Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna spana hapo Bali huyo RC hajitambui.

Ukidikiliza hoja yake Haina mashiko.Vikao anavyodai Makonda havina uwezo wa kutatua shida ya Barabara isipokuwa Viongozi wa Kitaifa

Huyo Makonda mara zote akija Rais au VP au PM Huwa anasema shida kubwa ya Arusha ni Barabara,Sasa anakuwaga hajajadili kwenye vikao?

Ni upuuzi kumkatisha mwakilishinwa Wananchi Kwa sababu za chuki binafsi.

Kama anakitaka Hilo Jimbo agombee.
Kwa nini bado ni RC wa Arusha??
 
Acha uswahili wewe.
Amesema aache kutafuta Sifa za "kijinga" hajamuita "mjinga".
Gambo mtoto wa ilala,angemtukana tusi kama Hilo pangechimbika hapo.
Mtoto wa Ilala amekuaje mbunge wa Arusha??
 
Mbona yeye ni mpenda kuongea public katika mambo mengi?

Anajisahaurisha kuwa huwa anaitisha mikutano ya hadhara na kuanza kuhoji watendaji juu ya mambo ambayo tayari yapo serikalini?

Huyu Makonda lazima ana matatizi ya kiakili Leo hii kageuka ghafla kuwa muumini wa vikao? Hataki tena habari za mambo hadharani?
Kaongea ukweli

Pambaneni na mandojo na domokaya
 
Ukicheck vizuri kwenye hiyo clips, mishipa ya kichwa imemtoka Gambo, utafikili anataka kupasuka. Hakika sisa ni shidaaa
Sio mishipa tu hata hali ya hewa inawezekana keshsachafua. Walioko karibu nae watatupatia majibu.
 
Kufanya kazi na huyu mwamba unahitaji Hekima.
Pole Gambo kwa spana, ndiyo ukubwa huo ukisikia mtu kakwepa mishale mingi ndo hii sasa.
Gambo hmuwezi Makonda hata kwa Ngumi anamkalisha 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Ukicheck vizuri kwenye hiyo clips, mishipa ya kichwa imemtoka Gambo, utafikili anataka kupasuka. Hakika sisa ni shidaaa
Lkn aliongea ukweli
Mi nimesikiliza yote
 
Huko ni kufitinisha watendaji na public. Analeta tuhuma kwenye public kwa sababu maafisa hawawezi kujitetea kwenye public. Anachosema Bashite ni kwamba ahudhurie vikao alete hizo tuhuma katika ground ambayo muhusika anaweza kujibu na kufafanua. Ikikosa majibu na kudhibitika ndio uende public
Very true
Makonda simpendi ila kwenye hili Yuko sahihi
 
Huyo Mako hilo jimbo analitaka kama chakula...Fujo zote nikijibrand tu
 
Gambo na Makonda wote ni wafitini... acha wapasuane tu. Gambo wakati akiwa RC aliwasweka watu ndani kisa wameenda kupeleka rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali ya Lucky Vicent. Gambo, Makonda na Sabaya hawafai kwa roho mbaya.
Kwa hiyo hapo wamekutana
Au ndiyo Gambo kakutana na kiboko yake 😄

Ova
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiambatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami ya Mianzini-Olemringaringa amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kuwa anahudhuria vikao mbalimbali vya maendeleo ndani ya Mkoa wa Arusha, badala ya kuwasubiri Viongozi wa Kitaifa na kuzungumzia kero mbalimbali ndani ya Jimbo lake.

Mhe. Makonda ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kutafuta huruma ya wananchi kinyume cha taratibu, akiziita kuwa ni siasa zisizokuwa za maendeleo kwa wananchi, akiagiza kuwa ni muhimu kwa Viongozi wateule na wa kuchaguliwa kushiriki vikao vya kupanga na kuamua kuhusu maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

Kauli ya Mhe. Makonda inafuatia maombi ya Mhe. Gambo aliyeomba kwa Waziri wa Ujenzi kujengewa barabara ya Kilombero pamoja na ufungaji wa taa kwenye barabara mbalimbali za Jiji la Arusha, masuala ambayo kulingana na Mhe. Makonda yalishajadiliwa na maamuzi kutolewa kwenye vikao mbalimbali vilivyofanyika chini ya Maagizo ya Mawaziri mbalimbali wa Kisekta ikiwemo Kikao cha mapema leo asubuhi kilichohudhuriwa na Waziri wa ujenzi Mhe. Abdallah Ulega na Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba.

View attachment 3194226
Tatizo la makonda ni kujiona yupo juu ya kila mtu, mkuu wa mkoa huwezi kuongea na waziri unampiga piga bega kama hawara yako huo ni utovu wa nidhamu mkubwa sana na ni dharau kabisa, nayote hiyo inatokana na kujiona yuko juu na ana nguvu pamoja na kwamba cheo chake ni cha chini.
 
Pamoja na Yote bado RC makonda amezingua sana Kumdharirisha Gambo mbele Ya kandamnasi tena Kiongozi aliyechaguliwa na Wananchi hio haijakaa Poa, Kesho Gambo akiwa Boss wake?

Makonda ajifunze Kuheshimu Viongozi wenzie mana hata Chongolo aliwahi Kumkolomea wakati ni RC Dar baadae tuliona Chongolo anakuja kuwa Boss wake hii haijakaa Poa ivo Viti vya Kuteuliwa una Serve at the wish ya aliyekuchagua Tusijione sana tumefika
Makonda ni mtu anayejionaga bora kuliko wengine na si mtu wa kufuata protokali. Sema wote masnitch wamekutana.
 
Back
Top Bottom