Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Hakika hiki ni kichekesho! Katika siku muhimu kama Mei Mosi kwa wafanyakazi.wanaowazia hatima ya kazi zao, mishahara na mafao yao ya kustaafu, pension zao, kupandishwa vyeo na kila linalowasibu eti ndio haya tena ya Makonda?
Mbele ya makamu wa Rais anayemwakilisha Rais mnasema bila aibu kuwa Makonda ni mbunifu kisa WADUDU?
Yaani bila aibu mnaleta vijana wakuwapeleka Rehab mbele ya Rais, mabalozi na wakuu wengine wakiwapo WAFANYAKAZI WATUKUFU?
Mbona toka aseme anawajua wanaolipa wamtukanao Rais sasa kujipendekeza kwake kumekuwa kukubwa kama kuogopa wasitajwe?
WADUDU NDIO UBUNIFU WA MAKONDA?!
View: https://youtu.be/aFZXjQc901U?si=08otvhLulbWRB6VL
Wadudu mbona wapo kitambo sana chalii yangu!