Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Huwajui wameru wewe. Unaikumbuka vita ya kugombea dayosisi ya kaskazini KKKT miaka ya 90 kati ya moshi na arusha? JWTZ ndio walikuja kutuliza hiyo vita ogopa mchungaji anaongoza ibada na panga limechomoza kwenye kanzu.
johnthebaptist kama unakumbuka elezea mawili matatu najua wewe ni Mlutheri nahisi 🤣
Kaskazini haswa wakristo wengi wana imani wameru wamelaaniwa, kuna watumishi wa Mungu walienda kuwahubiria wakawaua..
 
Yaaan wewe ni wakumtisha RC? Wameru ndio jeshi gani inchi hiiiiii?

RC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na jeshi la polisi limo kwenye kamati, RPC wa Arusha yupo chini ya Makonda (polisi wana vituo karibia kila kata nchi hii)

Kwaiyo taarifa za usalama za mkoa mzima zipo ofisini kwa Makonda

Mmeru na Masai nani kiboko, sasa kama masai wamefyata wanahama Ngorongoro, hebu kuwa na akili basi
Masai siyo korofi kama meru
 
Makonda kula nao Shahani Moja hao wanaojita wadudu..

FUTA usafiri wa vipanya katikati ya Jiji...

Masoko wapangwe Kwa mstari

Majengo yapakwe rangi

Usafi
Nk
Hizo ni kazi za halmashauri ya jiji sio kazi yake, just a president stooge
 
Huyo ndiye Makonda Mwamba kama Mwamba.kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara. Mtu aliyetangaziwa mwisho na Maadui zake lakini Mungu akautangaza mwanzo wake wa ushindi wa kishindo.kiongozi aliyeinuliwa na Mungu na kupewa kibali mkononi mwake.kiongozi mwenye ushawishi na anayependwa kama pesa. Kiongozi anayechanua muda wote utafikiri bustani ya kitalii.
Umwamba wake akiwa kifuani mwako tu
 
"Kama akifanya" is right.

Akifanya hata robo ya aliyoahidi atakuwa amefanya mengi kuliko marais na mawaziri wengi wa nchi hii na Afrika kwa ujumla.

Sijawahi kusikia kiongozi anaeamini nchi hizi za dunia ya tatu umefika wakati kufuta squatters and slums, kufuta uswahilini. Wataalam wa Mipango miji Makonda anawaambia wanaona uswahilini zinaanzishwa mbele yao, vichochoro na mifereji ya maji machafu ya uswekeni, zinajengwa wanaziangalia, ni wataalam mipango miji wa kubumba. Acha aendelee kuwachanaaa
!
Ila Arusha ni pa hovyooo mitaa mingi ni uswekeni
 
MAKONDA AAINISHA MPANGO KAZI WA VIPENGELE SITA:
LETS MAKE ARUSHA GREAT AGAIN!


April 8, 2024
Arusha


⦁ Mapokezi yamenitia moyo wa kuwa mtumishi mwema na mtetezi wa wanyonge. Kamwe sitaungana na fisadi kukandamiza haki zenu, nitakuwa sauti yenu mpaka ukamilifu wa dahali

⦁ Nawashukuru kwa maombi. Kwa dua njema mlionifanyia. Nimekoswa koswa mara tatu kupoteza maisha, na nawaambia, sitakufa bali nitaishi. Niyasimulie matendo makuu ya Mungu.

Nina mambo au mawazo sita. Lakini lazima nifanye kwanza ziara mniambie, ili yale tunayowaza sisi yafanane na majibu ya changamoto zenu. Nakuja kwenye wilaya zote sita tukutane. Ili kusudi tupate sauti moja.

La Pili: Hakuna maendeleo bila umoja. Tukishikamana bila kujali dini, kabila, chama, tutapiga hatua. Mkoa usiwe wa malumbano ya kisiasa, bali mkoa wa kujenga uchumi imara, na wa biashara kwa watu wake.

⦁ Sijaja kukandamiza wanasiasa. Sijaja kutangua torati. Wapinzani mkitaka kunishirikisha mnishirikishe. Mkitaka hata mafuta kama tunaweza tutachangia.

