Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Ndugu zangu Watanzania,

Katika sherehe za leo zinazoendelea mkoani Arusha na kwa nanmna zilivyofaana na kupendeza na kuvutia na kubwa zaidi kwa namna watu walivyofurika na kumiminika ni haijawahi kutokea katika Historia ya sherehe za Mei Mosi. Hii inabaki katika kumbukumbu ya Mei Mosi iliyohudhuriwa na watu wengi sana kuwahi kutokea katika Taifa letu.

Makonda ni Mwamba na bingwa wa mikakati na Jabali la mipango na hamasa. Jamaa anakubalika na kiongozi mwenye nyota kali sana ya kupendwa na watu pamoja na kuheshimika.leo Arusha imeitikia,kanda ya kaskazini imeamka na kwenda kuungana na Mwamba Makonda katika mapokezi mazito ya ugeni wa kitaifa na watu kutoka maeneo mbalimbali ya Taifa letu.

Kwa hakika ukitaka shuguli yako ipendeze katika jambo lolote lile ,basi wewe mkabidhi kazi hiyo Mwamba Makonda halafu muachie akufanyie kazi.kwa hakika leo Mwamba ameonyesha yeye ni mtu na nusu,ni kipenzi cha wana Arusha na watanzania wote kwa ujumla ,ni kipenzi cha vijana na watu wa makundi mbalimbali na ni kiongozi wa kutumainiwa na kutegemewa kwa Taifa letu.

Ipo siku Mwamba atashika nafasi za juu kabisa za uongozi ndani ya serikali yetu.ipo siku watu wataandamana na kumbeba Mwamba Makonda Mabegani mwao kumshukuru ,kumpongeza na kumtia moyo kwa uchapa kazi wake. Ukimchukia Mwamba Makonda unajiumiza tu maana kwa kadri unavyomchukia ndivyo anavyodhidi kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Usishindane na aliyepewa kibali na Mungu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Mimi nimempongeza sana kwa Kauli moja tu ya Makonda ,lile la KUFUTA ile kauli ya Katibu mkuu wa TUcTA kuhusu wazee wa mila kusimamisha mvua.Makonda kasema Kwamba kila kitu kiko chini ya Mungu na kutambua maombi ya viongozi wa Dini. Hiv ni kweli Waziri mkuu alisahau nafasi ya viongozi wa dini mpaka kuomba msaada kwa viongozi wa mila?
 
Kuna muda muwe mnatumia akili. Akili za kukusaidia kujua Mei Mosi inavyokuwa organised. Itakusaidia kujua ile sio ya Bashite bali ni maelekezo ya serikali kwa watumishi wake. Huko kuna roll-call lazima mtu aende. Huko watu wamesaini posho kuhudhuria. Nani hataki posho?
Akili mnatumia kufanyia nini?
Boss, nipo Arusha, watu esp vijana vijana wapo wa kutosha. Jana usiku saa sita wakati wa kupiga fataki tu watu walikuwepo, leo hizo bajaji na pikipiki ni za kutosha. Huo ndo ukweli hata kama haupendwi.
 
Kuna muda muwe mnatumia akili. Akili za kukusaidia kujua Mei Mosi inavyokuwa organised. Itakusaidia kujua ile sio ya Bashite bali ni maelekezo ya serikali kwa watumishi wake. Huko kuna roll-call lazima mtu aende. Huko watu wamesaini posho kuhudhuria. Nani hataki posho?
Akili mnatumia kufanyia nini?
uwanja ni mdogo ndiyo maana anaonekana kuuujaza na watu.
 
Zaburi 118:22-24
Jiwe walilolikataa waashi,
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Jambo hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu mno machoni petu.

Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana,
Tuishangilie na kuifurahia.
Ongeza na mwingine mkuu
 
Sijamuona Katibu Mkuu CDE Dkt Nchimbi na CDE Makalla kwenye Mei Mosi hapa Arusha. Ila nadhani kimoyo moyo walijisema lazima watu wasusie kwenda Arusha kisa Makonda.
Suala siyo kudodeha sikukuu, hofu ni nani ameinjinia menu ya leo?
 
kwahiyo hiyo ni nini? na mbona iko kwenye stationary yako pekeyako ndugu mfanyakazi. na inaonekana umepata tabu sana kuipiga picha na kuscan :pedroP:
Wafanyaz wanataka chaooo
Pole yaoo sana

Ova
 
Sikukuu ya wafanyakazi badala ukasikie mipango, mambo ya pensheni, mishahara na ajira imegeuka ya watu wamejaa au lah pamoja na wadudu kupendezesha shughuli, bongo ina safari sana 😀
 
GTs,
Sijamuona Katibu Mkuu CDE Dkt Nchimbi na CDE Makalla kwenye Mei Mosi hapa Arusha. Ila nadhani kimoyo moyo walijisema lazima watu wasusie kwenda Arusha kisa Makonda. Ila kwa hiyo nyomi nadhani wajiulize maswali mengi sana kwanini? Mungu ambariki sana Makonda.
Tuseme na kizimkazi alimsusia basi
 
Mshahara haujaomngezwa lakinii mashangingi ya ma DC yana nunuliwa
Mshahara haujaongezwa lakini misafara ya viongozi haipungui
Ulitaka DC atembee kwa miguu kwenda ofisini kwake.?

Ulitaka mheshimiwa Rais asindikizwe na gari moja..?

Muda mwingine jitahidi ufiche ujinga wako uepuke aibu ndogo ndogo
 
Back
Top Bottom