Wamarekani na washirika wao hawawezi kukubali kuona nchi maskini ya dunia ya tatu inaongozwa na Nationalist leader kama Magufuli na wenzie waliomtangulia nchi zingine kama akina Thomas Sankara, Patrice Lumumba, Fidel Castro, Hugo Chavez, Eva Morales, Ghadaf, Kim wa NK na wengine wengi.
Kisa cha Makonda ni mapango wa muda mrefu wa kuzuwia uwezekano wa yeye Makonda na wa mfano wa Magufuli kuja kushika nchi baada ya Magufuli.
Huu ni mpango mkakati wa taassisi zao za kijasusi.
Kuchaguliwa kwa Magufuli kuwa rahisi wa Tanzania hawa mabeberu walipigwa chenga ya mwili na akina Mkapa na watu wengine nyeti walio hakikisha vibaraka wa Magharibi wanapigwa chini na Magufuli anakuwa raisi.
Hawakutegemea Magufuli atakuwa raisi, hili ni pigo kubwa sana kwao tena ni kashifa kwa taasisi zao za kijasusi ukizingatia anayo fanya Magufuli kuhusu rasilimali za taifa na mikataba kama ya EPA na AGOA.
Najua sitaeleweka na nitabezwa lakini ipo siku ukweli huu utawekwa wazi na mabeberu wenyewe miaka mingi ijayo kama walivyoweka wazi mkakati wao wa kumuandaa mrithi wa Nyerere.
Akina Kabudi, Kingwangala, na wengine mnao fanana kidogo mitizamo na Magufuli mjiandae kisaikolojia, mtakumbana na mashambulizi mengi sana hadi kufikia 2025 kwa lengo la kuwazuia msije kuwa warithi wa Magufuli.
Beberu sio mtu mzuri kabisa.
Soma hapa
Top secret CIA files expose US covert operations in Tanzania