Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #141
Ndugu zangu Watanzania,
Ukiachana na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Samia ambaye nchi hii ameizunguka yote kama ilivyo mwaka 2015 na hata 2020, kuna mwamba mwingine aliyekuja na kuinuliwa katika namna ya kipekee sana .
Paul Makonda ni Mwamba kwelikweli, Ni jemedari na komandoo wa vita ya kumtetea mtanzania mnyonge. Amejaliwa uwezo ,stamina na nguvu isiyo ya kawaida katika hali ya kibinadamu.
Siyo jambo jepesi wala dogo kwa mtu wa kawaida asiye na misuli ya uvumilivu,uzalendo na upendo kwa watu ,anayeweza kufanya ziara katika mikoa 20 mfululizo bila kupumzika hata siku moja katika kutega masikio kwa unyenyekevu mkubwa kuwasikiliza Watanzania wanyonge.
Hii ni rekodi ,hii ni historia aliyojiandikia kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara Paul Christian Makonda katika ardhi ya Tanzania .amezungumza na Anaendelea kuzungumza kwa ujasiri wa hali ya juu sana ,katika kuwasemea watanzania wanyonge wasio na sauti mpaka wakati mwingine sauti inakuwa ni kama inaisha.
Amesikiliza kila aina ya kero ,kila aina ya sauti,kila aina ya kilio.amejionea maumivu ,machungu ambayo baadhi ya watu wameyabeba katika vifua vyao ,ambapo wakianza kueleza madhira yanayowasibu wanaishia kububujikwa na machozi ya uchungu kabla ya kufika mwisho. amesikiliza vilio vya watu waliodhulumiwa ardhi,walionyimwa haki zao ,waliopokonywa ardhi zao na wenye pesa,waliotekwa, walioporwa mali zao kwa uonevu.
Amesikiliza kwa uchungu sauti za wajane,sauti za wenye ulemavu,sauti za wazee,sauti za yatima zote kwa pamoja amezisikia katika masikio yake .amesikiliza Sauti za watanzania wa aina zote.
wakati mwingine hata yeye uchungu umemshika na kumuelemea moyoni mwake pale anaposikiliza kero na mapito ya watu. Kwa hakika ukifuatilia na kusikiliza yale yanayokuwa yanajitokeza huko unabaki unasema kwanini watu wengine hawana moyo wa huruma kwa watu? Kwanini mtu huyu ametendewa hivi?
Paul Makonda ni kioo kinachomulika na kuonyesha mengi sana huko mikoani na wilayani. Kwa hakika ziara za Mheshimiwa Makonda zitamsaidia sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan kujuwa na kupata taswira ya utendaji kazi wa viongozi waliopo huko.
Afanyayo Mheshimiwa Makonda siyo jambo analoweza kila mtu na kila kiongozi. wengi wameshindwa na kukaa maofisini tu wakijizungusha kwenye viti. wakati watu hao wamepewa magari ya serikali,mafuta full tanki,dereva na kila kitu ,lakini huwezi ukaona wakitoka maofisini mwao kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuwapa majibu.
unakuta mtu yupo ofisini mwaka hadi mwaka na hajawahi kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao.ndio maana kuna kuwa na mabango mengi kutoka kwa wananchi kueleza kero zao pale viongozi wakuu kitaifa wanapofanya ziara katika maeneo hayo.Kana kwamba maeneo hayo hayana viongozi au wote wapo rikizo makwao.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.