia asubiri mpaka benki ipeleke hesabu hazina ndo wazione. Maana japo benki wanakupa risiti, hutapigwa picha wala finger prints bila anayefanya hivyo kuiona hiyo pesa kwenye mtambo wao. Nikashauriwa na walionijazia fomu nikalipe kwa simu maana huonekana ndani ya dakika chache.
Ukiwa na kila kitu chako tayari, unahakikisha tu unakuwa pale mapema maana kuna foleni kubwa ya kutoka kwa wale mapassport officers kuitwa kwenye finger prints. Ukiwa kwenye hizo foleni lazima utahudumiwa hiyo siku hata usiku wa manane. Wakikupiga picha na finger prints zako, in principle kesho yake pasi yako inatoka. Ila unapewa tarehe ya keshokutwa kuichukuwa makao makuu ya zamani mjini.
Kwahiyo kama huna cheti original cha kuzaliwa anzia RITA, au kwa wazee kwa mwanasheria, vitambulisho vya uraia nenda NIDA, Vyeti vya ndoa kama ulibadili majina, etc. Ili mradi uende pale umekamilika.
Ukiingia kwenye mtandao wao, utaona mahitaji ya vinavyotakiwa kwa aina ya pasi unayoitaka.
Tusiwe wepesi kupenda mteremko, na kukompliketi mambo sie wenyewe bila sababu. . Uhamiaji nilikuwepo september na kiukweli wanajitahidi kwenda na mfumo mpya na kasi ya bwana mkubwa.