Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
.
Jr[emoji769]
Katika sababu zilizotajwa kwa Makonda kuzuiliwa kwenda Marekani ni "kuwanyima watu haki ya kuishi na usalama wao" Hi ni sentensi nzito kwa watu wanaofikiria mambo kwa umakini, kwa kuwa unapomnyima mtu haki ya kuishi ina maana huyo mtu haishi tena, hayuko hai tena kwa kuwa umeondoa haki yake ya kuishi, au umemnyima haki yake ya kuwa hai - umemuua. Hilo ndilo wanalosema USA juu ya Makonda.
Watu wengi wanafikiria kwamba Makonda amezuiliwa kwenda USA kutokana na msimamo wake juu ya suala la ushoga, lakini ni wazi kutokana na kauli ya USA kwamba kuna zaidi ya hilo. Je kuna mambo ambayo Watanzania tumefumbwa kwa muda mrefu sana na serikali yetu lakini USA wana taarifa zote?
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusiana na watu kuuwawa, kutekwa na majaribio ya kuuwawa ncini ambazo serikali haijawa wazi sana kuzieleza au kuonyesha kuwa inayafanyia kwa uzito upelelezi wa hayo matukio. Kuna dalili basi, kwamba hawa USA wana ufahamu wa haya mambo kuliko tunavyofikiria.
Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi. Lakini kwa sasa, Makonda kutuhumiwa kwamba amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi ni jambo kubwa sana!
Reference:Makonda apigwa 'stop' kuingia Marekani
View attachment 1343097
Jr[emoji769]