Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiambatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami ya Mianzini-Olemringaringa amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kuwa anahudhuria vikao mbalimbali vya maendeleo ndani ya Mkoa wa Arusha, badala ya kuwasubiri Viongozi wa Kitaifa na kuzungumzia kero mbalimbali ndani ya Jimbo lake.

Mhe. Makonda ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kutafuta huruma ya wananchi kinyume cha taratibu, akiziita kuwa ni siasa zisizokuwa za maendeleo kwa wananchi, akiagiza kuwa ni muhimu kwa Viongozi wateule na wa kuchaguliwa kushiriki vikao vya kupanga na kuamua kuhusu maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

Kauli ya Mhe. Makonda inafuatia maombi ya Mhe. Gambo aliyeomba kwa Waziri wa Ujenzi kujengewa barabara ya Kilombero pamoja na ufungaji wa taa kwenye barabara mbalimbali za Jiji la Arusha, masuala ambayo kulingana na Mhe. Makonda yalishajadiliwa na maamuzi kutolewa kwenye vikao mbalimbali vilivyofanyika chini ya Maagizo ya Mawaziri mbalimbali wa Kisekta ikiwemo Kikao cha mapema leo asubuhi kilichohudhuriwa na Waziri wa ujenzi Mhe. Abdallah Ulega na Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba.

View attachment 3194226
Gambo kabaki kumezameza mate kama kobra, hajui anataka kucheka au kulia 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Kidemokrasia aliyechaguliwa kwenye sanduku la kura ni mtu muhimu na ana sauti kuliko mteuliwa ,ni hayo
Nashangaa na Mimi na Wafuasi wa Bashite wameshikilia Bango wakati ametoa Boko.

Kwanza Gambo ana hakuna wajibu,Makonda kazi yake atoe majibu na kama hawezi ndio Hilo liko Kwa Waziri.

Sasa Makonda anaongea nini hapo Cha maana?
 
Gambo kanyong'onyea ghafla kama KASONGO.

Kasongo mbona wewo, mombali nanga.

Kisha Kasongo akameza fundo la mate huku akigugumia spana za Bashite.

KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME.
 
Gambo kanyong'onyea ghafla kama KASONGO.

Kasongo mbona wewo, mombali nanga.

Kisha Kasongo akameza fundo la mate huku akigugumia spana ya Bashite.

KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME.
Ndio hivyo amekutana na mpuuzi ambae hajui anachoongei hukunakidai kanyooka.

Na hakika hata hili Spika.anatakiwamkulikemea.

Unawezaje kumkataza mwakilishinwa wa Wananchi kuongea shida zao Kwa Kiongozi? Makonda kama.nani?
 
Nimefarijika kusikia Arusha kuna kikao cha maendeleo,Dodoma pia nilisikia wanacho na Ndugai alitoa mawazo kwa TANROAD,SASA sijui Morogoro kama vipo?Maana TANROAD kwa mwaka ukiondoa Mizani ya Mikumi kipande gani cha urefu angalau KM 30 cha lami kwenye njia zake za TANROAD sijaona wamefanya chochote ,tunaona ni kuziba viraka na kupiga rangi madaraja.
Tungependa kikao chao waje na njia ya Mzunguko kutoka Pangawe hadi Tungi ambayo kwa mwaka wa 2023 walisaini ujenzi wa njia za kata za Tungi.
Au wajenge parking ya maegesho ya maloli Kuanzia nane nane hadi msavu hadi sanga sanga ,pataamsha na kuleta msukumo wa pesa kwa maroli yanayopaki.
au wajenge njia nne kutoka Cate hotel hadi Msamvu,halafu Msamvu hadi Sanga Sanga au Mindu.na upande wa Dodoma njia nne hadi Mkundi.
Any way tuendelee tu kuwa wasikilizaji.
 
Alichokifanya Makonda hata Mh Rais hawezi fanya, unamuitaje kiongozi mwenzio mbele ya kadamnasi na camera zote zile Mjinga??
Wewe inaonekana humjui Gambo.. yaani hapo wamekutana washenzi acha wapasuane tu
 
Gambo na Makonda wote ni wafitini... acha wapasuane tu. Gambo wakati akiwa RC aliwasweka watu ndani kisa wameenda kupeleka rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali ya Lucky Vicent. Gambo, Makonda na Sabaya hawafai kwa roho mbaya.
Na hao ndio viongozi wa Arusha!
 
Nimefarijika kusikia Arusha kuna kikao cha maendeleo,Dodoma pia nilisikia wanacho na Ndugai alitoa mawazo kwa TANROAD,SASA sijui Morogoro kama vipo?Maana TANROAD kwa mwaka ukiondoa Mizani ya Mikumi kipande gani cha urefu angalau KM 30 cha lami kwenye njia zake za TANROAD sijaona wamefanya chochote ,tunaona ni kuziba viraka na kupiga rangi madaraja.
Tungependa kikao chao waje na njia ya Mzunguko kutoka Pangawe hadi Tungi ambayo kwa mwaka wa 2023 walisaini ujenzi wa njia za kata za Tungi.
Au wajenge parking ya maegesho ya maloli Kuanzia nane nane hadi msavu hadi sanga sanga ,pataamsha na kuleta msukumo wa pesa kwa maroli yanayopaki.
au wajenge njia nne kutoka Cate hotel hadi Msamvu,halafu Msamvu hadi Sanga Sanga au Mindu.na upande wa Dodoma njia nne hadi Mkundi.
Any way tuendelee tu kuwa wasikilizaji.
Bila shaka utakua jirani yangu hapa kitungwa, nimependa wazo la barabara ya tungi-pangawe.
 
Ila pia hekima ya kiungozi ni kumwambia alipokosea kiongozi mwenzako pembeni au mbele ya mamlaka yake na sio mbele ya wananch ambao hawachelewi kwenda na upepo na si hali halisi ya tukio. Kuna kitu hakipo sawa kati yao.
Kuisubiri busara kwa makonda ni sawa na kusubiri manukato mazuri kwenye shimo la choo.
 
Hakuna spana hapo Bali huyo RC hajitambui.

Ukidikiliza hoja yake Haina mashiko.Vikao anavyodai Makonda havina uwezo wa kutatua shida ya Barabara isipokuwa Viongozi wa Kitaifa

Huyo Makonda mara zote akija Rais au VP au PM Huwa anasema shida kubwa ya Arusha ni Barabara,Sasa anakuwaga hajajadili kwenye vikao?

Ni upuuzi kumkatisha mwakilishinwa Wananchi Kwa sababu za chuki binafsi.

Kama anakitaka Hilo Jimbo agombee.
Huwa nawashangaa sana wanao muona makonda eti ni kiongozi huwa nawaona wana upeo mdogo sana wa akili na fikra
 
Back
Top Bottom