Jambo la tatu, najua Arusha ni mji wa kitalii. Rais Samia ameipendelea Arusha, hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje aungane nanyi. Takwimu za serikali za sekta ya utalii zinatofautiana kati ya Maliasili, na RAS wa Mkoa, na Bodi ya Utalii. Unajiuliza, hawa watu si ni serikali moja ? Which means vyumba hakuna! Kumbi za mikutano hakuna. Tutajenga kumbi mbili kubwa za mikutano. Tutajenga apartment ya vyumba 400, na kiwanja cha mpira cha watu 30,000. Tuache siasa za kunyoosheana vidole, hazituingizii pesa.

Jambo la nne. Ninalo tangazo jema kwa yeyote anaedai haki yake: Kwa neema na mapenzi ya Mungu utaipata. Kama niko nimekanyaga mahali hapa, na nina kibali cha Rais, basi haki yako utaipata. Hujui kusoma, hujui kuongea ukaeleweka, huna hela, nitakulinda na kukupigania!

Jambo la tano. Watendaji na watumishi wote Arusha popote ulipo, funga mkanda! Mkurugenzi, RPC, Mkuu wa Idara, DC, Uhamiaji, kaa kwenye kiti chako ueneee. Habari ya kutumia madaraka kuwakandamiza wanyonge, kupendelea wenye pesa imefika mwisho. Kwenye idara yako kama huwakudumii wananchi, cha mtema kuni utakiona.

⦁ Arusha tembeeni kifua mbele. Ya Kwamba Mtaheshimika kwa utu wenu, sio pesa, elimu wala connection. Wanaosema niketolewa uenezi, nimeletwa u RC, sasa CCM nilikuwa nasema wafanye wengine, huku nafanya mwenyewe. Ofisi yeyote ukienda wakikuhudumia vibaya njoo kwangu. Hospitali ukijibiwa vibaya, Polisi wakikunyima dhamana, njoo kwanguuuu... Silogeki! Hofu iliondoka na kitovu waliponikata...

⦁ Jambo la sita: Kamishna wa ardhi NJOO HAPA! Una miezi mitatu kumaliza migogoro ya ardhi. Mnongoza kwa rushwa! Na msijioendekeze kwangu kwa kunipa kiwanja, Arusha viwanja ninavyo. Ardhi ni kilio namba moja...

⦁ Afisa Mipango Miji NJOO HAPA! Mnazalisha squatter! Hakuna mipango miji, mmeshuhudua inajengwa bypass lakini hamkwenda mkapanga na kupima viwanja kuwe na barabara zinazopitika. Mnashinda kule Bulka na Sanawali kwa sababu kuna rushwa. Sasa una miezi mitatu tutakuita utoe ripoti umekuta migogoro mingapi, umetatua mingapi, umekuta watu wangapi hawana hati, umetoa hati ngapi. Na, umejipangaje kuhakikisha migogoro mingine isitokee... Migogoro ya ardhi inasababishwa na nyinyi wataalam wa ardhi! Mtendaji, Mtumishi, usipojipanga tunakupanga!

⦁ Uhamiaji: Mtu ana nyaraka zote, kwa nini passport ichukue siku 14? Na foleni ya Namanga foleni masaa matatu. Natka iwe mwisho dakika 60!

⦁ Mabango kila mahali, mara masaji, mara dawa za kienjeji, hapana. Tunataka screens. Watu wanatushangaa.

⦁ Sisi ni matajiri kuliko wanaokuja kutuhurumia! Maji Arusha yanatoka matope, na kuna suala la bili kubambikizwa. Zinakuja kufungwa mita za pre-Paid.

⦁ Ndugu zanguni, mambo ni mengi. Tutakaa mtanambia mnataka RC wa aina gani lakini kamwe sitawasaliti. Maombi yenu ndio yananiweka hapa. Wajane, vijana, wazee wananambia endelea. Sitawaangusha. Sitalumbana na mtu. Mwenye wazo la kutengeneza ajira, mwenye wazo la kujenga uchumi, kuboresha Arusha, mlango uko wazi.

⦁ KIla anaekuja Arusha apokelewe na kikombe cha kahawa. Ni mji unaotupatia pesa nyingi sana, hatuwezi kuuacha bure. Lets make Arusha Great Again.

⦁ Najua Yapo mambo ya Stendi. Ya soko. Ya boda. Ya dala dala. Ya Tatu Mzuka. Ya bajaji. Ya Wadudu. Nipeni muda.

