Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Naona watu wanajadili zuio la Makonda kuingia Marekani badala ya kujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Wenye akili ndogo wameanza kusema "Kwani Marekani ni mbinguni? Kwani asipoenda atapungukiwa nini?" Hii ni comment ya Mbunge mmoja wa CCM kule Twitter.

Lakini hoja si Makonda kuzuiwa kuingia Marekani au kuingia Chato. Hoja ya msingi ni madai yaliyotolewa na Marekani kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Makonda.

Pamoja na mambo mengine, Pompeo amesema Marekani ina USHAHIDI kuwa Makonda ameshiriki KUDHULUMU HAKI YA KUISHI KWA WATU KADHAA. Hii ni kauli ngumu sana, inayotafakarisha sana.

Kudhulumu haki ya watu kuishi means kuamua kumuondolea mtu uhai kabla ya wakati wake. Je ni kweli Makonda amefanya hayo? Kwa akina nani? Kwa ruhusa ya nani? Kwa sababu gani? Lini? Wapi? Na kwanini?

Kumbuka taifa lenye teknolojia kubwa kama Marekani linaposema lina USHAHIDI juu ya jambo fulani bila shaka limejiridhisha vya kutosha.

Kwahiyo ili tuwe na mjadala wenye tija tuachane na kujadili zuio, tujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Hata kama asingezuiwa kwenda Marekani, lakini tuhuma alizotajwa nazo ni kubwa sana. Zinaogofya, zinatafakarisha, zinatisha. Kumbuka Marekani imesema ina USHAHIDI na kumbuka Pompeo alikua Mkurugenzi wa CIA kabla ya kuwa Waziri.!
Kwahiyo anachokisema USA unaamini? Angalia matukio mengi aliyoyafanya duniani kwa kuidanganya dunia. Hiyo barua ukiiangalia kiundani ni copy paste. Yaani wamechukua barua ambayo washaandikiaga watu na kuedit jina la makonda tu. Swala hapo ni la ushoga tu hakuna kitu kingine. Nasikitika sana kuona waafrika wanawaamini sana USA katika kila jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USA wamelianzisha wenyewe sasa tusilaumiane,
Wanachopaswa waelewe kwa sasa sisi si dhaifu tena chini ya mwamba dokta JPM,
Kwanza wanampa tuhuma nzito Makonda bila kuweka ushahidi, huo ni umbea tu kama umbea mwingine,

Hatutawanyenyekea hata kidogo, ni heri kuwa masikini jeuri kuliko kunyanyaswa, yaani marekani atuamulie sisi namna ya kuishi? Yeye kama nani?
Hii nchi ni huru na inajiendesha yenyewe,

Hata aibu hana taifa kama USA eti anaweka ligi na TZ?

Sasa ni jino kwa jino, tunaomba Rais na wewe ujibu mapigo tuone sasa kama vipi hata uhusiano na Us uishe, kwanza hawa watu ni magaidi tu kazi yao kuvuruga nchi za watu,

Tuko nyuma yako JpM
Pole sana Makonda
Kwanza kabudi alihaidi atahakikisha anapambana kuiondolea vikwazo zimbabwe, na kwa hili ninaimani hatashindwa!

Tuko nyuma yako Kabudi
Viva jpm [emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Kama kweli tatizo la Makonda ni mambo ya kulawitiana, basi nina hakika akina Superbug, Echilio, erythrocyie, Sky Eclat, nk. wote mutatueleza musimamo wenu. Imefikia hatua unashangilia kila linalokuja kinyume cha serikali bila kujua wewe linakugusa vipi?

Au ndo haki alizotaja Zitto kwenye barua yake?
 
Ila bebebru hata siku moja hawezi kuwa mbuzi jike, Hivi hawajui kama ubalozi wao uko chini ya himaya ya Makonda?
 
Hahaha nimeona vikosi vya lugalo pale vikipasha...

Kumbe yale maandiko taifa kubwa duniani litadondoshwa na taifa ndogo hilo taifa ndogo ni tanzania??

usa waanze kuomba msaada kwa washirika wake[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I think there are some laws in Tanzania tells something about homosexual and its clearly stated that homosexual is prohibited in Tanzania. With no doubt, this law existed since independence and still working if not somebody can correct. If this law was there since Nyerere till now, Why this tycoon USA want now to deal with our friend Makonda??
As far as I know, there are some nations in Africa have strictly prohibit homosexual with strong punishment when some body caught involved, Why do USA deal with only Tanzania and Paul not these nations?

I will be back.. please somebody help on those questions.
 
USA ni wapumb**v*". Sasa kumnyima Visa ya kuingia Marekani ndo watazuia juhudi zake na serikali kupiga vita madawa ya kulevya na genge la madawa ya kulevya paomoja na ushoga? Ataendelea tena kwa saana kwasababu amewashika pabaya! Moja ya mikakati ya USA ni kuungana na magenge ya uhalifu wa kimataifa kuzinyongonyeza nchi masikini ili wapore mali na utajiri wa nchi za kiafrica. Moja ya mbinu inayozitumia marekani ni pamoja na kusupport magenge ya madawa ya kulevya kuingizwa katika nchi masikini kuharibu vizazi ili kutengeneza mwanya wa kuziporwa a rasilimali zao!
Huko kwenye madawa na mashoga unajua wewe,jamaa yenu anapotezea watu haki ya kuishi
 
Back
Top Bottom