Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Inafurahisha na kukereketa sana mwanaume kumvimbia mwanaume mwenzake! Hahhahhaa umaskni ni mbaya sn jaman wapi Ndugai jaman🤣! Wapi Lusinde? Mko wapiii😸😸
 
Kwa
Usimfananishe General wa iran na vitu vya kipuuzi, and mind you marekani ukizidi kua threat kwao lazima waku eliminate

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Nini umeamua kumjibu lakn? Yeye kwa akili yake ana mainisha kama Marekani inauwa inaowaita watu hatari wanao ratibu magenge ya ugaidi middlle East basi ni halali pia Bashite kuwauwa watanzania wakosoaji. Rejea "Roma atapatikana Jpili" pia ujue kuwa Bashite alivamia studio clouds na Askari wa Ikulu halafu Nape alipotaka kufatilia kwa kina akafukuzwa kazi na alipotaka kuongea na umma akatishiwa bastola.
 
LeMutuz nae hajatoa tamko tu

Sent from my ONEPLUS A5010 using Tapatalk
Namnukuu

FREE EDUCATION: Le Commandant RC @baba_keagan ...Kanyaga Tumechelewa Sana hili Taifa na Majungu Majungu na ujinga ujinga mabadiliko ya kweli sio mchezo maana sasa mpaka USA wanalia lia kama Watoto wadogo na majungu majungu ....

Yaani wanataka kutuaminisha Watu Wazima wenye Akili Timamu na Elimu Kubwa kwamba RC wa Dar ni mkubwa kuliko Serikali maana anawezaje kuvunja haki za binadam bila kushirikiana na Mashirika ya Dola ya Serikali? ....

hata Wamarekani wameshajua kuwa tuna Wabongo wengi ambao hawawezi kufikiri sawa sawa ndio maana na wao wameamua kujiingiza kwenye ujinga ujinga ....

Maadui wa RC wa Dar siku zote ni MAADUI WA RAIS MAGUFULI kazi yao ni kujificha ficha nyuma ya pazia la RC wa Dar kwa sababu wanajua ndiye namba one supporter wa Rais na nia ni njema kabisa wamepigana aondolewe wameshindwa maana wanashindwa kulitumia Jiji la Dar kwa mambo yao ya kuvuruga Nchi maana ukivuruga Dar una nafasi ya kuvuruga Taifa zima .....

sasa wameenda kushitaki kwa wanaowatuma ambao nao akili finyu sana America ndilo Taifa namba moja Duniani kwa kujali haki za Mtuhumiwa lakini America hiyo hiyo imemuhukumu RC wa Dar na Mkewe bila ya kuwapa .."DUE PROCESS" yaani unamuhukumu vipi Binadam bila kumpa nafasi ya kujitetea? .....

yaani America wameshindwa kumuita Balozi wetu USA na kumpiga maswali kuhusu RC wa Dar? ....mambo ya aibu sana sasa Wamarekani wanadhani sisi Wabongo wote ni wajinga hatujui kwamba tatizo lao ni Rais Magufuli sasa wanajifichia nyuma ya RC ....

Eti wanataka kuwatisha Viongozi wetu waogope kumuunga mkono hadharani Rais Magufuli maana sasa wanajua kuwa kama RC wa Dar watapigwa marufuku kwenda USA na kutangazwa in the Public hahahaha yaani ni yale yale mambo ya Wakoloni kina Carl Peters ya "DIVIDE AND RULE" ....

kwa maneno ya hukumu yao ina maana RC wa Dar na kundi lake binafsi la kuvunja haki za binadam maana ni mkubwa kuliko Serikali ndio maana USA haikuihukumu Serikali ila RC tu wa Dar hahahahahaha the biggest joke of the Century ....KAMANDA MAKONDA ...kanyaga Twende Mbele Tumechelewa Sana U know ....

KANYAGA hakuna maandamano hapa Dar bila Kibali hata USA huwezi kuandamana bila kibali ....
Pompeo TUWACHE KIDOGO U know! ..hahaha! - @lemutuz_superbran
 
Wamuondolee ul
Basi na nyie wawekeeni vikwazo. Lakini pia angalia USA hawakuficha juu ya hilo. Basi Makonda nae aweke wazi nani kamnyima haki ya kuishi.

Na usisahau kwa Makonda ni jambo linalohusu Watanzania wenzetu
Wamuondolee ulinzi tu utaona mbona watu tupo tayari kabsa ni swala la mda tu
 
ID Hazimtetei Kwakuwa Kuna Usemi Usemao Huu Sasa Ni Wakati Wa "Nyani Kumkana Mwanaye "

Mtoto Mdogo Wa Nyani Hubebwa Tumboni Muda Wote Hadi Awe Mkubwa
Ikitokea Kwa Bahati Mbaya Ama Nzuri Akaanguka Mara Wanapokimbizwa Kamwe Mama Hampokei Tena
 
Habari jukwaa hili,,

Hili swala la waziri wa Tanzania kuwa na mjadala na USA kuhusu Ban ya Makonda kutokusafiri kwenda USA limekuwa hot topic kwa sasa.Swala hili limefikia hatua ya Tanzania kutishia kuwaamuru Wamarekani kuondoka nchini!!....Kweli!!?, Kisa Makonda na baadhi ya viongozi kukatazwa kwenda Marekani!

