Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Mimi ni msema kweli tu ndugu yangu.
Jipige kifua chako mara tatu, na kutamka, "mimi nimekuwa punguani. Njaa imenifanya niwe punguani. Nimeamua kuwa mnafiki kiasi cha kupoteza ubinadamu wangu kwa sababu ya njaa inayosababishwa na uvivu wangu. Ndugu zangu nisaidieni maana uwezo wangu umefikia ukomo"
 
Ndugu zangu Watanzania,

Fahamu ya kuwa Ndugu Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa,yule mwamba wa siasa za majukwaani na ambaye anachukuliwa kama sauti ya wanyonge na ambaye alitangaziwa Mwisho na maadui zake lakini Mungu akatangaza Mwanzo,ambaye kwake zege halilali,na ambaye anatajwa kama kijana jasiri sana katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.

Ambaye akizungumza na kuanza ziara basi nchi yote husimama,vyombo vyote vya habari hushindana kupamba picha zake kurasa za mbele na mitandao yote hutekwa na habari zake na ambaye amekuwa kiboko ya CHADEMA anakwenda kuitikisa na Kuitetemesha mikoa kumi mfululizo kwa ziara ambayo inasubiriwa kwa hamu sana na mamilioni ya watanzania ambao walikuwa wanamsubiri kwa hamu kuwafikia huko waliko ili wamueleze kero zao kusudi azipeleke serikalini.

Sasa kama ulikuwa na shughuli yako au biashara yako unataka kuitangaza kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii,basi nakushauri usipoteze muda ,ni bora usubili huyu mwamba amalize ziara yake ,maana kwa sasa anakwenda kuiteka nchi yote kimijadala na watu wote wanakwenda kutega masikio yao kusikiliza nini anazungumza na nini kinajiri katika ziara zake.

Kama wewe ni msanii na ulipanga kutoa wimbo wako basi ni bora uuweke kwanza pembeni mpaka Mheshimiwa amalize ziara zake,maana akishaingia mitaani huyu basi wimbo utakuwa ni mmoja tu ambao ni Makonda na utekelezaji wa ilani ya CCM tu.

Endeleeni kutulia Watanzania wenzangu maana najuwa mlimkumbuka sana na mlikuwa na hamu ya kumsikiliza mwamba akiunguruma kama Simba majukwaani.sasa amewasikia na anakuja kwa kishindo.

Watendaji wa serikali na wateule wa Mheshimiwa Rais andaeni majibu ya kila kitu juu ya kazi mnazofanya na kusimamia katika utekelezaji wa ilani ya CCM Katika maeneo yenu.Maana huyu mwamba huwezi kujuwa atakupiga wapi.kumbuka huyu ni msemaji wa chama na mjumbe katika vikao vyote muhimu vya CCM. sasa wewe lete nyodo zako huko uone kitakachokupata atakaporejea kupeleka mrejesho kwa chama juu ya aliyoyabaini mikoani huko na akina nani wanakichonganisha chama na wananchi au wanatesa wananchi au hawatoi huduma stahiki kwa wananchi au wanapuuza wananchi au hawawasikilizi wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Labda akutetemeshe wewe na mabwege wenzako waabudu wanaadamu wenzenu kwa tamaa ya vyeo na madaraka.
 
Kibaraka asiyelipwa.
Wenzie wako mezani wanakula yeye Yuko chini ya meza anasubiri mifupa.
Kwani hujui watu wanapokula mezani wanaweza kuwa wametulia, LAKINI mbwa ambaye yupo pembeni akisikia harufu ya vinono, huwa anahangaika na kutikisa mkia ili walaji wa nyama wamwone na kumrushia mifupa? Mwashambwa anatikisa mkia, ndiyo maana kila mara anarusha kanamba kake ka simuili arushiwe hata mifupa maana anaisikia halafu ya chakula ambacho binadamu wanakula yeye akiwa mbali na meza ya chakula, huku akiamini masazo ya chakula yanaweza kurushwa kwenye jalala lililo karibu naye.
 
