Katika sababu zilizotajwa kwa Makonda kuzuiliwa kwenda Marekani ni "kuwanyima watu haki ya kuishi na usalama wao" Hi ni sentensi nzito kwa watu wanaofikiria mambo kwa umakini, kwa kuwa unapomnyima mtu haki ya kuishi ina maana huyo mtu haishi tena, hayuko hai tena kwa kuwa umeondoa haki yake ya kuishi, au umemnyima haki yake ya kuwa hai - umemuua. Hilo ndilo wanalosema USA juu ya Makonda.
Watu wengi wanafikiria kwamba Makonda amezuiliwa kwenda USA kutokana na msimamo wake juu ya suala la ushoga, lakini ni wazi kutokana na kauli ya USA kwamba kuna zaidi ya hilo. Je kuna mambo ambayo Watanzania tumefumbwa kwa muda mrefu sana na serikali yetu lakini USA wana taarifa zote?
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusiana na watu kuuwawa, kutekwa na majaribio ya kuuwawa ncini ambazo serikali haijawa wazi sana kuzieleza au kuonyesha kuwa inayafanyia kwa uzito upelelezi wa hayo matukio. Kuna dalili basi, kwamba hawa USA wana ufahamu wa haya mambo kuliko tunavyofikiria.
Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi. Lakini kwa sasa, Makonda kutuhumiwa kwamba amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi ni jambo kubwa sana!
Hakuna siku niliyofurahi Kama hii baada ya US secretary of state kum blacklist Makonda Kama mtu hatari asiyetakiwa kukanyaga ktk taifa hilo kubwa Duniani kuliko yote..
Ni Makonda amekuwa akitumia madhabahu za Kanisa la Mungu kujifanya kwamba yeye ni mcha Mungu kumbe ni mtu aliyejaa uovu wa kila aina .
CIA wana ushahidi wote jinsi Makonda alivyohusika ktk mission ya mauaji ya Ben Saanane na jaribio la mauaji ya Tundu Lissu yaliyofeli .
CIA wana ushahidi wote jinsi alivyohusika ktk kutengeneza Photoshop video ya kumchafua Mtumishi wa MUNGU Gwajima .
CIA wana ushahidi wote jinsi alivyohusika na mauaji ya mamia ya watu waliokuwa wakitoswa Baharini na mto Ruvu .
Lakini lengo la Marekani siyo Makonda, bali mfadhili wake, huyu ndiye hasa wanayemtafuta kwa udi na uvumba..
Tumemwomba sana Mungu ili Haya mambo yafike tamati, hatimaye muda umefika sasa. ..
Moto umewaka, taratibu utaunguza kila kilichokusudiwa.
Nimeshaandika mara nyingi humu kuwa Damu isiyo na hatia inamlilia Mungu ikidai kisasi.
Damu ya Azory Gwanda, Damu ya Alphonce Mawazo, Damu ya Ben Saanane na wengine wengi tu
Sasa kumnyima Visa ya kuingia Marekani ndo watazuia juhudi zake na serikali kupiga vita madawa ya kulevya na genge la madawa ya kulevya paomoja na ushoga? Ataendelea tena kwa saana kwasababu amewashika pabaya! Moja ya mikakati ya USA ni kuungana na magenge ya uhalifu wa kimataifa kuzinyongonyeza nchi masikini ili wapore mali na utajiri wa nchi za kiafrica. Moja ya mbinu inayozitumia marekani ni pamoja na kusupport magenge ya madawa ya kulevya kuingizwa katika nchi masikini kuharibu vizazi ili kutengeneza mwanya wa kuzipora rasilimali zao!
Kichwa unacho Ila akili nina wasiwasi Kama unayo, hakuna sehemu kwenye taarifa ya USA inazungumza juu ya hoja ya madawa, na kwa wajinga wasiofatilia ndiyo wanaamini juu ya upambanaji feki wa madawa.
Wamarekani na washirika wao hawawezi kukubali kuona nchi maskini ya dunia ya tatu inaongozwa na Nationalist leader kama Magufuli na wenzie waliomtangulia nchi zingine kama akina Thomas Sankara, Patrice Lumumba, Fidel Castro, Hugo Chavez, Eva Morales, Ghadaf, Kim wa NK na wengine wengi.
