Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Huyu mama ni waajabu aliwahi kuulizwa kuhusu yeye kuhama kwenye mkutano wake ndani ya viwanja vya kwaraa babati mjin ila ajabu alikana na kusema yeye hanunuliki ila ajabu yametokea
Huu ni uwendawazimu
Unaelewa kiswahili vizuri? Alisema 'hanunuliki' na hajanunulika isipokuwa dhamira imemuongoza kuondoka CHADEMA kwa utashi wake yeye mwenyewe bila kushawishiwa na pesa au chochote.
 
Unafiki nnaouona mimi kwa hawa wabunge wanaohama kabla hata hajapewa nafasi za kugombea wanajua kabisa kuhusu hayo makato
 
Mbunge huwa hajiuzulu na kura zake, kura ni mali ya chama, na ruzuku inahesabiwa kwa idadi ya kura siyo idadi ya wabunge.
hatakama uchaguzi ukirudiwa?
so kura za mara ya pili hazizingatiwi? basi katiba ya hovyo kabisa
 
Huo si ushuru ni kodi ushuru unalipa mara moja tu basi Chadema wamegeuka TRA kukata kodi mapato ya wabunge wa Chadema .Hayo makato hayako Kisheria Na wala hayako kwenye katiba ya Chadema kuwa Kila mbunge atakatwa laki tano Kila mwezi. Wabunge Chadema kataeni.Utawala wa Sheria uzingatiwe.Hayo makato hayako Kisheria
Aisee ni kweli mkuu. Af kibaya zaidi pamoja na yote hayo wanataka kum-mtweza. 'kumla mzigo' kodi nyingine hiyo! Hapana kwakweli bora kastuka.
 
Unaelewa kiswahili vizuri? Alisema 'hanunuliki' na hajanunulika isipokuwa dhamira imemuongoza kuondoka CHADEMA kwa utashi wake yeye mwenyewe bila kushawishiwa na pesa au chochote.
Kwani nani kasema amenunuliwa?
 
Nanukuu“Ni ukweli usiopingika kwamba mzigo wa kuendesha chama umeachwa mabegani mwa wabunge, chaguzi ndogo zilizopita hakuna msaada wowote kutoka chama makao makuu, fikiria kutoka mwaka 2015 mchango wa kuendesha chama kutoka makao makuu haujazidi shilingi za kitanzania laki tano(500,000). Chaguzi zote nigharamie mimi, ilihali chama kinapata ruzuku ya Zaidi ya milioni 300 kila mwezi na bado wanatukata zaidi ya 500,000 kila mwisho wa mwezi, hii sio haki” Mwisho wa kunukuu.
Mwenyekiti inabidi ajitafakari siyo kuja na visingizio vya kwamba eti wananunuliwa. Hata ningekuwa mimi kwa upuuzi huu ningehama chama haiwezakani ruzuku yote milioni 300 kila mwezi utafune halafu unikate tena laki tano kila mwezi hakika huu ni ulafi uliopitiliza.
Nadhani hii ni sababu kuu na ndiyo inayowafanya wengi kukimbia.Maana ubunge ni kazi kama kazi nyingine Sasa kama kazi hiyo ina makato mengi wakati kuna sehemu makato hayapo lazima wabunge watakimbia.Huenda Ruzuku inatunzwa Kwa ajili ya uchaguzi 2020 lakini pia kuwakamua sana wabunge kunawarudisha nyuma
 
CHADEMA wanaweza kuwa wanafanya makosa makubwa kama watakuwa wanachukulia kuhama kwa wabunge watakuchukulia kama kupoteza wananchama wao jimboni.

In fact, mara wahamapo wabunge hawa juhudi jimboni zinatakiwa ziongezwe mara dufu hata kama hawatashiriki kwenye chaguzi ndogo zitakazofuata.

Kuimarisha chama ndani ya majimbo hayo yaliyoachwa ni muhimu sana. Hawa wabunge walipata ubunge kwa vile wananchi wa maeneo hayo waliikubali CHADEMA. Kuondoka kwa wabunge hao haimaanishi kutokubaliwa kwa CHADEMA.
Naamini MTU huchaguliwa kwa Sera zake sio kwa kukipenda chama!
 
Kwa hiyo paroko anayehubiri kuwa uchawi, wizi na fitina ni dhambi mbaya uongozi wa jimbo ukimsahau na kumuachia parokia aliendeshe kwa fedha zake anaamua kuacha uparoko na kujiunga na kundi LA wachawi aliokuwa anawapinga kila siku?
Hayo maelezo ya kijinga mkawape mama wa mama zenu wazee kule kijijini labda ndio watawaelewa
 
Sioni, tatizo kama walikubaliana ikatwe hiyo laki 5. Nafikiri, kulikuwa na kikao rasmi, sasa kama palepale hakuwa tayari, halafu akakubali, kisha, anakuja kuona haikuwa vyema bila shaka alikuwa mnafiki tu. Aende ambako hawakati pesa. Aende ambako mambo yamekuwa shwari, kiasi kwamba wakulima na wafanyakazi hawalalamiki. Aende tu ambako, wafanyabiashara wana amani pia. Aende tu, ambapo watu hawapigwi hela. Lakini asisahau kuwa sababu alizotoa ni kazitoakwakuwa ni lazima uwe na sababu, unapoamua kuighiribu jamii.
 
Nanukuu“Ni ukweli usiopingika kwamba mzigo wa kuendesha chama umeachwa mabegani mwa wabunge, chaguzi ndogo zilizopita hakuna msaada wowote kutoka chama makao makuu, fikiria kutoka mwaka 2015 mchango wa kuendesha chama kutoka makao makuu haujazidi shilingi za kitanzania laki tano(500,000). Chaguzi zote nigharamie mimi, ilihali chama kinapata ruzuku ya Zaidi ya milioni 300 kila mwezi na bado wanatukata zaidi ya 500,000 kila mwisho wa mwezi, hii sio haki” Mwisho wa kunukuu.
Mwenyekiti inabidi ajitafakari siyo kuja na visingizio vya kwamba eti wananunuliwa. Hata ningekuwa mimi kwa upuuzi huu ningehama chama haiwezakani ruzuku yote milioni 300 kila mwezi utafune halafu unikate tena laki tano kila mwezi hakika huu ni ulafi uliopitiliza.
Ndio maana wengine waliamua kuchukua mikopo ya ml 600 wakose cha kukata!
 
Sioni, tatizo kama walikubaliana ikatwe hiyo laki 5. Nafikiri, kulikuwa na kikao rasmi, sasa kama palepale hakuwa tayari, halafu akakubali, kisha, anakuja kuona haikuwa vyema bila shaka alikuwa mnafiki tu. Aende ambako hawakati pesa. Aende ambako mambo yamekuwa shwari, kiasi kwamba wakulima na wafanyakazi hawalalamiki. Aende tu ambako, wafanyabiashara wana amani pia. Aende tu, ambapo watu hawapigwi hela. Lakini asisahau kuwa sababu alizotoa ni kazitoakwakuwa ni lazima uwe na sababu, unapoamua kuighiribu jamii.
Tatizo siyo kukatwa ila ni njisi gani pesa zilizokatwa zinatumika, wabunge wengi wa Chadema hawariziki na matumizi ya pesa zinazokatwa wanaona zinatafunwa tu na mwenyekiti wa chama kinyume na lengo lililokusudiwa tangia mwanzo.
 
Nadhani hii ni sababu kuu na ndiyo inayowafanya wengi kukimbia.Maana ubunge ni kazi kama kazi nyingine Sasa kama kazi hiyo ina makato mengi wakati kuna sehemu makato hayapo lazima wabunge watakimbia.Huenda Ruzuku inatunzwa Kwa ajili ya uchaguzi 2020 lakini pia kuwakamua sana wabunge kunawarudisha nyuma
Mkuu kwa mawazo yangu naona kama anasema wabunge wa hicho chama wanakatwa laki tano 500,000 kila mwezi na hamjui matumizi yake kwa nini msihoji mpambanaji wa kweli hakati tamaa kukimbia sio suluhisho
 
Daah tena na tena. Basi ifike wakati jamani hawa wabunge watumie tu angalau busara wangesubiri mwaka 2020 wahame vyama kama kweli si suala la maslahi ya watu binafsi. Ninachokiona mimi kwanza ni uharibifu wa fedha za umma kurudia uchaguzi, pili, CCM wanajitengenezea bomu la upinzani ndani kwa ndani (ni suala la muda). Wanadhani hii ina tija kwao kumbe ni hasara miongoni mwa wanachama. Na hawa wabunge wanaohama kwa kudhani ndio ngoma inogile kumbe wanajiharibia kwa kutumika kama nepi na kutoswa mbele ya safari. Yetu macho.
 
Back
Top Bottom