Pata milioni 15 kwa mwezi kwa biashara ya bodaboda

Pata milioni 15 kwa mwezi kwa biashara ya bodaboda

Hizo ni hesabu za kwenye calculator....
Kwa uhakika hakuna kitu kama hicho.
Dereva kuna siku ataumwa
Ajali
Pikipiki kuharibika/service
Uchakavu
Kuibiwa
Kuletewa manenošŸ™‚badala ya hesabu.
Si ndio amepigia asilimia 10
Au umesoma haraka haraka?
 
Duh, kwa hamasa hii maisha yangekuwa rahisi sana.
Swali langu ni je, hiyo nyumba ya m.100 wangapi wanayo?
Swali la logic sana hili.
Naongezea swali lingine"Mtu mwenye uwezo wa kujenga nyumba ya milioni 100 anakosa nini au ana shida gani mpaka akaanze kudili na bodaboda barabarani"

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja kwanza Penny,
Boda kuzinunua; 2 x 2,700,000 = 5,400,000

Marejesho ya siku kwa miezi sita, boda mbili; 10,000 x 30 x 6 x 2 = 3,600,000.

Yaani kwa miezi sita hizo boda mbili hazina ubavu wa kununua zingine mbili, hapo tunaweka consideration kwamba hiyo hela haiguswi, haicheleweshwi wala hakuna dharura.

Biashara ya kuwapa mkataba watu bodaboda ni upotevu wa pesa tu.
Yani unawekeza 2.7 millions kwenye boda af kwa siku unapata 10k tshs hiyo ni biashara ya mtu mvivu wa kufikiria! 2.7m inabid kwa siku ikupe atleast 30k net profitāœŒļø
 
Biashara ya bodaboda ilimfilisi GENTAMYCINE alikopa bodaboda mbili kwa mshahara wake wa ualimu zote zikapiga mzinga bunda mjini na hakuwa na insurance ya kueleweka
Hela ya bodaboda amekosa na benki kila mwezi WANAMKATA GENTAMYCINE


Biashara yoyote ni nzuri ukiwa unasimuliwa.

# elewa maana ya neno KUMKATA
Mshahara wa ualimušŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
 
_Pikipipi1 mpya = Kwa hesabu zako umeweka MAX 2000,000/=
_kilasiku unapokea 10000 x mwaka1[365] = 3650,000/=
_Mauzo ya pikipiki 1 kwa mwaka ni 3650,000 Toa pesa ya kununulia pikipiki 2000,000/= unapata 1,650,000/= [Faida ya pikipiki1 kwa mwaka]
_1,650,000 X Pikipiki50 = 82,500,000/=

Hesabu ya elf10 kwa mwaka means mkataba kwahyo baada ya mwaka hzo pikipiki si zako tena.. Za hao uliowapa. Labda ingekua hesabu ya day 7000/= hapo hakuna mkataba.


Umesomea wapi hizo hesabu za faida. Yaani mtaji umeuweka kwenye faida. Hyo Mil 180 toa mtaji uliouza nyumba unapata Mil 80 hyo ndo faida utayoingza kwa mwaka hapo ndio utoe na gharama za uendeshaji...
_Si doubt sana sababu huenda nilipo mimi na ulipo wewe gharama za marejesho ya pikipiki kwa siku ni tofauti.


NB: Kabla hujaanza biashara yeyote tathmini kwa kina, Pata uzoefu kwa watu wanaolijua vizuri eneo hilo, usikurupuke. Sababu biashara ni rahisi sana kichwani .
 
Wataalamu tujuzane wapi huko pikipiki mpya 2000,000. Mi natambua si chini ya 2.7 M. KWA mwaka huambulii kitu, Na pikipiki baada ya mkataba hazi zako tena. Huwezi wekeza Milioni 2.7 kuingiza elf3500 kwa siku. Hata muuza matikiti mwenye mtaji wa elf20 anakuzidi..

_Piga hesabu maokoto elf10 kwa siku x mwaka 365 = 3,650,000/=
_Toa 3,650,000 - Pesa ya mtaji uliyonunulia boda mpya labda 2,600,000.. unapata faida isiyopungua 1.2M kwa mwaka kwa pikipiki1 utatoa bima, TRA na mengineyo . .Tuwekee laki2 tu japo inazidi. Itabaki 1M

_1M gawanya kwa siku 365 upata sh ngapi hapo faida kwa siku?
_2700/= faida kwa siku
Kituko!


Labda kama unatania Money Penny
 
Back
Top Bottom