Kumweka Magufuli kundi moja na kina Lumumba, Nkrumah, Nyerere, Thomas Sankara ni uzwazwa wa kiwango cha lami! Magufuli anaweza fananishwa na kina Mobutu, Bokassa, Kagame, Nkurunziza na labda Museveni.
Magufuli hajafanya hata sehemu moja ya mia ya aliyoyafanya Nyerere. Na bado Nyerere hakuwekewa!
Nyerere alitaifisha migodi yote na kuifunga akidai kufanya hivyo 'hadi watakapopatikana Watanzania wenye ujuzi wa kuchimba kwa faida yangu vizazi vijavyo', alitaifisha mashamba makubwa, majumba yaliyojengwa kwa mapato ya 'kinyonyaji' aliifanya Tanzania kuwa ngome ya wapigania Uhuru na mengine kibao lakini hakuwekewa vikwazo wala kunyimwa misaada ikiwemo mikopo alipoihitaji!
Leo JPM kukamata kontena kadhaa za mchanga awe adui wa kuwindwa na 'Mabeberu'? Ni Ulaghai wa mchana kweupe.
Sababu za vikwazo imewekwa wazi kwa yeyote anayejua lugha, ni 'Human Rights abuse', yaani uvunjifu wa haki za Binadamu na kuwanyima watu haki ya uhai, ndiyo 'The right to life'! Kwa tafsiri rahisi ni 'Muuaji'! Na Marekani wanadai kuwa na ushahidi usiotiliwa shaka!
Bado unataka kutulaghai eti ni kwa sababu za uzalendo? Uzalendo upi? Wa kuteka, kutesa na kuwapoteza watu?
Sent using
Jamii Forums mobile app