Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwa binadamu yeyote anayetamani kuona Tanzania inapiga hatua ya maendeleo katika kila nyanja, basi bila shaka atakuwa anafurahishwa na jitihada za Makonda katika kutatua kero za wananchi.

Makonda ni mbunifu sana. Popote alipo lazima watu wamsikilize. Na hii ni kutokana na yeye mwenyewe kupenda kusikiliza.

Uenda asifanikiwe kwenye kila analolianzisha. Ila nia yake daima huwa ni njema. Dunia ni ngumu sana. Kuna watu wana nguvu na wanafanya kila wawezalo kukwamisha maendeleo kwa maslahi yao binafsi.

Makonda ni mpambanaji, mbunifu, msikivu, mpenda haki.
Sio mbunifu nikielelezo cha kuonesha mifumo imefeli au dhaifu kabisa, na niusanii tu ukifuatilia baada ya hapo kero zinazotatuliwa ni less than 1% kwakua mfumo ni dhaifu watu hawako tayari kufanya kazi (demotivated) hivyo bado unaona umuhimu wakua na katiba mpya ili tubadili muundo wetu wa uongozi wananchi wapate huduma katika maeneo husika sio kwa kukusanywa nakudhalilishwa huwezi taka tatua shida za watu nakuchukua vi clip na waandishi wa habari kuvitumia kujijenga! Nonsense kabisa kila mtu akiwa anatekeleza majukumu yake ajirekodi ili aonekane anafanya kazi hiyo haitakua kazi,mtenda haki anafanya kwa matendo sio maneno hivyo huyo jamaa yenu ni muigizaji ndio mana usingae anavyo chukua video kama movie
 
Kiuhalisia ni kwamba hakuna kero yoyote inayotatuliwa.

Huwezi kutatua kero za wananchi kwa kuwaita mmoja mmoja jukwaani kuwauliza kero zao kwenye nchi kama hii yenye watu milioni 60.

Kama kweli Makonda ana nia ya kutatua kero za wananchi, alitakiwa akae na viongozi wenzake wa ngazi za juu waweke MIFUMO THABITI itakayohakikisha kero hizo zinatatuliwa at regional/national level.

Kinyume na hapo ni cheap politics tu.
 
Kwa kuongezea, Makonda hata kama anajua kabisa njia anayoitumia sio sahihi hawezi kukubali kutumia njia sahihi.

Makonda anapenda sana kuita watu mmoja mmoja, tena mbele ya makamera ili SIFA ZOTE ZIRUDI KWAKE aonekane yeye ndio anapambana kusaidia/kutatua kero za wananchi!

Ukimuambia aweke mifumo thabiti hatakubali kwasababu yeye hataonekana tena na sifa zitagawanywa kwa viongozi wote.
 
Kama week hii bando zimeisha arusha.Huwa inavutia na kupata somo zuri jins malalamiko ya wananchi na jinsi yanavotatuliwa.kama jana kisa cha mwalimu beartice aliyepata ruhusa ya masomo lakin maafisa aelimu wake walivomkwamisha kwa roho mbaya,haitosh zaidi wakamnyima mpaka na mshahara,kwa kipind alichokuwa anasoma masters yake,mbaya zaid mshahar kila ukija wanau punch unarudi hazina hapewi wanasema mtoro, unajiuliza hiv hii ni roho mbaya kias gani? Ila yule mama jasiri sana na ana kila supporting doc zake mwisho wa siku kawabanisha mpaka kashinda CMA ,wamlipe malimbikizo yake kwa muda wote.ni kwanin maofisn wakiona unaenda kuongeza elimu huwa hawapend aidha utafanyiwa figisu utatolewa kwenye mpango,ukitaka kujilipia napo shida ruhusa,
So kuna mafunzo meng huwa yanapatikana
 
KAZI ANAZOFANYA MH PAUL MAKONDA NDIO KAZI ZA KIONGOZI

Na Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA

Mimi ni shabiki mkuu wa aina ya siasa za watu kama Paul Makonda. nimekuwa nikimshabikia bila woga akiwa kwenye madaraka na alipokuwa nje ya uwanja wa siasa za kitaifa,

Nasikitika sana kusema watu wengi hawajui kuchagua zuri na baya, nimewahi kusikia kelele za wajinga wanaomchukia Mh Paul Makonda mimi huwa nacheka kwa kicheko cha Magufuli RIP. Paul Makonda ni kiongozi kinara katika muongo mzima tangu 2010's katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, labla tunaweza kumweka kundi moja na Malema wa South Africa. katika siasa za kuwsinua wananchi, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Paul Makonda ni Jembe tena sio la mkono, ni jembe la kitu zaidi ya trekta.

Tumekuwa na wimbi la vijana wamejikita kwenye siasa za kusambaza sambaza posters na habari na kwa bahati mbaya muda mwingine ndio wanaopewa nafasi kwa sababu tu wana maneno ya asali asali kwa viongozi, Paul Makonda sijawahi kumwona hivyo,

Paul Makonda ni kiongozi anayeingia field na kuwagusa kabisa wale wenye shida na haogopi kitu, mimi nikimsikiliza makonda najisikia raha sana kujua kumbe aina ya siasa za hivi inawezekana, yaani ukipewa kazi ni kufanya kazi sio kwenda kuwabembeleza watu na kuwalamba lamba miguu ili upate mali za wizi.

