Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Pompeo anayajua zaidi ya hayo
Hilo Jambo linataka kukuzwa bila sababu, hizi Ni tuhuma hakuna mahali Makonda kashitakiwa.

Ni vyema Makonda aombe kukutana na Balozi wa Marekani ili amweleze kosa lake ni Nini, na Kama Kuna tuhuma basi apewe muda azijibu.

Baada ya hapo iundwe time ya pamoja Kati ya Marekani na Tanzania ipitie tuhuma zake na suluhisho lake report ipelekwe pande zote mbili kwa utekelezaji.

Baadae Makonda aonane na Pompeo amuombe radhi kwa tuhumu za kweli na tuhuma za uongo amweleze kuwa amemsamehe kwani na yeye ni binadamu.

Hatuhitaji kugangamala kama Albashir, tunahitaji kuwa wanyenyekevu na wasikivu, huo ndio uungwana. Uhuru Kenyatta pamoja na kuwa ni Rais alienda ICC na akahudhuria kesi na Sasa Yuko huru.

Pompeo hajawahi onana na Makonda Wala hamjui Ni maneno ya kuambiwa tu.

Binafsi maovu ya Makonda siyajui, najua anahamasisha ujezi wa shule na zahanati. Anaendesha harambee za tiba za moyo kwa watoto. Anapambana na majizi na wala madawa ya kulevya. Anapambana na uzembe kazini.

Amueleze Pompeo kuwa Hawa wanaompiga vita ni wachuuzi wa madawa ya kulevya. Magenge ya wezi maarufu Kama panyaroad. Matapeli ya viwanja na wabadhirifu wa mali za umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio ulofa. Huyo ni mwanamme anaye disa. Mwanaume Rijali haofii kifo. Mashoga kama wewe ndiyo malofa. Utaachaje kuulinda utu wako na ule wa wananchi wako eti kwa sababu ya kuogopa kifo. Kifo ni kifo tu. Uanguke na ndege, upate ajali ya gari, ufe kwa sababu ya maradhi ya ukimwi au wakati unautetea utu wako. Kifo ni kifo tu.

Nikifa kwa ajili ya kutetea maslahi na utu wangu mbona ni thawabu kwa mungu. Kuna kifo kizuri kama hicho?



Sent using Jamii Forums mobile app
We kwenda zako huko yani mie nife kwa kumtetea bashite?
 
Sasa kumnyima Visa ya kuingia Marekani ndo watazuia juhudi zake na serikali kupiga vita madawa ya kulevya na genge la madawa ya kulevya paomoja na ushoga? Ataendelea tena kwa saana kwasababu amewashika pabaya! Moja ya mikakati ya USA ni kuungana na magenge ya uhalifu wa kimataifa kuzinyongonyeza nchi masikini ili wapore mali na utajiri wa nchi za kiafrica. Moja ya mbinu inayozitumia marekani ni pamoja na kusupport magenge ya madawa ya kulevya kuingizwa katika nchi masikini kuharibu vizazi ili kutengeneza mwanya wa kuzipora rasilimali zao!
 
Juzi kati kondom tu zilikua hadimu watu wakaanza kulialia.
Swali: Hivi una umri gani?
USA wamelianzisha wenyewe sasa tusilaumiane,
Wanachopaswa waelewe kwa sasa sisi si dhaifu tena chini ya mwamba dokta JPM,
Kwanza wanampa tuhuma nzito Makonda bila kuweka ushahidi, huo ni umbea tu kama umbea mwingine,

Hatutawanyenyekea hata kidogo, ni heri kuwa masikini jeuri kuliko kunyanyaswa, yaani marekani atuamulie sisi namna ya kuishi? Yeye kama nani?
Hii nchi ni huru na inajiendesha yenyewe,

Hata aibu hana taifa kama USA eti anaweka ligi na TZ?

Sasa ni jino kwa jino, tunaomba Rais na wewe ujibu mapigo tuone sasa kama vipi hata uhusiano na Us uishe, kwanza hawa watu ni magaidi tu kazi yao kuvuruga nchi za watu,

Tuko nyuma yako JpM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujue kila mtoto chini ya miaka 5 huwa anaona baba yake bonge la swaziniga. Yaani huwa wanaamini hata lije jambazi la aje baba atalibonda.

Mdogo wangu ukikua kidogo tu utatambua hata huyo baba yetu na swaziniga wetu anawaogopa kishenzi hao jamaa.
 
Mbona USA ilimnyima haki ya kuishi yule jenerali wa IRANI?Tusiwe kasuku
Wairan wanatuhusu nini sisi, sisi wanatuuma Watanzania wenzetu wanaonyimwa haki ya kuishi na Makonda na genge lake. Tunawalilia Watanzania wenzetu Azory Gwanda na Beny Saanane waliopotezwa kwa sababu tu ya uwajibikaji wao. Tuanze kujadili Iran na Iraq tuache kujadili kuuawa kwa Mawazo na kutekwa na kuteswa kwa Mdude? Kwani tumeanza Jana kusema mnaua Watanzania wenzetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa mabeberu waache kuingilia mambo yetu ya ndani, watuachie uhuru wetu.. Wao nani anawaingilie kwenye mambo yao..

USA hatuendi sio lazima, zipo nchi nyingi za kwenda zenye amani kuliko huko USA wanakouana kila siku..

Ukishapigwa ban na marekani hujue na nchi nyingine itakuwa issue kupata visa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
USA wamelianzisha wenyewe sasa tusilaumiane,
Wanachopaswa waelewe kwa sasa sisi si dhaifu tena chini ya mwamba dokta JPM,
Kwanza wanampa tuhuma nzito Makonda bila kuweka ushahidi, huo ni umbea tu kama umbea mwingine,

Hatutawanyenyekea hata kidogo, ni heri kuwa masikini jeuri kuliko kunyanyaswa, yaani marekani atuamulie sisi namna ya kuishi? Yeye kama nani?
Hii nchi ni huru na inajiendesha yenyewe,

Hata aibu hana taifa kama USA eti anaweka ligi na TZ?

Sasa ni jino kwa jino, tunaomba Rais na wewe ujibu mapigo tuone sasa kama vipi hata uhusiano na Us uishe, kwanza hawa watu ni magaidi tu kazi yao kuvuruga nchi za watu,

Tuko nyuma yako JpM
Pole sana Makonda

Tuko nyuma yako Kabudi
Tutembee kifua mbele sisi ni donor country 😂😂😂😂
 
Basi na nyie wawekeeni vikwazo. Lakini pia angalia USA hawakuficha juu ya hilo. Basi Makonda nae aweke wazi nani kamnyima haki ya kuishi.

Na usisahau kwa Makonda ni jambo linalohusu Watanzania wenzetu
Katazo hili kwa kiasi kikubwa tunaweza kusema ni kuhusu kauli zake kwenye mambo ya ushoga. Tangu atoe lile tamko la kukurupuka, nchi za Magharibi hazikufurahishwa kabisa.

Haya mengine wameyaweka tu kwani wanajua wangesema tu ni ushoga basi wananchi wengi wange-react negatively! Tusidanganyane eti wamekasirishwa na manyanyaso yake kwa raia. All in all, wakulaumiwa hapa ni rais mwenyewe.

Huyu Makonda alikwishaonyesha kabisa ni mtu asiye na busara ya uongozi, hafanyi kazi yoyote bali ni msanii na mabovu mengine mengi lakini kwa sababu anazojua aliyemteua hataki kumwondoa. Hata wananchi wengi wa Tanzania hawampendi na Makonda mbaya zaidi anasababisha chuki kati ya serikali na wananchi.
 
Back
Top Bottom