Paul Makonda: Sijawahi kuvamia Clouds Media. Nimetumika sana na Clouds, Ruge alikuwa ananipigia sana simu

Kwa kauli yake hiyo kwamba aliwasaidia clouds kusort vimeo vyao kwa TCRA ambapo kwa hakika ilikuwa anakiuka sheria na taratibu za nchi. Hii inatosha sana jamaa kupoteza nafasi na uhaminifu wa kupewa ofisi ya umma. Anatakiwa kutenguliwa haraka sana
 
Haya sawa tuseme hukuvamia, kwanini hukutaka kuhojiwa na kamati iliyoundwa na waziri Nape kwa wakati huo?

Ni suala hili hili la clous lilimfanya Nape atumbuliwe, hata alipotaka kuongea na wanahabari yaliyojir alitishiwa na bastola mbona kwenye hilo hajaongelea. Anajikangaga kanyaga asifikiri tumesahau
 
Kwa kauli yake hiyo kwamba aliwasaidia clouds kusort vimeo vyao kwa TCRA ambapo kwa hakika ilikuwa anakiuka sheria na taratibu za nchi. Hii inatosha sana jamaa kupoteza nafasi na uhaminifu wa kupewa ofisi ya umma. Anatakiwa kutenguliwa haraka sana
Wanasema ukweli sasa alianza Nape akapewa rungu la kichwa
 
...kamati iliyoundwa na waziri Nape kwa wakati huo?...
Kwa wakati huo, Makonda alikuwa anawajibika kwa wananchi kupitia Mamlaka ya uteuzi wake na Ile tume ya maadali. Nape wakati huo Hakuwa na legal ama administrative basis kumuweka kiti moto Makonda!! Sidhani kama nimekosea kwenye ujengaji huu wa hoja!
 
Hii Nchi beans inaendeshwa kihuni Sana. Kwa Hiyo Makonda ameona huu ndio wakati wake WA kujisafisha au anautaka Ubunge wa Arusha mjini?
 
Hiyo imeundwa na Nape ilioundwa na Mwakiembe inasemaje? Kama ungekuwa umemsikiliza ungekuwa umeshapata majibu
 
Paulo Makonda alivyo mkosa akili anaona fahari kwamba alikuwa anatumia mamlaka yake kuzuia vyombo vya serikali kama TCRA kutimiza wajibu wake, without shame hicho ni kitu cha kuwa proud of. FCK OFF.
 
Kwa wakati huo, Makonda alikuwa anawajibika kwa wananchi kupitia Mamlaka ya uteuzi wake na Ile tume ya maadali. Nape wakati huo Hakuwa na legal ama administrative basis kumuweka kiti moto Makonda!! Sidhani kama nimekosea kwenye ujengaji huu wa hoja!
Kumbuka kile ni chombo cha habari, alikuwa na dhamana ni waziri wa habari, so kwa Nape alikuwa sahihi, ndio maana akasema hiyo ripoti ataipeleka kwa wakuu wake, means waziri Mkuu, Raisi na makamu wa Raisi hao ndio walikuwa wakubwa kwa Nape..

Waziri na Mkuu wa Mkoa wote ni wateule wa Raisi, labda tuulizane nani ambaye yuko juu ya mwenzake kiutendaji?
 
Bora angeendelea kukaa kimya,amechafuka na anazidi kujichafua,sijui kwanini watu wa namna hii wanaendelea kupewa dhamana ya kuongoza watu wakt ata kujiongoza wenywe wanashindwa.
Ukimwangalia aliyemteua Makonda, unadhani ana Iq bora kumzidi Makonda ?
 
Namaanisha kumtaja katika tuhuma mbalimbali zinazo hitaji muhusika atoe majibu au utetezi.
Mfano utekaji na mauwaji.
Kumtaja marehemu katika jambo linalohitaji uhakiki zaidi kunahitaji ushahidi zaidi.

La sivyo, tutajuaje kilichosemwa ni ukweli na si hadithi ya kutungwa tu ambayo imesemwa kwa sababu marehemu hayupo kunyoosha maneno?
 
First things first, the sun does not rise, it appears to rise.

And even that appearance will not always be there for every tomorrow. That is against the laws of physics.

The sun has a finite amount of energy to burn and in a few billion years will not appear to rise. The earth will be devoured.

So much for your malnourished physics.
 
Waziri na Mkuu wa Mkoa wote ni wateule wa Raisi, labda tuulizane nani ambaye yuko juu ya mwenzake kiutendaji?
Majibu umeisha yatoa, hivyo umehitimisha kuwa tume ya Nape haikuwa na uwezo wa kumuhoji Mheshimiwa Makonda
 
Hapo kwenye uvamizi wa Clouds Makonda amejichanganya, na huenda amekiri kukiuka maadili ya utumishi wa umma. Kuna ripoti ya uchunguzi ilitoka ikimtuhumu kuvamia. Pia nadhani hata watendaji wa Clouds walijitokeza kulaumu uvamizi huo. Sasa kama Makonda amedanganya ktk suala hili itakuwa shida sana kuamini majibu yake ktk tuhuma nyingine. Nadhani alikuwa anakwenda vizuri alipoamua kukaa kimya. Majibu haya Makonda hawezi kuyafuta.
 
Sawa mzee wa AI. Maana kwa kebehi nitakuwezaje!? H ahahaha aa! Na umeleta hii kebehi makusudi kuzuia kuhojiwa zaidi kwenye nyanja hii na "sane people".
====
Hapana. Nimekuonesha kwamba hujui unachoandika.

Kwa kuanzia na habari hiyo tu ya jua, umekubali hukujua ulichoandika ili tuimalize hii fake news tuendelee na mengine?

Nimeanza kwa kuandika "first things first" kwa makusudi.

Hapo nimeanzia tu, sijamaliza bado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…