Kisa cha Makonda ni mapango wa muda mrefu wa kuzuwia uwezekano wa yeye Makonda na wa mfano wa Magufuli kuja kushika nchi baada ya Magufuli.
Huu ni mpango mkakati wa taassisi zao za kijasusi.
Kuchaguliwa kwa Magufuli kuwa rahisi wa Tanzania hawa mabeberu walipigwa chenga ya mwili na akina Mkapa na watu wengine nyeti walio hakikisha vibaraka wa Magharibi wanapigwa chini na Magufuli anakuwa raisi.
Hawakutegemea Magufuli atakuwa raisi, hili ni pigo kubwa sana kwao tena ni kashifa kwa taasisi zao za kijasusi ukizingatia anayo fanya Magufuli kuhusu rasilimali za taifa na mikataba kama ya EPA na AGOA.
Najua sitaeleweka na nitabezwa lakini ipo siku ukweli huu utawekwa wazi na mabeberu wenyewe miaka mingi ijayo kama walivyoweka wazi mkakati wao wa kumuandaa mrithi wa Nyerere.
Akina Kabudi, Kingwangala, na wengine mnao fanana kidogo mitizamo na Magufuli mjiandae kisaikolojia, mtakumbana na mashambulizi mengi sana hadi kufikia 2025 kwa lengo la kuwazuia msije kuwa warithi wa Magufuli.
Beberu sio mtu mzuri kabisa.
Soma hapa Top secret CIA files expose US covert operations in Tanzania
Jamani jaribuni kunielewa. Mimi hata siku moja sikatai kuwa jamaa anatumia madaraka vibaya, ni msanii na hakuna kazi yoyote anayofanya zaidi ya kujionyesha, na pia amelewa madaraka. Issue yangu ni kuwa pamoja na haya madhambi yoooote asingekuwa ameropoka suala la ushoga wala wasingemgusa.
Kwa wapinzani huu ni wakati mhimu na 'delicate' sana.
Wasibweteke, ni wakati wa kuweka mikakati itakayowawezesha kusimama na waTanzania wawaone kuwa wapo bila ya kuonekana kuwa wanatumiwa na mataifa ya nje.
Wakifanya makosa hapa, watakuwa wanaruhusu hawa 'wazalendo feki' kuendelea kuwarubuni wananchi na kuwapaka matope wapinzani.
Kumweka Magufuli kundi moja na kina Lumumba, Nkrumah, Nyerere, Thomas Sankara ni uzwazwa wa kiwango cha lami! Magufuli anaweza fananishwa na kina Mobutu, Bokassa, Kagame, Nkurunziza na labda Museveni.
Magufuli hajafanya hata sehemu moja ya mia ya aliyoyafanya Nyerere. Na bado Nyerere hakuwekewa!
Nyerere alitaifisha migodi yote na kuifunga akidai kufanya hivyo 'hadi watakapopatikana Watanzania wenye ujuzi wa kuchimba kwa faida yangu vizazi vijavyo', alitaifisha mashamba makubwa, majumba yaliyojengwa kwa mapato ya 'kinyonyaji' aliifanya Tanzania kuwa ngome ya wapigania Uhuru na mengine kibao lakini hakuwekewa vikwazo wala kunyimwa misaada ikiwemo mikopo alipoihitaji!
Leo JPM kukamata kontena kadhaa za mchanga awe adui wa kuwindwa na 'Mabeberu'? Ni Ulaghai wa mchana kweupe.
Sababu za vikwazo imewekwa wazi kwa yeyote anayejua lugha, ni 'Human Rights abuse', yaani uvunjifu wa haki za Binadamu na kuwanyima watu haki ya uhai, ndiyo 'The right to life'! Kwa tafsiri rahisi ni 'Muuaji'! Na Marekani wanadai kuwa na ushahidi usiotiliwa shaka!
Bado unataka kutulaghai eti ni kwa sababu za uzalendo? Uzalendo upi? Wa kuteka, kutesa na kuwapoteza watu?
Nationalist alikuwa Nyerere tu hao wengine ni mbwembwe za kujinafkisha kwa wanachi, MTU anatembelea V8, Range over anaishi ghorofani anawatukana watz walipakodi unamwita nationalist ni kumkosea Mungu