Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

BADO KUNA SWALI NAJIULIZA, HIVI MBOWE NI NANI KATIKA NCHI HII AWEZE KUFANYA MADUDU YOTE HAYO BILA KUCHUKULIWA HATUA. KAMA ALIKUWA ANAKATWA BILA RIDHAA YAKE, KWANINI HAKUSHITAKI KWENYE VYOMBO VVYA USALAMA
Mbowe alimficha Dereva wake Lissu tangu tukio lilipotokea eti ameathirika kisaikolojia. Jamaa ana figisu kibao. Kila kukicha anazidi kuachwa wazi kama vitumbua vya uswazi.
 
Mbowe alimficha Dereva wake Lissu tangu tukio lilipotokea eti ameathirika kisaikolojia. Jamaa ana figisu kibao. Kila kukicha anazidi kuachwa wazi kama vitumbua vya uswazi.
Hivi huyo Mbowe ni nani nchi hiii hadi afanye mambo ya ajabu kama hayo bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria?
 
C walipitisha maamuzi kwa pamoja km wajumbe anacholalamika ni nn?huyo mama hana shukrani hata chembe ameona laki 5 ina thaman kubwa kuliko ubunge wa zawadi aliopewa 2010.
undefinedswali ni hawa wanaohamia huku ccm,sisi makada tutawapisha wao ndo wangombee?,au baada ya kutoka tutawadump,
 
Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

P.
Acha kujitoa fahamu. Huyo aliinuliwa kutoka viti maalum mwaka 2010 /15 kadumu na ubunge miaka 5 kama kiti maalum hakuona huko ku twezwa? Ameona sasa ni mbunge wa jimbo na ameahidiwa miaka mingine mitano bwerere akanunulika. Kama siyo hivyo viti maalum nani angemfahamu huko kwa maccm? Haya aende akakutane na jiwe maana huwa hatwezi
 
Mbunge wa Babati Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Manyara na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Kanda ya Kaskazini Pauline Gekul amejivua uanachama wa Chadema, na kujiuzulu nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo usiku huu na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).
_
Gekul ametaja sababu mbili za kufanya maamuzi hayo. Ya kwanza ni chama kuwabebesha wabunge mzigo shughuli za ujenzi wa chama. Anasema kwenye chaguzi ndogo zote zilizofanyika Manyara alitoa fedha zake mfukoni kugharamia, na chama kilileta laki tano tu, licha ya kwamba kinapokea ruzuku ya zaidi ya milioni 300 kwa mwezi. Pili amesema ni kupigwa majungu na viongozi wenzie wa Chadema.!
View attachment 897234
View attachment 897236
View attachment 897240
Hivi wabunge viti maalum hawaoni hizo juhudi?
Natabiri kuwa baada ya bunge hili kuvunjwa kwa ajili ya uchaguzi nao wataunga mkono maana they will have nothing to loose.
 
Acha Ujinga
nenda kwenye mada husika
Laki tano kila mwezi za mbunge za nini na zinaenda wapi
Milion 300 kila mwezi zinaenda wapi
Hamna hata Banda la kuku!!
Mnashindwa kujiongoza Nchi hii mtaiongoza!!
Acheni ujinga wenu,chama kilianza kupata ruzuku ya milioni 300 baada ya uchaguzi mkuu uliopita? au ni baada ya uchaguzi mkuu uliopita? ,wakati mteja wenu anatumia pesa zake za mfukoni chama kilikuwa kinapata ruzuku ya kiasi hicho? Je CCM wamemrudishia pesa zake alizotumia kwenye uchaguzi ndiomaana kajiunga na CCM? Je hamuoni kuwa ni ujinga na upumbavu kuhurumia fedha ulizotumia kwa kitu ambacho ni kwa ajili ya faida yako mwenyewe na kushindwa kuhurumia mabilioni ya fedha za wananchi ambazo zingitumika kufanya kazi za maendeleo ya nchi badala yake zitatumika kwenye marudio ya uchaguzi?.
 
Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

P.
Pascal tunakuheshimu sana, katika hili la hamahama hamna sababu yeyote iwayo itamfanya mtu yeyote mwenye hata uelewa wa chini kuziamini sababu zinazotolewa na hawa malaya wa kisiasa. Kwa umri wako wapo wabunge wa ccm hata wamevunja ndoa zao za awali na kuoana wao kwa wao, ati huyu mama anakoenda ni salama sana! Upuuzi tu!. Hawa watu wanatia hasira, ni ubinafsi mkubwa sana. Kupoteza kiti cha upinzani kwa style hiyo inauma sana, kuna waliokuwa vilema, wamepoteza maisha kwa ajili yake leo anakuja na issue za gharama za kujenga chama kilichojengwa juu za roho za watu?. Watu wameuawa kwa kukijenga chama, kuna gharama zaidi ya hiyo?.Pascal kila mtu anajua serikali na chama tawala wameamua kuchagua njia haramu kuua upinzani wala usipoteze mda wako kutuchambulia. Siasa mufilisi njoo huku tutakurudishia ubunge wako..., imagine. Watanzania ni wapole sana ila Ipo siku hawataamini ni hawa tuliokuwa tunawachezea.
 
Kwa viunu, vibwagizo na mapambio...
Tunajenga viwanda na umoja wa kitaifa!!!
Wanaogopa nini kufuta vyama vya siasa ibaki fisiemu pekee?
 
Heri yake ajaogopa macho ya watu,wengine wasiogope macho ya watu wakishangaa deadline ishapita,kuunga mkono ni haki ya kikatiba
 
Acha kujitoa fahamu. Huyo aliinuliwa kutoka viti maalum mwaka 2010 /15 kadumu na ubunge miaka 5 kama kiti maalum hakuona huko ku twezwa? Ameona sasa ni mbunge wa jimbo na ameahidiwa miaka mingine mitano bwerere akanunulika. Kama siyo hivyo viti maalum nani angemfahamu huko kwa maccm? Haya aende akakutane na jiwe maana huwa hatwezi
Kumbe katokea Viti maalum.....du! Hana huruma huyu mama! Impact yake si viti maalumu vitapungua chadema? Hivyo kuwa na double impact!. Hawa malaya wa kisiasa hata mwalimu walimkera sana.
 
Mkuu huyu mama kaandika barua mwanana na imeshiba. Amedadavua mengi mno na kuwavua nguo viongozi wa CHADEMA kuanzia kulamba ruzuku, kugeuka TRA na kuwatoza PAYE wabunge na pesa kuliwa na mwisho juhudi za kuwatweza wakinamama!!!
Angalia vizuri mtiririko wa barua hii kisha angalia zilizopita utaona mtiririko umepangwa na mtu mmoja anachofanya ni kujaribu kuchomekea sababu ili ionekane tofauti lakini anashindwa kubadili paragrafu ili zisifanane.
 
Aliemfuata kwa wingi wa kura aendeleze gurudumu
Thubutu,Mheshimiwa alishasema ukienda vitani na ukateka silaha za adui yako na hapo hapo unaendelea kupigana nae utakachofanya hapo silaha za adui ulizoziteka basi unaanza navyo ivyo vifaa kumshambulia navyo,ndivyo wanavyofanya Ccm,
 
Back
Top Bottom