Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Mkweli ambaye hata jina lake ni fake!

Kesi za nyumba na wahindi kila siku

ukabila wa kutisha

kusingizia watu watumia madawa ya kulevya

kuonea watu kiasi cha kupigwa marufuku kutokuingia USA

TUENDELEE!!!
 
Mkweli ambaye hata jina lake ni fake!
Kesi za nyumba na wahindi kila siku
ukabila wa kutisha
kusingizia watu watumia madawa ya kulevya
kuonea watu kiasi cha kupigwa marufuku kutokuingia USA
TUENDELEE!!!

Mbona haujamshitaki, si unaprufu zote ushinde fasta au?
 
Mbona haujamshitaki, si unaprufu zote ushinde fasta au?
Nitafaidika nini kumshitaki tu mjinga tena kwenye mfumo huu wa mahakama fake kama za TZ ambazo kesi zinachukuwa miaka!.

Angalia kesi za Covid 19 zimekaa muda gani! wataamua wakati bunge la miaka 5 limeisha sasa hapo tuna mahama kweli?? Tuache ujinga! hongera chawa
 
Nitafaidika nini kumshitaki tu mjinga tena kwenye mfumo huu wa mahakama fake kama za TZ ambazo kesi zinachukuwa miaka!. Angalia kesi za Covid 19 zimekaa muda gani! wataamua wakati bunge la miaka 5 limeisha sasa hapo tuna mahama kweli?? Tuache ujinga! hongera chawa

Umejuaje kuna ujinga na uchawa kama havikuhusu wewe...

Acha kuandika visingizio nenda kashitaki... na kwenda nje ya mada haraka sanaaa 🤣🤣🤣
 
Moderetor mimi sifi leo sifurahishwi kabisa na

Ukosefu wenu wa adabu!(nimeanza hivyo ili mjue nachukia najua mtafta uzi uhuu ili jf member wasisome nilivyo wasema maana nyie mwataka tuwaone malaika ili hali mu wanadamu kama sisi).

Katibu Mwenezi mteule wa ccm Ndugu Paulo Makonda akipitia kwenye mitandao kuna alligation nyingi sana zinatupwa kwake hasa na Makamu Mwenyekiti Ndugu Tunsu Lisu hizi aliigation ni nzito haifai kuwa katibu mwenezi na allligation za namna hii.

Kwa kuwa Tundu Lisu anasema alipata taafira kutoka kwa credible source of information yakuwa Ndugu Paulo Makonda alikuwa miongoni mwa waratibu wa kikosi kazi kilichotaka kumtoa uhai Tundu Lisu,ili jambo hatuwezi sisi lifumbia macho

Kama kweli Ndugu Makonda anaona yanayosemwa siyo sahihi sisi wananchi na wadau tunamshauri aende Mahakamani akamshitaki Tundu Lisu ili hii alligation iweze futwa kinyume chake sisi kama wadau wa siasa tutampokeaje mtu tuliyeambiwa ni mmoja wa waratibu wa mauaji kuja kwetu kueneza chama?

Moderetor nawaomba sana HOJA YANGU IPOKELEWE IJADILIWE HACHENI WATU TUWE HURU.

hivi hiki nimachokihoji kama aliyenusurika kuuwa ni Baba yako au Mama yako na anae shutumiwa yupo wewe moderetor ungefuta uzi wangu?
 
Moderetor mimi sifi leo sifurahishwi kabisa na

Ukosefu wenu wa adabu!(nimeanza hivyo ili mjue nachukia najua mtafta uzi uhuu ili jf member wasisome nilivyo wasema maana nyie mwataka tuwaone malaika ili hali mu wanadamu kama sisi).

Katibu Mwenezi mteule wa ccm Ndugu Paulo Makonda akipitia kwenye mitandao kuna alligation nyingi sana zinatupwa kwake hasa n Makamu Mwenyekiti Ndugu Tunsu Lisu hizi aliigation ni nzito haifai kuwa katibu mwenezi n allligation za namna hii.