Kwani hujui watu wanapokula mezani wanaweza kuwa wametulia, LAKINI mbwa ambaye yupo pembeni akisikia harufu ya vinono, huwa anahangaika na kutikisa mkia ili walaji wa nyama wamwone na kumrushia mifupa? Mwashambwa anatikisa mkia, ndiyo maana kila mara anarusha kanamba kake ka simuili arushiwe hata mifupa maana anaisikia halafu ya chakula ambacho binadamu wanakula yeye akiwa mbali na meza ya chakula, huku akiamini masazo ya chakula yanaweza kurushwa kwenye jalala lililo karibu naye.
Sina njaa ya chakula wala ya chochote kile wala kuhitaji malipo kama unavyofikiria wewe
 
Jipige kifua chako mara tatu, na kutamka, "mimi nimekuwa punguani. Njaa imenifanya niwe punguani. Nimeamua kuwa mnafiki kiasi cha kupoteza ubinadamu wangu kwa sababu ya njaa inayosababishwa na uvivu wangu. Ndugu zangu nisaidieni maana uwezo wangu umefikia ukomo"
Mimi sina njaa hata kidogo ndugu yangu.mimi ni mkulima na nina kula kwa jasho langu mwenyewe na siyo kulishwa au kutegemea misaada
 
Wewe, unafiki umekufanya kuwa punguani. Jielimishe.

Unamfahamu aliyemwua Gadafi? Kulikuwa na askari hata mmoja aliyekuwa kwenye ground ili kumwua Gadafi?

Hivi Gadafi aliyekuwa anawaua wanaohoji utawala wake na kuwazika kwenye makaburi ya pamoja, ilikuwa ni halali?

Sadam Hussein, ni kweli aliondolewa kwa operation za kijeshi zilizoongozwa na Marekani, Ufaransa, Uingereza, zikisaidiwa na mataifa mengine 46, ; chini ya azimio la Umoja wa mataifa. Sadam Hussein aliyewahi kuwaua watu wake waliokuwa wakipinga utawala wake kwa kuwamwagia gas ya sumu iliyoua kila kiumbe, mpaka watoto na wanyama, kwako wewe punguanu, unaona ilikuwa ni sahihi?

Hivi unaamini wewe kwa huo upunguani ulio nao, unaamini unauelewa zaidi ya mataifa 49, yakiwemo mataifa ya Kiarabu na Afrika yaliyoamua kuwasaidia Waraq kuondokana na utawala wa dictator Sadam Hussein?

Countries participated in the US-led coalition: Afghanistan, Albania, Australia, Azerbaijan, Bulgaria, Colombia, the Czech Republic, Denmark, El Salvador, Eritrea, Estonia, Ethiopia, Georgia, Hungary, Iceland, Italy, Japan, South Korea, Latvia, Lithuania, Macedonia, the Netherlands, Nicaragua, the Philippines, Poland, Romania, Slovakia, Spain, Turkey, the United Kingdom and Uzbekistan.[9]

On March 20, 2003, the White House released a list with the following additions: Costa Rica, the Dominican Republic, Honduras, Kuwait, the Marshall Islands, Micronesia, Mongolia, Palau, Portugal, Rwanda, Singapore, Solomon Islands, Uganda.[9][2] Panama was added to the list the next day.[2] In April 2003, Angola, Tonga and Ukraine were included in the list, bringing the number of allied nations to 49.
Ndege za NATO hazikuteja nankutawala anga la libya? Sasa kwa akili yako kisoda NATO ni akina nani?
 
kina mbowe watajuta kua wapinzani walah
si kwa uchapaji kwazi huu uliotukuka wa chama cha mapinduzi
Mbowe anatamani kuhamia CCM ila anataka mpaka ahakikishe CHADEMA inabakia mifupa mitupu kwa kuinyonya huku manyumbu wake wasiojitambua wakiendelea kupiga makofi na kushangilia kama mahayawani tu.
 
Back
Top Bottom