Wakati tetesi za Uteuzi wa Paul Makonda kwenye nafasi ya Ukatibu Mwenezi wa CCM zilipoibuka na uzi wake kuwekwa humu JF, Nakumbuka Mimi nilitoa comment kwamba "Naomba Mungu habari hii iwe kweli ili kuharakisha Anguko." Nafikiri wahusika walikuwa hawajanielewa, matokeo yake kweli Makonda aliteuliwa, na hatimaye ndani ya kipindi kifupi kabisa akasababisha mtikisiko mkubwa sana kwenye Chama Chao hadi kupelekea Katibu mkuu wao kujiudhuru.
Wananchi wenzangu tukubali ukweli mchungu kwamba Paul Makonda ni mtu asiyefaa kuongoza binadamu, hana hata sifa moja ya kuongoza watu.
Isitoshe, kwa Sasa hapa nchini Tanzania amekuwa ndiye Mkuu wa Mkoa mbumbumbu zaidi kuliko wenzake wote, Rais anapaswa kuondokana naye kwa kumuweka kando.
Kama Rais anaona kwamba haitawezekana kabisa kumuweka kando kutoka ktk Serikali yake, basi amteue Paul Makonda kuwa Balozi na amtume kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa ambayo Sera zake ziko against na nchi ya Marekani pamoja na washirika wake, kama vile nchi ya Korea ya Kaskazini, Myanmar (Burma), Belarus, n.k.