Naona hauelewi vita za proxy, Kagame hahitaji kwenda Kenya ila obviously Uganda ni koloni la Watutsi so in any war itakua via Uganda.
2. Kingine Kenya Ina vikundi kibao vya uasi sio tu NFD region kwa wasomali na wafugaji ila hata makundi ya msimamo mkali wa kiislamu wa kujitenga huko Pwani. Kagame anaweza fanya kazi na hao watu na ikapigwa vita ya proxy kama tu ilivyokua Ile ya M23..
3. Ukabila ni mkubwa sana Kenya kiasi kwamba wafuasi wa Upinzani yaani Wakamba, waluo, Waluhya, Pwani n.k wakiskia tu jeshi la Kenya limeingia vitani basi watakua wa kwanza kwenda barabarani kupinga nchi kuingia vitani na watakataza wafuasi wao kwenda Frontline. In fact wataona ni short cut ya kumpindua Ruto asubuhi na mapema.
4. Kuhusu uimara wa jeshi yes it's true linatengenezwa ila experience matters. Nchi zilizopo kwenye Kashi Kashi za kivita zinakua hazina margin of error so muda wote majeshi Yako busy. Mfano Rwanda ana majeshi kwenye nchi zaidi ya 13 yote hiyo ni kuwapa exposure na activeness kwenye battlefield. Sasa unadhani akikutana na wanajeshi wavaa ndala wa Westgate Nini kitatokea?? Rwanda fought in the Africa's world war, the audacity to take head-on 13 African countries in a stalemate war for 5 years should be a lesson to Ruto, unless he's dumb enough to disregard history!!
Sasa tukija kwenye proxy wars hapo ndio Rwanda inapigwa mapema kuliko Kenya. Rwanda ina uwezo wa kutoa hata $500 million kufadhili makundi pale Kenya? Kenya inao uwezo wa kuipata hiyo hela bila kukopa wala kuombaomba.
Kwa sasa waasi wenye silaha wanaopingana na Rwanda wapo pale Congo, kuna waasi wenye silaha wanaopambana na Kenya ukiachana na kundi la kigaidi ambalo halina claim na throne ya Kenya? Kenya haihitaji wala kuanzisha kundi jipya, ni kuyapa makundi hasimu ya Rwanda kama FDRL ambayo hata sasa yanatafuta nafasi na ukiyataka yapokee silaha na training leoleo yanakubali.
Kama unaona Rwanda itaitumia Uganda kuipiga Kenya, mbona huoni kama Kenya itaitumia Congo na Burundi kuipiga Rwanda. Burundi na Congo wana uhasama na Rwanda kuliko Kenya ilivyo na Uganda. Na unadhani Uganda ni wapumbavu wapigane na Kenya kisa Rwanda. Hata kama Museveni angekuwa hana akili ila kile sio chama cha vikoba ni nchi, hawezi risk madaraka yake na urithi wa mwanae kwa kutafuta mgogoro na jirani anayepitisha over 80% ya mizigo kwenye bandari yake.
Kenya haihitaji kurusha hata risasi moja kuikomoa Uganda. Funga bandari, barabara na reli zisiingize mizigo Uganda itokee inflation uone kama vijana wa Kampala watamuacha Museveni na walivyomchoka.
Nilikuwa nakuona kwenye uzi LIVE wa uchaguzi mkuu wa Kenya. Unaweza kutuwekea majimbo ya uchaguzi na matokeo yake hapa ukiambatisha na hayo makabila ili tuone upinzani wa Kenya ulivyo wa kikabila.
Kenya ina makabila 56 na hakuna civil war, genocide, assassination of head of state wala mapinduzi yaliwahi tokea. Rwanda ina makabila almost mawili tu yaliyopigana na yashaua marais pinzani, mauaji ya kimbali, uasi hadi sasa, mapinduzi. Nani kati ya hizi nchi mbili ana ukabila kuliko mwingine?
Kama vita ni mazoea basi unasema Switzerland ambayo haijawahi pigana miaka zaidi ya 500 iliyopita ni wapuuzi tu vitani wakati enzi za Cold War walikuwa na maandalizi makali kupindukia, maandaki ya kuficha population nzima ya nchi plus 10% ya ziada, na hakukuwa na nchi yenye uwezo wa kuficha hata 10% ya population. Last time Japan wamepigana vita ni 1945, kwamba kwa sasa wana jeshi yeboyebo?
Mbona Tanzania ya Mwalimu Nyerere iliipiga Uganda ya Iddi Amin mwanajeshi na mipango yake mingi. Mbona Libya ya Ghaddafi ilishindwa kuipiga Chad wakati Libya ilikuwa na harakati nyingi za kijeshi.
Ebu mkuu kaa chini jifikirie utafakari iami yako ya Uganda itaipiga Kenya kwa niaba ya Rwanda, kwa sababu ya Congo.