Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Mimi sifanyi kazi kwa ajili ya malipo na sipo CCM kwa ajili ya kulipwa.nipo CCM kwa sababu ni chama kinachojali na chenye uchungu na maisha ya watu na chenye itikadi inayoeleweka na yenye kugusa maisha ya watanzania. Sasa mavyama kama CHADEMA hayawezi hata kuandaa ilani yake. Rejea 2015.
Kweli wanatujali, mtaani kwangu umeme hakuna kuna dogo hapa ni jirani ana saloon kakosa buku ya kupata breakfast
 
Mimi sifanyi kazi kwa ajili ya malipo na sipo CCM kwa ajili ya kulipwa.nipo CCM kwa sababu ni chama kinachojali na chenye uchungu na maisha ya watu na chenye itikadi inayoeleweka na yenye kugusa maisha ya watanzania. Sasa mavyama kama CHADEMA hayawezi hata kuandaa ilani yake. Rejea 2015.
Bro acha ujinga basi unajizima data. Haya majizi yana uchungu na nani labda na matumbo ya na watoto wao. Kwa ufisadi na dili wanazopiga tu wakipumzika mwaka 1 tu nchi itasogea ile wako busy usiku na mchana.
 
CCM na Serikali yake ndio mlinzi wa mali na rasilimali za Taifa letu anayeaminika na kila mtanzania mzalendo.matapeli yapo huko CHADEMA ambako wanatafuna hadi michango ya watu.
 
CCM na Serikali yake ndio mlinzi wa mali na rasilimali za Taifa letu anayeaminika na kila mtanzania mzalendo.matapeli yapo huko CHADEMA ambako wanatafuna hadi michango ya watu.
ULAANIWE WEWE NA KIZAZI CHAKO KWA KUTETEA WATU AMBAO WANATUUMIZA....popote utakapotembea sauti za manung'uniko juu ya shida ambazo wananchi wanazipata ziwe ndani ya nafsi yako.
 
ULAANIWE WEWE NA KIZAZI CHAKO KWA KUTETEA WATU AMBAO WANATUUMIZA....popote utakapotembea sauti za manung'uniko juu ya shida ambazo wananchi wanazipata ziwe ndani ya nafsi yako.
Fanya kazi na timiza wajibu wako na siyo kutaka majukumu na wajibu wako katika maisha ubebwe na mtu mwingine. Mafanikio yako yapo katika mikono yako mwenyewe.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Fahamu ya kuwa Ndugu Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa,yule mwamba wa siasa za majukwaani na ambaye anachukuliwa kama sauti ya wanyonge na ambaye alitangaziwa Mwisho na maadui zake lakini Mungu akatangaza Mwanzo,ambaye kwake zege halilali,na ambaye anatajwa kama kijana jasiri sana katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.

Ambaye akizungumza na kuanza ziara basi nchi yote husimama,vyombo vyote vya habari hushindana kupamba picha zake kurasa za mbele na mitandao yote hutekwa na habari zake na ambaye amekuwa kiboko ya CHADEMA anakwenda kuitikisa na Kuitetemesha mikoa kumi mfululizo kwa ziara ambayo inasubiriwa kwa hamu sana na mamilioni ya watanzania ambao walikuwa wanamsubiri kwa hamu kuwafikia huko waliko ili wamueleze kero zao kusudi azipeleke serikalini.

Sasa kama ulikuwa na shughuli yako au biashara yako unataka kuitangaza kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii,basi nakushauri usipoteze muda ,ni bora usubili huyu mwamba amalize ziara yake ,maana kwa sasa anakwenda kuiteka nchi yote kimijadala na watu wote wanakwenda kutega masikio yao kusikiliza nini anazungumza na nini kinajiri katika ziara zake.

Kama wewe ni msanii na ulipanga kutoa wimbo wako basi ni bora uuweke kwanza pembeni mpaka Mheshimiwa amalize ziara zake,maana akishaingia mitaani huyu basi wimbo utakuwa ni mmoja tu ambao ni Makonda na utekelezaji wa ilani ya CCM tu.

Endeleeni kutulia Watanzania wenzangu maana najuwa mlimkumbuka sana na mlikuwa na hamu ya kumsikiliza mwamba akiunguruma kama Simba majukwaani.sasa amewasikia na anakuja kwa kishindo.

Watendaji wa serikali na wateule wa Mheshimiwa Rais andaeni majibu ya kila kitu juu ya kazi mnazofanya na kusimamia katika utekelezaji wa ilani ya CCM Katika maeneo yenu.Maana huyu mwamba huwezi kujuwa atakupiga wapi.kumbuka huyu ni msemaji wa chama na mjumbe katika vikao vyote muhimu vya CCM. sasa wewe lete nyodo zako huko uone kitakachokupata atakaporejea kupeleka mrejesho kwa chama juu ya aliyoyabaini mikoani huko na akina nani wanakichonganisha chama na wananchi au wanatesa wananchi au hawatoi huduma stahiki kwa wananchi au wanapuuza wananchi au hawawasikilizi wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Labda atetemeshe kalio.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Simba wa Serengeti.

Kipenzi cha watanzania.

Jamaa linapendwa sana hili halafu amekaa kimamlaka ukimuona tu unajua yes huyu kiongozi..

Itoshe kusema jamaa ana nyota ya uongozi.
Siku moja huyu jamaa atakuja kuwa Rais wa nchi hii nipo nimekaa pale.

# Makonda mbele kwa mbele
 
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Naona unazidi kuboresha utambulisho tu huku mikeka ikiendelea kukupita.

Tatizo uchawa unaufanyia kijijini huko na connection huna. Stuka acha ushamba, uchawa unalipa mjini si vijijini huko. Huwaoni chawa wenzio akina baba revo, mwijaku nk?

Unategemea connection za teuzi ufanyiwe na katibu wa sisiemu ngazi ya tawi au kata? Utajitambulisha hadi mtoto wa Yesu na bado utazeekea uchawani, shauri yako.

Hao akina bashite wafuate hukohuko mjini tafuta connection wakupe hata kinarua cha kuwabebea mabegi uwe busy uepuke kujidhalilisha humu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba wa Serengeti.

Kipenzi cha watanzania.

Jamaa linapendwa sana hili halafu amekaa kimamlaka ukimuona tu unajua yes huyu kiongozi..

Itoshe kusema jamaa ana nyota ya uongozi.
Siku moja huyu jamaa atakuja kuwa Rais wa nchi hii nipo nimekaa pale.

# Makonda mbele kwa mbele
Umenena kweli kabisa.Mheshimiwa akisimama jukwaani hata popote pale na kuzungumza unaona kuwa ni kiongozi kasimama kuzungumza .
 
Simba wa Serengeti.

Kipenzi cha watanzania.

Jamaa linapendwa sana hili halafu amekaa kimamlaka ukimuona tu unajua yes huyu kiongozi..

Itoshe kusema jamaa ana nyota ya uongozi.
Siku moja huyu jamaa atakuja kuwa Rais wa nchi hii nipo nimekaa pale.

# Makonda mbele kwa mbele
Labda wenye akili timamu wote tukishafariki.
 
Back
Top Bottom