Nina mengi ya kusema kuhusu kiongozi huyu Jasiri, Mbunifu, Asiye na Chuki wala upendeleo, Muwazi, Asiyependa Majungu na Unafiki, PAUL MAKONDA.

SABAYA ARUDI KWENYE HATAMU KAZI ZIFANYIKE.

Ndimi Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CCM LIA LIA
MTIA NIA MCHACHACHALI JIMBO LA KAWE
Ukweli mchungu, thanks
 
Mimi ni shabiki mkuu wa aina ya siasa za watu kama Paul Makonda. nimekuwa nikimshabikia bila woga akiwa kwenye madaraka na alipokuwa nje ya uwanja wa siasa za kitaifa,
kwani kumshabikia mtu kunahitaji uoga au ujasiri?

kumshabikia mtu ni maamuzi yako binafsi kulingana na kile ukipendacho kutoka kwake.

mfano mimi namchukia Makonda, na ni maamuzi yangu.
 
Chadema arusha wamebanwa hawasikiki. Mwananchama mwenzangu bora uje na mbinu mpya hii ipo waz sana.ni kweli arusha hatufurukuti mana tumepoteana,
 
Makonda hajawahi kutatua kero ya mtu yeyote zaidi ya kuwadhalilisha wahusika. Aliwahi kuwaita akinamama Dar es Salaam waliotelekezewa watoto, hakuna alichokifanya. Akajifanya kuwasaidia walimu wapate vitambulisho ili waweze kupanda bure daladala, hiyo nayo ikashindikana kwa kuonekana ni kama walimu wanadhalilika zaidi kwenye daladala kuliko kusaidika. Ilipokuja ishu ya dawa za kulevya, akaja na orodha ndefu ya majina ya watu aliokuwa na visasi nao. Zaidi ya hapo kilifuata nini, hakuna mtu hata mmoja aliyefungwa mahakamani kwa kosa hilo la dawa za kulevya. Hata kwenye ziara zake za uenezi amefanya kitu gani? Anadhalilisha tu watu kupitia matatizo yao, huku yeye akitafuta kiki ya kisiasa
Wivu ukizidi sana hugeuka kuwa nini? Naomba kila atakaye toa jibu hapa amtag Kichuchunge
 
Tangu kuteuliwa kwa RC Makonda Arusha, Lema ni kama amepotea, watu wapo bize na makonda in short kama hali itaendelea hivi hivi A town Lema ana kazi sana.

Utendaji kazi wa RC unawakosha watu na kuona jinsi chama chao cha mapinduzi ni sikivu nenda uone jinsi watu wanavyosaidiwa kero zao.

Huu muziki ukiendelea hivi hivi kelele za kina Lissu zitakuwa maeneo mengine ila sio Arusha, Istand to be corrected.
 
Makonda hajawahi kutatua kero ya mtu yeyote zaidi ya kuwadhalilisha wahusika. Aliwahi kuwaita akinamama Dar es Salaam waliotelekezewa watoto, hakuna alichokifanya. Akajifanya kuwasaidia walimu wapate vitambulisho ili waweze kupanda bure daladala, hiyo nayo ikashindikana kwa kuonekana ni kama walimu wanadhalilika zaidi kwenye daladala kuliko kusaidika. Ilipokuja ishu ya dawa za kulevya, akaja na orodha ndefu ya majina ya watu aliokuwa na visasi nao. Zaidi ya hapo kilifuata nini, hakuna mtu hata mmoja aliyefungwa mahakamani kwa kosa hilo la dawa za kulevya. Hata kwenye ziara zake za uenezi amefanya kitu gani? Anadhalilisha tu watu kupitia matatizo yao, huku yeye akitafuta kiki ya kisiasa
.. Hajawahi kutatua kero...!

Ona huyu naye!

Yawezekana wewe ni punda ama zungu la unga kabisa isee!

Unaweka chuki zako za wazi hadharani ili angalao upoze machungu kidogo au siyo?

Hata mimi ningelikuwa tapeli wa mali za watu na majumba, muuza madawa ya kulevya na fisadi ningelimchukia sana Makonda kwa nmna utendaji wake unanyofukunyua, kubaini na kudhalilisha.
 
Tatizo lake huwa hafikirii mambo!! Wewe kama RC, jambo liko mahakamani, na lingine limeshatolewa hukumu, unawezaje kumsaidia mtu?!!!
Wewe acha uongo na maneno mengi! Makonda kwenye kliniki yake ya kutatua kero za wananchi amewatumia wanasheria wa Tanganyika Law Society! Mnapenda kumwekea maneno mengi na ujinga ujinga mwingi sana!
 
.. Hajawahi kutatua kero...!

Ona huyu naye!

Yawezekana wewe ni punda ama zungu la unga kabisa isee!

Unaweka chuki zako za wazi hadharani ili angalao upoze machungu kidogo au siyo?

Hata mimi ningelikuwa tapeli wa mali za watu na majumba, muuza madawa ya kulevya na fisadi ningelimchukia sana Makonda kwa nmna utendaji wake unanyofukunyua, kubaini na kudhalilisha.
Funga mdomo, hunijui. Nipe ushahidi wa alichotatua kikazaa matunda. Hilo la madawa ya kulevya angalau tungeonyeshwa mfano wa wawili au watatu waliofungwa kwa ajili hiyo lakini ziliishia drama tu za kutafuta kiki. Acheni uchawa wa kumfagilia Makonda.
 
Back
Top Bottom