Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kijana wao hafundishwi kumezea ya OVYO.

Hahahah ,maadili gani? Wajumbe wa kamati ya maadili ya CCM ni waking nani ? Nasi tufanye tafiti za uadilifu wao kwanza.

Siasa za kizamani sana za kijiji kimoja CCM wanapaswa kuachana nazo ......
 
Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigumu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.

Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.

Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.

Historia hii inatufundisha nini?

Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ila hakukutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwenye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.

Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.
 
Huyu Mzee hua ananiacha hoi sana, Kuna siku alihojiwa akaulizwa unazungumziaje hali ya sasa ya maisha ya watanzania.... Akajibu


"Mimi niliwaambia wanichague Mimi wawe wanakula ubwabwa bure na matunda Kila Kona niliwaambia ntawapandia miti wakakataa, waache wapambane"
 
Taarifa za jogging basi tena ni makonda tu!
 
Mkapa ni maji marefu sana, ndiye aliijenga nchi ikakaa kimfumo, japo na yeye akikuwq na mapungufu yake, Dar iliacha kumuimba Mwaibula ikaanza kuimba SUMATRA na LATRA
 
TOKA MAKTABA

CCM na bunge lake pamoja na kamati za maadili ya CCM lao moja ...

2017 29 March

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

View: https://m.youtube.com/watch?v=TVUFE2rzX5I
Kamati ya Haki, maadili na madaraka ya Bunge imemuhoji mkuu wa mkoa wa Daresalam Paul Makonda anayetuhumiwa kuingilia haki, uhuru na madara ya bunge kufuatia kauli yake ya kwamba wabunge wanasinzia Bungeni jambo lilotafsiriwa kuzarau chombo hicho ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…