Kabudi anashindwa kufanya opportunity cost; athari za kuwaondoa Wamarekani Tanzania ni kubwa kuliko Makonda kutokwenda Marekani. Na tuna watanzania walipa kodi wanaofanya shughuli zao huko Marekani ambao nao itabidi warudi nchini. Miradi na uhusiano wa nchi hizi utakufa.

By the way, Makonda anaenda USA kufanya nini?....kama ni maswala binafsi hamna haja ya serikali ya Tanzania kuingilia katazo lako (ni kati ya Makonda na USA) sio Mkuu wa Mkoa wa Dar na USA. Kama ni shughuli za serikali (shughuli gani ambazo mkuu wa mkoa WA DAR anaenda kuwakilisha nchi ambayo walipa kodi hatuijui?), kwanini serikali isimtume waziri mkuu?.

Wapo Watanzania wengi ambao wamekatazwa kusafiri kwenda nchi za nje, what makes Makonda so special mpaka nchi ingilie kati swala hili?

Kuna mambo mengi muhimu ya kushughulikia kwenye nchi hii sio swala la kulazimisha Makonda aruhusiwe kwenda Marekani.

Swali muhimu: Serikali ya Tanzania inamtetea Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Dar au kama raia wa Tanzania?


Sent using Jamii Forums mobile app
Kabudi anaelewa kuwa Makonda hatakiwi nina hakika kabudi angekuwa boss wake angemfukuza ila sasa anamtetea tu kwani hana la kufanya isipokuwa unafiki.
 
83200789_611871486300621_7693937448385823342_n.jpg



ZE AKILI ZANGU ZA ASUBUHI LIVE:.....MR. SUPERBRAND AKILI KUBWAZZZZ ...Kwenye Sheria kuna vitu viwili kuna "Credible Evidence" na "Credible Information".....

Marekanii kwa maandishi yao wanasema walichonacho sio "Credible Evidence" isipokuwa "Credible Information"....Katika
Statement yao kwa kifupi eneo lenye utata ni hili hapa, na I quote....

"Department has credible information that Makonda was involved in such violations in his capacity as the Regional Commissioner of Dar es Salaam"......

Now Kisheria walitakiwa kuwa na "CREDIBLE EVIDENCE" ambayo hawana ndiyo wangekuwa na uwezo hata wa kuiomba Mahakama ya The Haque au AICC kuingilia kati ....hakuna Sheria ya Taifa lolote Duniani inayomhukumu binadam yoyote kwa makosa yaliyotokana na "CREDIBLE INFORMATION" .....

hahahahahaha.....so Pompeo amechapia chapia na kukurupuka tu lakini kwa mfano RC wa Dar akiamua kuwa challenge katika Mahakama ya Dunia wataishia kuaibika sana kwa kumuhukumu wakiwa wametumia "Credible Information" zuio lao ni "Null and void" kisheria na halina uhalali......

sema kwa vile ni Nchi yao basi funika kombe tu lakini kwenye hilo tamko hawana Sheria kabisa ni Mhemuko tu ...hahahahahaha....NDIO MAANA HAPO SPIKA WAO WA CONGRESS ANAWASHANGAA SERIKALI YAKE! ....na ndio maana Rais Uhuru Kenyatta na Rutto walishinda kesi zao the Haque ilikuwa ni makosa kama haya ya "Credible Information" ..
Badala ya "CREDIBLE EVIDENCE".....yaani so far Kisheria ..
WAMEJICHORESHA..hahahahahah...I am just saying U know LE MUTUZ SUPERBRAND AKILI KUBWAZZZ U KNOW...Good Morning! - @lemutuz_superbrand
 
ID Hazimtetei Kwakuwa Kuna Usemi Usemao Huu Sasa Ni Wakati Wa "Nyani Kumkana Mwanaye "

Mtoto Mdogo Wa Nyani Hubebwa Tumboni Muda Wote Hadi Awe Mkubwa
Ikitokea Kwa Bahati Mbaya Ama Nzuri Akaanguka Mara Wanapokimbizwa Kamwe Mama Hampokei Tena

Pia huwa anajaribishwa kwa kuweekewa mawe na matunda ili achague kipi ni chakula [emoji23][emoji23]


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Author,

Hii Majalala ni takataka moja ya ajabu kutokea

Badala ya ku calm down the situation,anaweka moto zaidi,na loser ni sisi zaidi

Kasomea wapi diplomacy huyu Majalala?

Mahiga arudi,watu sober!
 
Back
Top Bottom