Wadau mtaniwia radhi kwa hili,
Nimeshuhudia mara nyingi kwa wanasiasa kuwa leo ana msimamo huu kesho ule.
Na leo limejirudia kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha mheshimiwa Paul makonda.
Wakati ule alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kumchana makavu pierre liquid(pale mlimani city kwenye kongamano la mtoto wa kike) akisema:
"HATUWEZI KUWA NA TAIFA AMBALO LINA-PROMOTE WATU HOVYO , WANAKUWA HADI MA-BRAND AMBASSODOR ... HALAFU UNATEGEMEA WATOTO WETU WATAFIKIA KWENYE MAFANIKIO ??
Mi nilielewa alikuwa akiwakosoa na kuwashambulia watu waliokuwa wanam-brand na kumprote kwa sababu alikuwa mlevi na comedian.
View attachment 2978301
Picha linageuka,
Leo ni yeye huyuhuyu anawapromote na kuwabrand wadudu/machalii wa Arusha akisema:
"HAWA WADUDU NI JINA, NI BRAND , MKOA HUU NINA KILA AINA YA VIJANA WENYE VIPAJI MBALIMBALI ........"
View attachment 2978302
Sasa hawa wadudu wanatofauti gani na pierre wa wakati ule ?
Amesahau ? Au ndo siasa ilivyo ?