Ndugu zangu Watanzania,
Katika sherehe za leo zinazoendelea mkoani Arusha na kwa nanmna zilivyofaana na kupendeza na kuvutia na kubwa zaidi kwa namna watu walivyofurika na kumiminika ni haijawahi kutokea katika Historia ya sherehe za Mei Mosi. Hii inabaki katika kumbukumbu ya Mei Mosi iliyohudhuriwa na watu wengi sana kuwahi kutokea katika Taifa letu.
Makonda ni Mwamba na bingwa wa mikakati na Jabali la mipango na hamasa. Jamaa anakubalika na kiongozi mwenye nyota kali sana ya kupendwa na watu pamoja na kuheshimika.leo Arusha imeitikia,kanda ya kaskazini imeamka na kwenda kuungana na Mwamba Makonda katika mapokezi mazito ya ugeni wa kitaifa na watu kutoka maeneo mbalimbali ya Taifa letu.
Kwa hakika ukitaka shuguli yako ipendeze katika jambo lolote lile ,basi wewe mkabidhi kazi hiyo Mwamba Makonda halafu muachie akufanyie kazi.kwa hakika leo Mwamba ameonyesha yeye ni mtu na nusu,ni kipenzi cha wana Arusha na watanzania wote kwa ujumla ,ni kipenzi cha vijana na watu wa makundi mbalimbali na ni kiongozi wa kutumainiwa na kutegemewa kwa Taifa letu.
Ipo siku Mwamba atashika nafasi za juu kabisa za uongozi ndani ya serikali yetu.ipo siku watu wataandamana na kumbeba Mwamba Makonda Mabegani mwao kumshukuru ,kumpongeza na kumtia moyo kwa uchapa kazi wake. Ukimchukia Mwamba Makonda unajiumiza tu maana kwa kadri unavyomchukia ndivyo anavyodhidi kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Usishindane na aliyepewa kibali na Mungu.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.