Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Wewe waache tu wamarekani, tuwapiga shangazi zao mpaka wanyooke😂😂😂😂
ngoja nikupe siri uliyokuwa uhifahamu "sisi tuna uwezo wa kupigana na dunia nzima na tukashinda(one state army), hata USA ajiunge na nchi zote duniani"
usimwambie mtu yoyote juu ya hili
 
Ujue kila mtoto chini ya miaka 5 huwa anaona baba yake bonge la swaziniga. Yaani huwa wanaamini hata lije jambazi la aje baba atalibonda.

Mdogo wangu ukikua kidogo tu utatambua hata huyo baba yetu na swaziniga wetu anawaogopa kishenzi hao jamaa.
😃😃
 
Hivi Bashite mwenyewe alivyo mwepesi wa kutoa matamko baada ya zuio hilo hadi sasa hajatoa kauli yoyote inayohusiana na huko kupigwa marufuku?
Atakua anasubiri Jumapili aende Church akalie,poor him ametu cost wenzake hadi saivi tumepigwa pini na America.Nadhani Yajayo yanafurahisha zaidi tusubiri tu[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh chief hiki kingereza chako kiboko. Ungetuandikia kiswahili tungekuelewa
The thred was writen on English, I like very much those language thus why I had to coment using the English language. You should right you're coment on English too.
 
ngoja nikupe siri uliyokuwa uhifahamu "sisi tuna uwezo wa kupigana na dunia nzima na tukashinda(one state army), hata USA ajiunge na nchi zote duniani"
usimwambie mtu yoyote juu ya hili
Nakuapia hiyo Siri nitakufa nayo😂😂😂😂😂
 
Hilo Jambo linataka kukuzwa bila sababu, hizi Ni tuhuma hakuna mahali Makonda kashitakiwa.

Ni vyema Makonda aombe kukutana na Balozi wa Marekani ili amweleze kosa lake ni Nini, na Kama Kuna tuhuma basi apewe muda azijibu.

Baada ya hapo iundwe time ya pamoja Kati ya Marekani na Tanzania ipitie tuhuma zake na suluhisho lake report ipelekwe pande zote mbili kwa utekelezaji.

Baadae Makonda aonane na Pompeo amuombe radhi kwa tuhumu za kweli na tuhuma za uongo amweleze kuwa amemsamehe kwani na yeye ni binadamu.

Hatuhitaji kugangamala kama Albashir, tunahitaji kuwa wanyenyekevu na wasikivu, huo ndio uungwana. Uhuru Kenyatta pamoja na kuwa ni Rais alienda ICC na akahudhuria kesi na Sasa Yuko huru.

Pompeo hajawahi onana na Makonda Wala hamjui Ni maneno ya kuambiwa tu.

Binafsi maovu ya Makonda siyajui, najua anahamasisha ujezi wa shule na zahanati. Anaendesha harambee za tiba za moyo kwa watoto. Anapambana na majizi na wala madawa ya kulevya. Anapambana na uzembe kazini.

Amueleze Pompeo kuwa Hawa wanaompiga vita ni wachuuzi wa madawa ya kulevya. Magenge ya wezi maarufu Kama panyaroad. Matapeli ya viwanja na wabadhirifu wa mali za umma.
No comment, ila nimecheeeeeka mpaka luku ikakata, huu sasa ni utani wa mwaka.
 
Ni upunguani wetu sisi wenye ngozi nyeusi.
Kila siku tunapiga mipicha na kutuma fb, Twitter na WhatsApp hata bila kujua hiyo mitandao Ni ya akina Nani na Nani Yuko nyuma ya hii mitandao .
Tukitaka kufanya uhalifu,sisi watu weusi tunatumia hii mitandao mfano call,sms,na WhatsApp kutekeleza uhalifu bila kujua aliyepo nyuma ya hii mitandao Ni Nani?.
Kama umefanya uhalifu mfano mauaji,uvamizi na hata wizi na maandalizi ukayafanya kupitia hii mitandao je Marekani ikikutafuta itakukosa?.
Tusitetee mambo ya kishenzi ndani ya nchi yetu,tusimamie maadili ya kitanzania.
 
Katazo hili kwa kiasi kikubwa tunaweza kusema ni kuhusu kauli zake kwenye mambo ya ushoga. Tangu atoe lile tamko la kukurupuka, nchi za Magharibi hazikufurahishwa kabisa. Haya mengine wameyaweka tu kwani wanajua wangesema tu ni ushoga basi wananchi wengi wange-react negatively! Tusidanganyane eti wamekasirishwa na manyanyaso yake kwa raia. All in all, wakulaumiwa hapa ni rais mwenyewe. Huyu Makonda alikwishaonyesha kabisa ni mtu asiye na busara ya uongozi, hafanyi kazi yoyote bali ni msanii na mabovu mengine mengi lakini kwa sababu anazojua aliyemteua hataki kumwondoa. Hata wananchi wengi wa Tanzania hawampendi na Makonda mbaya zaidi anasababisha chuki kati ya serikali na wananchi.
Mbombo ngafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa wamempa umaarufu na mtaji mkubwa wa kisiasa Makonda.
Makonda sio waziri na kazi zake hazina umuhimu wa kwenda Marekani.

Hawezi kufa kwa kushindwa kuingia Marekani, kama ana fedha ataenda kutibiwa Ulaya au India na China, anaweza kuita madaktari bingwa toka Marekani na wakamhudumia hapa hapa Tanzania.
Zaidi ya 98% ya watanzania wanakufa kabla hawajatoka nje ya Tanzania kwenda Marekani au nchi jirani za EAC.
Kabla hujaendelea kuandika hembu tambua kuwa ukizuiwa Marekani umezuiwa ulaya na kwa nchi rafiki zote kwa Marekani mfano Israel. Nadhani hufahamu kuhusu maombi ya visa na interviews za visa application

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom