Paul Makonda unatakiwa ujifunze na ujitafakari sana

Paul Makonda unatakiwa ujifunze na ujitafakari sana

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Kitu pekee ambacho ninajifunza katika hii dunia ni kwamba kila nifanyalo ni lazima lipite, itakua "ilishakuwa". Kiufupi ili uendelee kufurahia maisha katika hii dunia tendwa wema wenzako, tenda haki, jiepushe na arrogance (kibri na majivuno).

Paul Makonda aliyekabidhiwa mkoa mkubwa wenye population kubwa kama Dar es Salaam leo hii yupo benchi anasugua miguu kweli? Huyu mtu naona si bure kuna mengi ambayo si mazuri alifanya nyuma ya pazia ambayo anayajua yeye na Mungu wake pamoja wanaomjua kiundani. Kama tunaambiwa kua Sabaya ni cha mtoto kwa huyu jamaa, hivi kwake ilikuaje?

Yaani unafikia mapaka hatua ya kuwekewa kikwazo na taifa la Marekani wewe si wa kawaida, unaambiwa inanyima watu haki yao ya kuishi maana yake nini? Yawezekana kabisa hata mamlaka zinaona kabisa haifai kabisa huyu mtu kumpa hata ukuu wa Wilaya.

Yawezekana kabisa mamlaka zimemkataa huyu bwana kwa matendo na tabia zake, kumpa mamlaka tena ni kumrudisha kule kule alikokuwa akifanya. Mtu unafikia hadi kuomba kibali hadharani kwa mkuu wa nchi kuwashughulikia wanaomkosoa?

Makonda hakuona shida kuwakejeli mawaziri na hata kuwachongea kwa Rais. Huyu alikua RC tu, angekua hata Waziri ingekuwaje?

Tujifunze kua kibri,dharau na majivuno kwa binadamu wenzako si kitu.
 
Kweli kila zama na kitabu chake, jamaa kweli alikuwa "Mkuu" wa mkoa ilikuwa kama hutakiwi kuwa ndani ya mkoa wake hata kama hakujui ila by association hutakiwi kuwepo aisee utatafuta njia mwenyewe uondoke🏃🏃🏃
 
Ninacho jua sababu kuu ya Marekani kumpiga ban ni baada ya yeye kuwashikia njuga mashoga kama wewe.

Sio ninyi mliokuwa mnapiga kelele kuwa ana vyrrti deli atolewe. Amesha tolewa tena mnashangaa eti kwanini hateuliwi.

Hii nchi ni ngumu Sana
 
Sielewi mantiki ya mada yako.

Umekuja kumpgia kampeni huyo mtu wako kupitia hapa hapa JF ili wakubwa wasimsahau au unatakaje?

Huyo Bashite naye ni mtu mwenye hadhi ya kuanzishiwa mada hapa JF ili watu wapoteze muda kumjadili; halafu iweje?

Mbona JF limekuwa kama jalala siku hizi!
 
Sielewi mantiki ya mada yako.

Umekuja kumpgia kampeni huyo mtu wako kupitia hapa hapa JF ili wakubwa wasimsahau au unatakaje?

Huyo Bashite naye ni mtu mwenye hadhi ya kuanzishiwa mada hapa JF ili watu wapoteze muda kumjadili; halafu iweje?

Mbona JF limekuwa kama jalala siku hizi!
😅😅😅promo
 
Andhani yaliisha? Hata ajikalishe kimya watu wanapima upepo. Jinai haifi hata baada ya miaka 50 awe Uswisi awe Urusi atakuwa Deported tu.

Alishalikoroga hata kaa apate amani maishani
Lazima alinywe, ALISHALIKOROGA
 
Unataka ajifunze nini sasa we nae , umemuona ana shida gani ? Kama ni ofsi aliamua kuiacha mkae nayo , ametulia zake Kwa aman, mnaanza chokochoko ....Hana shida na teuzi angekuwa na shida ungemuons anaongea huku na kule ,
 
  • Thanks
Reactions: ZNM
Back
Top Bottom