Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Anagombea hapo na shaka anagombea kilosa. Wewe nina wasiwasi utakuwa unapewa za ndaaani sana maana sio wengi wanajua hili.
 
Amekula "maharagwe-uvundo" na mayai yaliyochemshwa.Afadhali yangekuwa maharage tu.Maana kuna tofauti kati ya maharage na maharagwe.
Asichojua ni kuwa siasa za Arusha ni tofauti na mkoa mwingine TANZANIA.

Wanaweza wakawa viongozi 20 wa sisiem na wakipiga kura ya Siri kuchagua kati ya sisiem na CHADEMA ukahesabu kura utakuta asilimia kubwa wamempigia wa CHADEMA na sio wa Chama Chao Cha CCM.

Siasa za Arusha kiongozi mkubwa anafungua shina la wakereketwa bila kujua ni la wanachadema.


Siasa za Arusha ni kama tikiti maji (watermelon)
Kwa nje kijani; ndani jekundu.

Ndio sababu tangu miaka ya 90 jimbo la Arusha mjini limekuwa likichukuliwa na upinzani tu.

This is Arusha
 
Muda ndiyo kila kitu, kwa muda huukuwa na majibu ni mapema sana
 
Shaka mzanzbari
So what..??
Kama Mzanzibari anapewa hadi ukuu wa wilaya utashangaa kuwa mbunge..?
Kwanza kwa taarifa yako sasa, shaka ana ndugu wengi sana Morogoro na kilosa, sijui upande wa nani kwenye familia yake wanatokea Morogoro but wapo wengi sana.
 
Kwahiyo tuache kuzungumzia kikokotoo na nyongeza ya mshahara tuanzie zungumzia wadudu na ubunifu WA Makonda. Watz tumelogwa
 
Hakika hiki ni kichekesho! Katika siku muhimu kama Mei Mosi kwa wafanyakazi.wanaowazia hatima ya kazi zao, mishahara na mafao yao ya kustaafu, pension zao, kupandishwa vyeo na kila linalowasibu eti ndio haya tena ya Makonda?
Mbele ya makamu wa Rais anayemwakilisha Rais mnasema bila aibu kuwa Makonda ni mbunifu kisa WADUDU?
Yaani bila aibu mnaleta vijana wakuwapeleka Rehab mbele ya Rais, mabalozi na wakuu wengine wakiwapo WAFANYAKAZI WATUKUFU?
Mbona toka aseme anawajua wanaolipa wamtukanao Rais sasa kujipendekeza kwake kumekuwa kukubwa kama kuogopa wasitajwe?
WADUDU NDIO UBUNIFU WA MAKONDA?!

View: https://youtu.be/aFZXjQc901U?si=08otvhLulbWRB6VL

Samia kaogopa kwenda Arusha upepo WA lissu unatisha
 
Mwamba Makonda anawatesa sana wapinzani na nyumbu wa CHADEMA. Mafuriko yaliyomiminika leo uwanjani mpaka wengine kukosa nafasi na kuamua kubakia nje ya uwanja kumewaumiza na kuwatetemesha sana sana CHADEMA, mpaka sasa wamebaki wanaweweseka tu kama wagonjwa wa malaria kali. Hapo bado Mwamba hajamaliza hata nusu mwaka.
Umepinda hadi ubongo. Huo kwako ulikuwa ni mkutano wa siasa wa Mkuu wa Mkoa????
 
Back
Top Bottom