Hilo Jambo linataka kukuzwa bila sababu, hizi Ni tuhuma hakuna mahali Makonda kashitakiwa.
Ni vyema Makonda aombe kukutana na Balozi wa Marekani ili amweleze kosa lake ni Nini, na Kama Kuna tuhuma basi apewe muda azijibu.
Baada ya hapo iundwe time ya pamoja Kati ya Marekani na Tanzania ipitie tuhuma zake na suluhisho lake report ipelekwe pande zote mbili kwa utekelezaji.
Baadae Makonda aonane na Pompeo amuombe radhi kwa tuhumu za kweli na tuhuma za uongo amweleze kuwa amemsamehe kwani na yeye ni binadamu.
Hatuhitaji kugangamala kama Albashir, tunahitaji kuwa wanyenyekevu na wasikivu, huo ndio uungwana. Uhuru Kenyatta pamoja na kuwa ni Rais alienda ICC na akahudhuria kesi na Sasa Yuko huru.
Pompeo hajawahi onana na Makonda Wala hamjui Ni maneno ya kuambiwa tu.
Binafsi maovu ya Makonda siyajui, najua anahamasisha ujezi wa shule na zahanati. Anaendesha harambee za tiba za moyo kwa watoto. Anapambana na majizi na wala madawa ya kulevya. Anapambana na uzembe kazini.
Amueleze Pompeo kuwa Hawa wanaompiga vita ni wachuuzi wa madawa ya kulevya. Magenge ya wezi maarufu Kama panyaroad. Matapeli ya viwanja na wabadhirifu wa mali za umma.