Kwa kuwa Tundu Lisu anasema alipata taafira kutoka kwa cfedible source of information yakuwa Ndugu Paulo Makonda alikuwa miongoni mwa waratibu wa kikosi kazi kilichotaka kumtoa uhai Tundu Lisu,ili jambo hatuwezi sisi lifumbia macho

Kama kweli Ndugu Makonda anaona yanayosemwa siyo sahihi sisi wananchi na wadah tunamshauri aende Mahakamani akamshitaki Tundu Lisu ili hii alligation iweze futwa kinyume chake sisi kama wadah wa siasa tutampokeaje mtu tuliyeambiwa ni mmuajo kuja kwetu kueneza chama?

Moderetor nawaomba sana HOJA YANGU IPOKELEWE IJADILIWE HACHENI WATU TUWE HURU.

hivi hiki nimachokihoji kama aliyenusurika kuuwa ni Baba yako au Mama yako na anae shutumiwa yupo wewe moderetor ungefuta uzi wangu?
Hi tunaifuta mda sio mrefu.
 
Tuhuma nzito sana , naona serikali IPO kimya , hata kiongozi wa juu akituhumiwa na tuhuma nzito kama izo inabidi ajiuzulu Ili kupisha uchunguzi.
 
Naunga mkono

Pia Lema akamatwe na Polisi ili awataje waliopanga Njama za kuuiba Mwenge wa Uhuru
 
Tazama Facebook utaona jina "Sala Pita Makonda". Bila Shaka hiyo ndio Sarah Peter Makonda.
Need we say more,kwamba tuna mashaka kidogo kuhusu teuzi wa watu kama hawa katika nafasi hizi za juu kabisa za uongozi wa nchi yetu?
 
Tuhuma nzito sana , naona serikali IPO kimya , hata kiongozi wa juu akituhumiwa na tuhuma nzito kama izo inabidi ajiuzulu Ili kupisha uchunguzi.
Unaleta tuhuma after the event. Tuhuma ulitakiwa kutoa kabla ya Rais Samia kumchagua Makonda kuwa Katibu Mwenezi.
 
● Julai 29, 2011: Aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi (MUCCoBS).

● Septemba 27, 2011: Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) ulimchagua Paulo Makonda katika nafasi ya Mwenyekiti, akiwashinda wagombea wengine kutoka vyuo vikuu vinne.

● Oktoba 24, 2012: Paul Makonda aligombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na kushika nafasi ya pili baada ya kupata kura 241 nyuma ya Mboni Mhita aliyepata kura 489 katika duru ya pili ya uchaguzi huo.

● Februari 7, 2014: Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Paul Makonda kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba, akiwakilisha kundi la watu wenye malengo yanayofanana linalojumuisha wajumbe 14 kutoka Tanzania Bara.

● Februari 19, 2015: Rais Kikwete alimteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

● Machi 13, 2016: Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli afanya mabadiliko na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26. Katika mabadaliko hayo alimteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

● Julai 20, 2020: Makonda aibuka mshindi wa pili kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata kura 112, nyuma ya mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Faustine Ndugulile.

● Oktoba 22, 2023: CCM ilimteua Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.


☆☆☆☆ Hakika Makonda ana uzoefu wa kutosha katika medani za siasa nchini na ni mbobezi wa medani hiyo, hivyo pasi na shaka ataitendea haki nafasi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.
 
Idara ya itikadi na uenezi ndio moyo wa Chama Cha Mapinduzi kutokana na majukumu nyeti ya idara hiyo ambayo kwa mujibu wa katiba ya CCM ina majukumu makuu manne ambayo ni pamoja na kueneza itikati,falsafa misingi na sera za CCM,Kusimamia uendeshaji wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM,Kusimamia na kuratibu mafunzo ya makada ,viongozi na wanachama wa CCM na kusimamia masuala ya mawasiliano na uhamasishaji wa umma.

Kama mwana CCM naunga mkono kuondolewa kwa Dada yetu Sofia Mjema katika nafasi hiyo na ninaunga mkono uteuzi wa Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuwa Mwenezi mpya kwani Sofia Mjema alishindwa kabisa kufanya kazi za uenezi kutokana na ukweli kuwa tokea alipoteuliwa kuwa Mwenezi alikuwa akifanya kazi moja tu ya uMC Kwenye mikutano ya Katibu Mkuu ndugu Daniel Chongolo pamoja na kufanya press baada ya vikao vikuu vya CCM kama vile kamati kuu na Halmashauri kuu ya taifa.

Mikutano hiyo ni muhimu sana katika kukijenga na kukiimarisha chama lakini kwasisi tunaokijua Chama hatukutegemea Mwenezi wa taifa kufanya majukumu hayo pekee.

Kushindwa kwa Sofia Mjema kunatokana na ukweli kuwa siyo mwana CCM kindakindaki na hivyo hakuwahi kuandaliwa tofauti na Paul Makonda ambaye amekulia ndani ya CCM na hivyo inaijua vyema sera ya ujamaa na kujitegemea vilevile ni wazi kuwa uongozi ndani ya Chama cha siasa na uongozi serikalini ni vitu viwili tofauti kwani Chama cha siasa kuna vionjo vyake na kama hujui vionjo hivyo basi uongozi utakushinda hivyo katika makala haya sina nia mbaya ya kumchafua Dada yetu Sofia Mjema na ninamtakia mafanikio makubwa katika wadhifa wake mpya.

Paul Makonda ana uwezo mkubwa wa kutawala jjukwaa na ana uwezo wa kujenga hoja ,sifa muhimu sana katika kutekeleza majukumu ya idara hiyo.

Hatahivyo Paul Makonda ana deni kwa wana CCM na baadhi ya Watanzania kutokana na kuhusishwa na baadhi ya matukio yaliyotokea wakati wa utawala wa awamu ya tano hivyo anapaswa aweze kutulia na aonyeshe uwezo wake kwani kama kiongozi ameonyesha kuwa haogopi kuchukua maamuzi na huwa haogopi kulaumiwa.


Kwakuwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu naamini kuwa Paul Makonda atakisaidia vizuri Chama chetu katika kubuni mpango mkakati wa kunadi mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwani hivi sasa japo serikali ya COM inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan inafanya mambo mazuri kwa wananchi lakini wananchi wengi hawajui mambo hayo kutokana na ukweli kuwa hawaelimishwi vya kutosha.

Mwisho,Kama mwana CCM nitatoa natoa ushauri kwa Mwenezi wetu mpya kila wakati nitakapoona inafaa ili kuiboresha idara hiyo nyeti na mpaka sasa nimeandaa maandiko kadhaa ambayo ni

Umuhimu wa kurudisha kitengo cha Propaganda

Madarasa ya itikadi na

Mpango mkakati wa kunadi mafanikio ya serikaliya awamu ya sitakupitia mitandaoya kijamii

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Umesahau

1. Ana tamaa kubwa sana ya pesa na mali kiasi anaweza kumfanya mtu chochote kile ile apate pesa au mali.

2. Ana hulka ya ubabe na kupenda kutumia nguvu kiasi anaweza kumuumiza mtu ili tu afanikishe lengo lake.

3. Hana nidhamu wala adabu. Anaamini katika nguvu za aliye juu yake tu anayemlinda. Mtu kama huyu hafai kufanya kazi katika mifumo thabiti ya uwajibikaji na utendaji.

4. Ni mtu anayeamini kutengeneza mifumo nje ya mifumo halali ya nchi katika kutimiza malengo yake. Amewahi kutengeneza vikundi vilivyokuwa vikifanya kazi chafu hadi kusababisha Rais wa nchi kukosana na vyombo vya dola
 
Back
Top Bottom