Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

Chongeni tena tuchukue mwingine
Sikushangai kwa jinsi unavyoshangilia ujinga huu na jinsi kodi za wananchi zinavyotumika vibaya kwa kisingizio cha chaguzi za marudio zisizo na tija na nikijumlisha na hii avatar yako upo sahihi! Na usichojua ni kwamba nickname husadifu personality ya mwenyenalo!
 
CHADEMA kuna matatizo makubwa sana ya kimuundo na kiuongozi. Ukishaona wabunge wa kuchaguliwa wanahama kila siku, usikimbilie kudai wananunuliwa; no! hayo ni mapungufu kwa chama.Kuna watu waliohama CCM kwenda CHADEMA lakini CCM haikulalamika kuwa wananunuliwa; tena wengine walikuwa ni wazito sana- Lowassa na Sumaye. CHADEMA jichambueni tena la sivyo itakuwa kama stori ya NCCR-Meguzi.
 
Yaani wewe ndiye umetoa pumba kabisa kwa kuwa hakuna niliposema kuwa kuendesha uchaguzi ni faida ya mbunge,bali nilichomanisha ni kwamba ubunge ni kazi kama kazi nyingine yoyote ile ambapo mbunge analipwa mshahara kwa ajili ya matumizi yake binafsi na familia yake na hawagawii wapiga kura wake, anapewa gari ya kutembelea na mwisho wa ubunge wake anapewa kiinunua mgongo yeye kama yeye.

Na bado kuna wabunge waliokuwa kwenye nyazifa mbalimbali kama wakuu wilaya wakuu wa mikoa nk waliachia nyazifa zao nakwenda kutafuta ubunge,kibaya zaidi wengine wamepata ubunge kwa kuhonga, je ninani ambaye anaweza akaachia ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa au nafasi yoyote iliyokuwa inamuungizia kipato na kwenda kutafuta ubunge kwa gharama yake ambao anajua kuwa hauna faida kwake?.
 
Sawasawa,Mungu yupo anayaona haya malipo yapo tena Kwa pande mbili zote.
Poleni watumishi, Poleni watanzania.Maisha yenu yatabaki hivo milele
Bila kuwa na katiba itakayo mhakikishia mtu uhuru wa kusema kile anacho kiamini bila hofu, maendeleo ktk nchi hii yatakuwa ndoto.
 
Afadhali huyu ni MALAYA kama wale wa kimboka, wanaoshangaza ni kina baba kujiuza
Kwa nini umamuita malaya? Huna nidhamu wewe. Hujui aliekuzaa wewe pia ni mwanamke? Nae ni malaya? Huna akili na ushike adabu yako.
 
Kumbe ww ulikuwa CDM kwa ajili ya maslahi binafsi na sio maslahi mapana ya watu wa Manyara. Kutumia pesa zako kwa wapendwa wako ni dhambi? Huko green house umefata fedha ili ugawane na wana Manyara au utasweka tumboni mwako tu? Ndio maana Africa ni imebaki nyumba sababu ya watu kama ww. Haya wahi dera lako Lumumba.
 
Nitaamini kitu kimoja tu kama huyu mbunge kweli hajahama kwa kuadiwa mshiko. Pale chama tawala watakapo muacha na kumuweka mgombania mwingine. Hiyo ni njia nzuri chama tawala kujisafisha kwamba haihusiki na kununua wabunge wa upinzani!
 
Sababu alizozitoa hazina mashiko kamwe. by the way unatokaje upinzani na kujiunga na ccm? chama ni imani.hivi unaacha uislamu kisa umepigwa majungu na viongozi wa msikiti? hawa ndo wabunge wetu. ni hasara. wabunge wa namna hii wako pande zote ccm na upinzani. kwao siasa sio misngi bali kuvuna mahela.
 
Kifupi wanalipia ushuru kwakuwa wabunge kupitia CHADEMA!
Hii ni kali kama ni kweli.
Kama wamefikia hatua hii, basi hakuna chama tena hapo!

Ni vigumu kwangu kuwaamini moja kwa moja hao wabunge wanaoondoka sasa hivi ndani ya chama kwa sababu mbalimbali. Lakini inaelekea CHADEMA nao wanachangia kurahisisha kuondoka kwa hao wabunge.
 
Ndani ya Chadema kuna wabunge wengi tu wamekuwa kama samaki , wanamengi ya kusema ndani ya chama ila mdomo umejaa maji, hii ndio njia pekee na ukisema ndani ya chadema utaambiwa msaliti au mamluki, mwenyekiti hamuamini mtu kumpokea kiti hiyo ndiyo demokrasia? kama ndio hivyo wakina Mtei wangeng'ang'ania ingekuwaje? , na bado wakina Suzani Lyimo na wenginewe ndio wakati huu mlioelemewa na mizigo kuja kufanya demokrasia ya kweli kwa ajili ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…