Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Wangeeleweka kama wasingekuwa wakirudi kugombea,kweli ni mtetezi wa wanyonge, wataelewa wakiwa wamechelewa.
 
Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

P.
 
bora wasipate ila wawe na amani
 
Kukatwa hela siyo tatizo kama mmekubaliana hizo fedha ni kwa ajili ya kujenga na kukiimarisha chama. Sasa kama mpaka chaguzi ndogo mbunge anagharamia mwenyewe hizo laki 5 zinaenda wapi? Ofisi za kanda hazipelekewi hela kwa ajili ya kujiendesha. Mpaka leo hatuna Makao Makuu ya chama inayoeleweka. Hizo fedha zinaenda wapi? Msitetee ujinga hapa kuna tatizo kubwa.
 
Kazungumzia kuwa hili suala la malalamiko yake aliyoyasema kama sababu za kujiuzulu aliyafikisha sehemu za juu kwenye chama chake na kutosikilizwa? Au alijibiwa vipi?

Ingependeza zaidi kama angetueleza hatua alizowahi kuzichukua dhidi ya malalamiko yake na matokeo ya hatua hizo, hapo ndio angeonekana mtu mwenye maamuzi mazuri kuliko na kusema kitu ambacho hajawahi kukifanya
 
C walipitisha maamuzi kwa pamoja km wajumbe anacholalamika ni nn?huyo mama hana shukrani hata chembe ameona laki 5 ina thaman kubwa kuliko ubunge wa zawadi aliopewa 2010.
 
Wanazi wa chadema ni vipofu. Hawaoni matatizo ya ndani na hawataki hata kuyajua.
 
Mkuu kwa mawazo yangu naona kama anasema wabunge wa hicho chama wanakatwa laki tano 500,000 kila mwezi na hamjui matumizi yake kwa nini msihoji mpambanaji wa kweli hakati tamaa kukimbia sio suluhisho
Waliohoji walishapewa makaripio makali sana na kutishiwa kutoteuliwa kugombea ubunge 2020. Hii ni Karma kwa M/kiti Chacha wangwe alikufa na kihoro, Dk. Slaa aliondoka na kinyongo.
 
Acha Ujinga
nenda kwenye mada husika
Laki tano kila mwezi za mbunge za nini na zinaenda wapi
Milion 300 kila mwezi zinaenda wapi
Hamna hata Banda la kuku!!
Mnashindwa kujiongoza Nchi hii mtaiongoza!!
 
Kwa hiyo CCM wamemrudishia fedha zote alizotoa mfukoni mwake wakati wa uchaguzi ndiomaana kawasaliti wapiga kura wake na kuhamia CCM?.
 
Sawa, uamuzi wake ni mzuri lakini? Hapakuwa na jinsi yeyote ambayo wangeweza kaa na kusolve.? Nachokiona ni Njaa, na hofu ya maisha, inayotia kiwewe cha kurudi bungeni tena.
Sasa hili anatakiwa afanye Mbunge au Chama?
 
C walipitisha maamuzi kwa pamoja km wajumbe anacholalamika ni nn?huyo mama hana shukrani hata chembe ameona laki 5 ina thaman kubwa kuliko ubunge wa zawadi aliopewa 2010.
Matumizi yanakwenda wapi
 
Laki tano mbona ndogo mno,?undefinedHalafu milioni 300 kwa chama kilichoenea nchi nzima,sio pesa nyingi kivile,unless labda watumishi wawe wanajitolea,hawalipwi,undefinedmilioni 300 ni hela ya mafuta ya magari tu hiyo,
 
RUDIA KUSOMA TENA NILICHOANDIKA, MTUHUMIWA NI MBOWE NDIYE ANATAKIWA KUSHTAKIWA. KAMA MAAMUZI YAMEFANYWA NA CHAMA INA MAANA NA HAO WANAOLALAMIKA NI SEHEMU YA WALIOTOA HAYO MAAMUZI
Ishu hapa siyo kukatwa hela. Mbunge anahoji hizo hela wanazokatwa zinakwenda wapi?
 
Mbona wabunge wa vit maalumu hawahami? Mbona wabungewa zanzinar hawahami?

We are not fools
 
Hizi habari hunifanya niache kuwasha internet kwenye PC na hata kwenye simu. ujinga kama huu unafanywa Tanzania tu
 
Hakuna lolole, Wanasiasa wengi hawa ni waongo na Wanafiki tu..msitake kuwaamini sana.

Kungekuwa bado na maslahi huko hayo yote yangevumilika kama alivyovumilia muda wote,na huenda wanakubaliana nayo kabla hata hawajajiingiza humo. Na tena kama ungejitokeza wewe wa nje na kuhoji angekujibu 'yetu hayakuhusu fuata maisha yako'

Leo kwa kuwa tu amepata uchaguzi 'option' basi yatasemwa yoooote ili ahalalishe anachotaka kufanya.

Ina maana kusingekuwa na CCM kuna siku angejitoa na kurudi uraiani kwa ajili ya hizo shutuma?
 
Hivi wamebaki wabunge wangapi sasa? Kamati kuu ya Chama kuendelea kukaa kimya (as if nothing is happening....) bila kukutana kujadiri hii situation na kuassume blindly wanaohama wananunuliwa ni uzuzu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…