Nanukuu“Ni ukweli usiopingika kwamba mzigo wa kuendesha chama umeachwa mabegani mwa wabunge, chaguzi ndogo zilizopita hakuna msaada wowote kutoka chama makao makuu, fikiria kutoka mwaka 2015 mchango wa kuendesha chama kutoka makao makuu haujazidi shilingi za kitanzania laki tano(500,000). Chaguzi zote nigharamie mimi, ilihali chama kinapata ruzuku ya Zaidi ya milioni 300 kila mwezi na bado wanatukata zaidi ya 500,000 kila mwisho wa mwezi, hii sio haki” Mwisho wa kunukuu.
Mwenyekiti inabidi ajitafakari siyo kuja na visingizio vya kwamba eti wananunuliwa. Hata ningekuwa mimi kwa upuuzi huu ningehama chama haiwezakani ruzuku yote milioni 300 kila mwezi utafune halafu unikate tena laki tano kila mwezi hakika huu ni ulafi uliopitiliza.