Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Anagombea hapo na shaka anagombea kilosa. Wewe nina wasiwasi utakuwa unapewa za ndaaani sana maana sio wengi wanajua hili.
 
Amekula "maharagwe-uvundo" na mayai yaliyochemshwa.Afadhali yangekuwa maharage tu.Maana kuna tofauti kati ya maharage na maharagwe.
Asichojua ni kuwa siasa za Arusha ni tofauti na mkoa mwingine TANZANIA.

Wanaweza wakawa viongozi 20 wa sisiem na wakipiga kura ya Siri kuchagua kati ya sisiem na CHADEMA ukahesabu kura utakuta asilimia kubwa wamempigia wa CHADEMA na sio wa Chama Chao Cha CCM.

Siasa za Arusha kiongozi mkubwa anafungua shina la wakereketwa bila kujua ni la wanachadema.


Siasa za Arusha ni kama tikiti maji (watermelon)
Kwa nje kijani; ndani jekundu.

Ndio sababu tangu miaka ya 90 jimbo la Arusha mjini limekuwa likichukuliwa na upinzani tu.

This is Arusha
 
Muda ndiyo kila kitu, kwa muda huukuwa na majibu ni mapema sana
 
Duh aiseee
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
 
Shaka mzanzbari
So what..??
Kama Mzanzibari anapewa hadi ukuu wa wilaya utashangaa kuwa mbunge..?
Kwanza kwa taarifa yako sasa, shaka ana ndugu wengi sana Morogoro na kilosa, sijui upande wa nani kwenye familia yake wanatokea Morogoro but wapo wengi sana.
 
Kwahiyo tuache kuzungumzia kikokotoo na nyongeza ya mshahara tuanzie zungumzia wadudu na ubunifu WA Makonda. Watz tumelogwa
 
Samia kaogopa kwenda Arusha upepo WA lissu unatisha
 
Umepinda hadi ubongo. Huo kwako ulikuwa ni mkutano wa siasa wa Mkuu wa Mkoa????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…