● Julai 29, 2011: Aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi (MUCCoBS).
● Septemba 27, 2011: Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) ulimchagua Paulo Makonda katika nafasi ya Mwenyekiti, akiwashinda wagombea wengine kutoka vyuo vikuu vinne.
● Oktoba 24, 2012: Paul Makonda aligombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na kushika nafasi ya pili baada ya kupata kura 241 nyuma ya Mboni Mhita aliyepata kura 489 katika duru ya pili ya uchaguzi huo.
● Februari 7, 2014: Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Paul Makonda kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba, akiwakilisha kundi la watu wenye malengo yanayofanana linalojumuisha wajumbe 14 kutoka Tanzania Bara.
● Februari 19, 2015: Rais Kikwete alimteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
● Machi 13, 2016: Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli afanya mabadiliko na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26. Katika mabadaliko hayo alimteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
● Julai 20, 2020: Makonda aibuka mshindi wa pili kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata kura 112, nyuma ya mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Faustine Ndugulile.
● Oktoba 22, 2023: CCM ilimteua Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.
☆☆☆☆ Hakika Makonda ana uzoefu wa kutosha katika medani za siasa nchini na ni mbobezi wa medani hiyo, hivyo pasi na shaka ataitendea haki nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.