⦁ Tarehe 12 tutampokea Rais katika tukio kubwa la kumuenzi Hayati Sokoine aliyefanya kazi ya heshima katika taifa hili. Ndio maana mimi ni mchanganyiko wa mtoto wa masai, wa jeshi, wa kisukuma... Sieleweki kwa sababu Mungu amejaa ndani yangu. Nimechukua combination zote nzuri ndo maana pa kunyooka tunanyooka kweli kweli.


⦁ Nimeongea na RPC tunaenda kuongeza nguvu ya ulinzi Arusha, maduka hayafungwi saa 11, saa 12 mbili. Zinakuja camera, taa za kutosha, patrol za baskeli za polisi, pikipiki, rescue team, mpaka helicopter za patrol. Kuhakikisha mnalindwa barabara.

⦁ Mungu wangu na awabariki sana

WATU EEEEEEEEEEEEEEHHHHHHHHHHHHH!


View: https://youtu.be/ijwCgxv5seg

SHANGWE NA VIGEREGE, NA VIGEREGERE, NA VIGEREGEE NA VIGEREGERE NA VIGEREGEREEEEEEEEEEE

Haya yote ni upuuuzi mtupu! Kwanza atoke huko hotelini anakoishi kwa gharama za maskini!
 
Ni wazi kuanzia Oktoba 2023 akiwa Katibu wa Itikadi na Uwenezi wa CCM na hatimaye kuwa RC Arusha kuanzia April 2024, tumeshuhudia kauli nyingi chafu kutoka kwa Makonda kwenda kwa wateule wako.

Haokutosha tu, Makonda aliweza hata kuudhalilosha mhimili wa Mahakama.

Yaani huyu Makonda anaweza kuwa na TAARIFA za ndani kuliko TISS wenye kazi yao?

Kama ambavyo akiwa Mwenezi wa CCM hakujua majukumu yake, huku nako kwenye u RC wa Arusha bado Makonda hajui kazi yake.

USHAURI KWA RAIS SAMIA:
Chonde chonde Rais Samia USIINGIE mtego huu wa Makonda. Huyu NI ZEROBRAIN atakuharibia uRais wako.

Haiba yako Rais Samia na ya Makonda haziendani. Wewe ni muungwana na mpenda haki na uhuru wa maoni. Huyu ananuka damu za watu aliowaua na anatamani na wewe umruhusu aanze kuteka na kuua.

Piga chini, muache na maisha yake maana hata Magufuli aliyemleta mwaka 2016 kama RC Dar alikuja akamchoka na akamtema mwaka 2020.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kama kawaida ya Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ni mtu wa kuteka hadhira, ni mtu wa kuteka mijadala, ni mtu wa kuondoka na point tatu na magoli ya kutosha,ni mtu anayeijuwa siasa,ni mtu msema kweli, jasiri,imara, hodari, madhubuti, shupavu na mwenye misimamo yake na ya aina yake.

popote alipo ni lazima pafahamike na kuvuma kama upepo wa baharini, ni Mwamba kwelikweli, ni field Marshall ambaye akianza kuzungumza unaona hata sisiminzi wanatulia kusubiri amalize kuzungumza ndio waendelee na shughuli zao.kiukweli huyu Mwamba ni jasiri sijapata kuona. Ni jasiri mpaka shetani mwenyewe anamuogopa.

Leo katika kutoa kwake neno amemmwagia sifa kemkemu Askofu mkuu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Pengo kwa kusema kuwa amesimama naye wakati akiwa na cheo na wakati akiwa hana cheo.

Akaendelea kusema kuwa anafurahi tena kumuona akikanyaga katika ardhi aliyopewa na Mheshimiwa Rais kuiongoza na ni bahati ya kimungu , na kwamba ni mwisho kuzaliwa kwa mapooza na kwamba ardhi haitazaa tena mapooza.

Mnafikiri alimaanisha nini Mwamba kwa kauli hii ndugu zangu. Mnauonaje ujasiri wa Mwamba awapo jukwaani na Maiki Mdomoni pake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
 
I have never heard such a stupid utterance from such a stupid politician. Yeye anajiona yupo ikulu. Kuteuliwa tu kuwa mkuu wa mkoa anakuwa na mbwembwe hizi, siku akiteuli2a kuwa Naibu Waziri mbona atajinyea!
It's very stupid indeed
 
Back
Top Bottom